Faru John aliondolewa Ngorongoro kwa ukorofi - wahifadhi


Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,162
Likes
20,178
Points
280
Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,162 20,178 280
FARU JOHN ALIONDOLEWA NGORONGORO KWA UKOROFI - WAHIFADHI

Sakata la kuondolewa kwa faru mweusi anayeitwa John kutoka Creta ya Ngorongoro, limechukua sura mpya baada ya kuelezwa kuwa aliondolewa kutokana na ushauri wa kitaalamu wa taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii.

Juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliituhumu menejimenti na wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Baraza la Wafugaji (NPC) kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la Faru John ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh200 milioni kwenye Hoteli ya Grunet iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh100 milioni.

Alisema anataka kumuona faru huyo, nyaraka za kumuhamisha na kama amekufa, basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisema ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.
Faru huyo ambaye alizaliwa mwaka 1978 na wazazi wanaoitwa Betty aliyefariki mwaka 1992 na Hamisi (1991), alihamishwa Creta ya Ngorongoro Desemba 17 mwaka jana.

Faru John anaelezwa kuwa alikuwa amehodhi majike yote ya creta hiyo kutokana na ubabe wake na anadaiwa alikufa baada ya kupelekwa Serengeti eneo la Sasakwa Grumeti katika mazingira yenye utata.

fb_img_1481193004891-jpg.443846
 
PRODA LTD

PRODA LTD

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2016
Messages
1,005
Likes
1,305
Points
280
PRODA LTD

PRODA LTD

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2016
1,005 1,305 280
Hii ni sinema ukiona ivyo ujue kwamba hakuna FARU wala PEMBE zake hapo hapa sasa ni watu kushitakiwa maana wamezoea kusema uongo huku wakijinufaisha na kutunisha mifuko yao. Kwa ufupi ni kwamba wajiandae kisaikolojia kwenda jela muda wa kuibiana mali asili umekwisha sasa. Wao watajane walio kula dili hilo
 
py thon

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Messages
2,479
Likes
4,269
Points
280
Age
49
py thon

py thon

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2016
2,479 4,269 280
Naona maelezo yako hayajaeleweka mara hamisi mara john hebu tupe report kamili
Soma pole pole ttzo tunasoma kwa kuruka ruka au juu juu

Alizaliwa mwaka 1978

Wazazi wake Betty na hamisi

Betty alifariki=1992
Hamis alifariki=1991
 
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
3,996
Likes
4,538
Points
280
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
3,996 4,538 280
inasikitisha sana, hii nchi, na tayari walishapiga kimya, najiuliza asingesema waziri mkuu, sijui ni nani angegundua huu mchezo, sasa kama hawakumuuza hizo mil mia ya kwanza ilikua ya nini?
 
L

legend jemedari

Senior Member
Joined
Sep 7, 2013
Messages
171
Likes
193
Points
60
L

legend jemedari

Senior Member
Joined Sep 7, 2013
171 193 60
Watoe nyaraka za transfer zilizohitajika, sio kwa maneno tu na tunahitaji kumuona faru wetu vinginevyo wawajibishwe bila kupepesa macho
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,791
Likes
27,954
Points
280
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,791 27,954 280
Hii ni sinema ukiona ivyo ujue kwamba hakuna FARU wala PEMBE zake hapo hapa sasa ni watu kushitakiwa maana wamezoea kusema uongo huku wakijinufaisha na kutunisha mifuko yao. Kwa ufupi ni kwamba wajiandae kisaikolojia kwenda jela muda wa kuibiana mali asili umekwisha sasa. Wao watajane walio kula dili hilo
sidhani kama wataenda jela! sana watahukumiwa kulipa faini Tshs.20,000/=
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,791
Likes
27,954
Points
280
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,791 27,954 280
Kuna watu toka juzi hawaja lala, ama wapo kwa waganga au BP zipo juu sana.
Na ukiona Majaliwa ameliongea hilo kwa kujiamini ina maana amepewa mtonyo wote ana taarifa hadi za uvunguni hivyo wajitahidi tu kuwa wakweli
 
Y

Yaleyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Messages
1,326
Likes
1,193
Points
280
Y

Yaleyale

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2011
1,326 1,193 280
Sasa Betty na Hamisi ndiyo waliompa jina la John? Vipi John yeye hakuoa na kama aliona mke wake ni nani maana naona umeeleza kuwa alihodhi majike yote, hiyo ni kusema alikuwa John alikuwa mhuni?
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,791
Likes
27,954
Points
280
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,791 27,954 280
Soma pole pole ttzo tunasoma kwa kuruka ruka au juu juu

Alizaliwa mwaka 1978

Wazazi wake Betty na hamisi

Betty alifariki=1992
Hamis alifariki=1991
Faru waliona mkristu (Betty) ambaye bila shaka ni Elizabeth na Muislamu Hamisi, but mtoto akabakia kwenye ukristu (John)
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,214
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,214 280
Na ukiona Majaliwa ameliongea hilo kwa kujiamini ina maana amepewa mtonyo wote ana taarifa hadi za uvunguni hivyo wajitahidi tu kuwa wakweli
Kuna bwana amehamishiwa huko kutoka mkoa fulani hana hata wiki 3, yule huwa hakosei hata kidogo. Amehamia tu hata wiki hajaisha nikasikia ziara ya PM nikajua hapa tayari.
 

Forum statistics

Threads 1,273,063
Members 490,259
Posts 30,469,410