FAO yaishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha nchi soko la Kimataifa

Siwezi kukubaliana na ushauri huu. Diversity ya ardhi, hali ya hewa hapa nchini inatoa furusa ya kulima mazao mbali mbali. Kwenye masuala ya nishati tunahimiza energy consumption mix ili kupunguza risks. Ni strategy hii pia inatakiwa itumike kwenye kilimo.
Hawana maana mazao mengine msilime,bali kuwepo na zao kiongozi kama vile cuba wanalima miwa siyo kwamba mazao mengine hawalimi.
Brazil kahawa,siyo kwamba mengine hawalimi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uelewa ulionao hata ashuke malaika hutoelewa.
Nimetumia lugha unayoielewa lakini 0
H ah haaaaa! Mkuu, umenichekesha kweli. Hata hivyo, nina wasiwasi kuna uwezekano swali limekuwa gumu kwako.

Labda nililegeze kigodo, yaani ninahitaji unitajie sifa za hili "zao la kipaumbele", kwa maani hili zao litakuwa na sifa maalumu zitakazolifanya linachukuliwe na serikali na hata wananchi kwa namna ya kipekee? mfano, ukilima zao hilo, serikali itakupa ruzuku za pembejeo, ukivuna kisha kuuza, hutakatwa kodi za miamala ya simu, utapata mkopo usio na riba benki, na ukisafirisha zao hili hutakatwa ushuru. Ukilima zao hili utapunguziwa tozo za kwenye miamala ya kibenk, hutalipa umeme wa Tanesco....nakadhalika na kadhalika.

Pia mifano mingine inayoweza kuwa sifa ya zao hili ni, litalazimika kulimwa msimu mmoja, ama miwili, na kuanzia muda fulani mpaka muda fulani kufit soko, litalimwa na mkulima atakayekuwa na eneo linaloanzia ekari kadhaa!

Najitahidi mkuu, unielewe ili malaika wasishuke.

Karibu.
 
Hahahaaaa........!
 
Shirika la Chakula duniani FAO limeishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha nchi yetu kwenye soko la kimataifa.

Chanzo: Radio One

My take; Pendekeza zao, binafsi Napendekeza Korosho
Tukikubali watatushauri tuwe na mbuga moja itakayotutambulisha kimataifa...waache ufyatu!
 
Kutegemea zao moja kwa la kibiashara sio wazo lenye afya ukizingatia volubility ya soko lenyewe , ushauri mzuri ungekua kufocus kwenye list ya mazao machache na kuwekeza nguvu kubwa huku. Na kitu cha msingi zaidi ni kuwa na kujenga uwezo wa kuchakata mazao ya kilimo hapa nchini na sio kuuza raw materials
 
Shirika la Chakula duniani FAO limeishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha nchi yetu kwenye soko la kimataifa.

Chanzo: Radio One

My take; Pendekeza zao, binafsi Napendekeza Korosho

=======

View attachment 1966827

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha Tanzania Kimataifa ili kuweza kupenya kirahisi katika soko la Kimataifa la mazao ya Kilimo.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Qu Dongyu alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo Roma, Italia.

Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa Tanzania ina mazao muhimu na mengi ya kilimo ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza pato la Taifa lakini changamoto kubwa ni namna ya kupenya katika soko la kimataifa kutokana na kukosa zao la utambulisho na kwamba Shirika hilo FAO iko tayari kusaidia ujuzi na kuijengea uwezo Tanzania kufikia lengo hilo.

View attachment 1966828

Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa kwa sasa FAO imeanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo.

Katika mazungumzo hayo Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Libearata Mulamula amesema Tanzania imeupokea ushauri wa FAO na kwamba itaufanyia kazi ili kuiwezesha Tanzania kutambulika na kunufaika katika soko la Kimataifa la mazao ya kilimo ili kuwawezesha wakulima kujikomboa kiuchumi kwa kuongeza pato la kaya na hivyo kuinua uchumi wa Tanzania.

Ameongeza kuwa Tanzania imejipanga kikamilifu kunufaika na mpango wa Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Matiafa (FAO) wa kuanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo

View attachment 1966829

Balozi Mulamula yuko Roma, Italia kushiriki Mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Italia pamoja na kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa amani.
Nadiliki kusema huo ushauri ni wakisenge sana tz ni nchi kubwa kwanini zao moja tunatakiwa kutambulika kwa mazao mengi kwa kadili iwezekanavyo
 
THANK YOU 🙏🏾 Akili kubwa hii.

Waende zao hapa!! Enzi za Mwalimu Nyerere tulikuwa na Pamba,Kahawa,Mkonge ,Chai na Muhogo kama Exports.Na tulikuwa Vizuri sana .Sasa hivi Wanaotuangusha ni Wanasiasa .Kama wakiwa makini Tanzania tutarudi no 1 kwenye export za mazao ya Kilimo
 
Back
Top Bottom