Faru John aliondolewa Ngorongoro kwa ukorofi - wahifadhi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
FARU JOHN ALIONDOLEWA NGORONGORO KWA UKOROFI - WAHIFADHI

Sakata la kuondolewa kwa faru mweusi anayeitwa John kutoka Creta ya Ngorongoro, limechukua sura mpya baada ya kuelezwa kuwa aliondolewa kutokana na ushauri wa kitaalamu wa taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii.

Juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliituhumu menejimenti na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Baraza la Wafugaji (NPC) kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la Faru John ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh200 milioni kwenye Hoteli ya Grunet iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh100 milioni.

Alisema anataka kumuona faru huyo, nyaraka za kumuhamisha na kama amekufa, basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisema ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.
Faru huyo ambaye alizaliwa mwaka 1978 na wazazi wanaoitwa Betty aliyefariki mwaka 1992 na Hamisi (1991), alihamishwa Creta ya Ngorongoro Desemba 17 mwaka jana.

Faru John anaelezwa kuwa alikuwa amehodhi majike yote ya creta hiyo kutokana na ubabe wake na anadaiwa alikufa baada ya kupelekwa Serengeti eneo la Sasakwa Grumeti katika mazingira yenye utata.

FB_IMG_1481193004891.jpg
 
Hii ni sinema ukiona ivyo ujue kwamba hakuna FARU wala PEMBE zake hapo hapa sasa ni watu kushitakiwa maana wamezoea kusema uongo huku wakijinufaisha na kutunisha mifuko yao. Kwa ufupi ni kwamba wajiandae kisaikolojia kwenda jela muda wa kuibiana mali asili umekwisha sasa. Wao watajane walio kula dili hilo
 
Hii ni sinema ukiona ivyo ujue kwamba hakuna FARU wala PEMBE zake hapo hapa sasa ni watu kushitakiwa maana wamezoea kusema uongo huku wakijinufaisha na kutunisha mifuko yao. Kwa ufupi ni kwamba wajiandae kisaikolojia kwenda jela muda wa kuibiana mali asili umekwisha sasa. Wao watajane walio kula dili hilo
sidhani kama wataenda jela! sana watahukumiwa kulipa faini Tshs.20,000/=
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom