Faru akipotea, anatafutwa kama Malaika, ila wananchi wakifa katika mazingira tata, kudhulumiwa, tunasema wahusika hawajulikani, seriously

T308A

Member
Aug 23, 2019
16
12
Nilikua najaribu kutafakari, maana halisi ya neno maarufu sana hivi karibuni, la "VITA YA KIUCHUMI". Huu msemo umekuwa maarufu sana, na mara nyingi naona hutumika kama kinga kwa baadhi ya watu, dhidi ya uharamu wa mambo yao.

Kwa uelewe wangu wa kawaida, vita ya kiuchumi, ni competition on resources and markets. Kila nchi inataka kuwa juu ya mwenzake, kwa mbinu zozote zile na mara nyingine, hata kwa figisu.

Lakini, bado sijaona nchi ya kupambana na Tanzania, yaan mbavu za nchi yetu bado ni teta katika hii vita. Na kama ni vita, adui yetu ni nani, katika biashara ipi. Na cha kushangaza, zaidi ya resources ambazo tunazo asilia, kwa neema ya Mungu, sioni kitu kikubwa cha maana, ambacho kama Tz imeshakifanya, cha kutishia mataifa mengine.

Hii naona ni vita, kati ya matamanio ya Nchi na uwezo wetu wa kufikiria, ni kwa namna gani tunaweza kufikia malengo hayo. Kama tunaamini, kuwa na vyerehani 3 ni kiwanda, ndani ya miaka 2, nchi kujenga viwanda zaidi ya 2500, ambavyo, hatujui viko wapi, vinazalisha nini, watumishi wake ni akina nani.

Nchi ambayo sifa za kuwa kiongozi ni kuwa na umri wa 18, kujua kusoma na kuandika na akili timamu, shule kwetu haina maana. Nchi ambayo, tunawapeleka vijana jeshini kwa mujibu wa sheria, kwa miezi mitatu, eti kuwafanya kuwa wazalendo, yaan uzalendo with in 3 months,seriously..!! na bado wananyimwa mikopo vyuoni.

Watu wenye elimu za PhD na Profs, wanapangiwa nini cha kufanya katika taaluma zao, na watu wasio wa taaluma husika, kwa sababu za kisiasa tu, ina maanisha hata wasomi wetu hawaaminiki na kuthibitisha kwamba, hatuiamini hata elimu tuliyo nayo, na bado tunaipigia debe iendelee kutolewa.

Wanasheria wa serikali, wanakesha kupambana na Lissu, lakini kuishauri serikali katika mikataba inayoingia, sera zisizokuwa na mashiko na zilizopitwa na wakati, kwetu sisi hapana. Watu wanaamini ujenzi wa barabara tu, ni zaidi ya miujiza, ambayo Jesus aliwafanyia wana wa israel.

Nchi ambayo haieleweki inataka nini, kwa sababu gani na kwa muda gani. Mara kilimo, mara viwanda, sijui atayekuja nae, ataleta nini. Yaan tunagusa gusa tu vitu na hatuna hata dira ya Taifa, inayoeleweka.

Tuko ovyo katika problem solving techiques (tunaona viongozi, wanayoyafanya, pale changamoto zinapoibuka), hatuna analysis ya yale yalikuwa yamepangwa, poor in designing and mobilizations, hasa kwa resources (ni aibu, Taifa lenye misitu, na bado wanafunzi wanakaa chini). Tunawajali wanyama pori, kuliko hata tunavyowajali Raia.

Yaan, Faru akipotea, anatafutwa kama Malaika, ila wananchi wakifa katika mazingira tata, kudhulumiwa, tunasema wahusika hawajulikani, seriously....!! Nchi ambayo, watoto wake, hufunzwa uoga na kutii bila kuhoji, eti ndio uzalendo
MCHAWI MKUBWA WA MAENDELEO YA TANZANIA, SIO WATANZANIA, NI UJINGA NA UFINYU WA MAWAZO KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO NA KUTUMIA RASILIMALI TULIZONAZO KWA MAENDELEO YA TAIFA, NA SIO HABARI ZA AKINA FULANI, WANAZUIA MAENDELEO.

Lazima tukubali, maendeleo yanahitaji akili kubwa, na sio ukubwa wa mwili au cheo.
 
Sure huyu jamaa anatumia kichwa cha habari vita ya uchumi huku hajui maana yake kabisa,tumemwamini kuendesha gari letu lakini hatimaye atatuangusha
 
Vita ya kiuchumi is misused and overrated phenomenon..!!

Our fascist leader uses it as camouflage to supersede democracy in favor of totally exercising executive power.
 
Back
Top Bottom