'Farouk Tech' inawafaa wengi hapa nchini kukomesha wizi: Mwizi akutwa amelala ndani ya gari

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Mwizi kaingia kwa Muandishi wa Habari Farouk Karim usiku wa kuamika leo Jumapili akaiba nguo na viatu na akaingia kwenye gari ya Farouk akachukua power window lakini hakuondoka tena akalala hapo hapo hadi asubuhi ya leo, wenyewe wakamgundua na kuja kuchukuliwa na Jeshi la Polisi.

Farouk hii Teknolojia ulotumia naiomba nzuri sana, duh kaganda hapo hapo!

---

Farouk anena kwamba kumuomba Mungu akulinde ndiyo silaha muhimu

Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim, amesema kuwa siri kubwa ambayo mtu yeyote anaweza kuifanya ili wezi watakapofika nyumbani kwake waibe lakini wapitiwe na usingizi hapo hapo ni kumuamini na kumuomba Mungu ili awalinde wote ndani ya familia.

Mwizi aliyekutwa ndani ya gari la Mwandishi wa Habari wa ITV Zanzibar, Farouk Karim.

Farouk ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020, wakati wa mazungumzo mubashara kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na ndipo aliposimulia mkasa wake baada ya mwizi kuruka geti la nyumba yake huko Fuoni visiwani Zanzibar na kuiba nguo na viatu lakini baadaye aliingia ndani ya gari na kupitiwa usingizi.

"Huyu mwizi kaingia usiku wa manane karuka geti, na hatuna mlinzi pale nyumbani, kakusanya zile nguo zilizokuwa zimeanikwa kaziwekwa kwenye mfuko, katika magari yaliyokuwepo pale gari moja lilikuwa wazi akaingia, akapitia mlango wa abiria akachukua power window, akaenda upande wa dereva kuchukua power window ikamshinda ndiyo akalala hapo hapo" amesema Farouk Karim.

Akielezea siri ya mwizi kumuibia na kisha kupitiwa na usingizi Farouk amesema,"Tumempeleka Polisi kama ambavyo huwa tuna msindikiza Bi harusi, na ile kulala huenda kaiba sana hivyo karidhika, na dawa kubwa ya kumfanya mwizi alale ni moja tu kumuomba Mungu akulinde wewe na nyumba yako, na watu kama sisi ambao hatuna madhambi, Dua zinakubalika, kama unataka hiyo Dua nitafute inbox".



IMG-20200602-WA0003.jpg
IMG-20200602-WA0004.jpg
IMG-20200602-WA0005.jpg
IMG-20200602-WA0001.jpg
 
Kama anatumia ndumba kwenye ulinzi anashindwaje kutumia ndumba kwenye kazi ya utangazaji ili awe maarufu? Mtumia ndumba huyo
All in all kila mtu anatumia ndumba kwa namna tofauti kwenye kazi au popote pale. Kumsnitch mtu pia ili upate mchongo fulani na yenyewe ni ndumba tu .. tunaishi mulemule
 
Mwizi kaingia kwa Mwandishi wa Habari Farouk Karim akaiba nguo na viatu na akaingia kwenye gari yake akachukua power window lakini hakuondoka tena akalala hapo hapo hadi asubuhi,wenyewe wakamgundua na kuja kuchukuliwa na Polisi.



IMG-20200602-WA0001.jpg
IMG-20200602-WA0000.jpg

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 

Attachments

  • IMG-20200602-WA0002.jpg
    IMG-20200602-WA0002.jpg
    62.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom