FAO yaishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha nchi soko la Kimataifa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
49,320
2,000
Shirika la Chakula duniani FAO limeishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha nchi yetu kwenye soko la kimataifa.

Chanzo: Radio One

My take; Pendekeza zao, binafsi Napendekeza Korosho

=======

f2_0.jpg


Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika zao moja la kilimo litakaloitambulisha Tanzania Kimataifa ili kuweza kupenya kirahisi katika soko la Kimataifa la mazao ya Kilimo.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Dkt. Qu Dongyu alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula(Mb) mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo Roma, Italia.

Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa Tanzania ina mazao muhimu na mengi ya kilimo ambayo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza pato la Taifa lakini changamoto kubwa ni namna ya kupenya katika soko la kimataifa kutokana na kukosa zao la utambulisho na kwamba Shirika hilo FAO iko tayari kusaidia ujuzi na kuijengea uwezo Tanzania kufikia lengo hilo.

f4.jpg


Dkt. Qu Dongyu ameongeza kuwa kwa sasa FAO imeanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo.

Katika mazungumzo hayo Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Libearata Mulamula amesema Tanzania imeupokea ushauri wa FAO na kwamba itaufanyia kazi ili kuiwezesha Tanzania kutambulika na kunufaika katika soko la Kimataifa la mazao ya kilimo ili kuwawezesha wakulima kujikomboa kiuchumi kwa kuongeza pato la kaya na hivyo kuinua uchumi wa Tanzania.

Ameongeza kuwa Tanzania imejipanga kikamilifu kunufaika na mpango wa Shirika la chakula na Kilimo la Umoja wa Matiafa (FAO) wa kuanzisha jukwaa maalum la kuwawezesha wanawake na vijana kunufaika na sekta ya kilimo kutokana na utafiti kuonesha kuwa wanawake wengi katika nchi zinazoendelea wanajihusisha na kilimo

f4.jpg


Balozi Mulamula yuko Roma, Italia kushiriki Mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Italia pamoja na kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa amani.
 

Chipukizi

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
3,068
2,000
Waende zao hapa!! Enzi za Mwalimu Nyerere tulikuwa na Pamba,Kahawa,Mkonge ,Chai na Muhogo kama Exports.Na tulikuwa Vizuri sana .Sasa hivi Wanaotuangusha ni Wanasiasa .Kama wakiwa makini Tanzania tutarudi no 1 kwenye export za mazao ya Kilimo
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
18,452
2,000
Siwezi kukubaliana na ushauri huu. Diversity ya ardhi, hali ya hewa hapa nchini inatoa furusa ya kulima mazao mbali mbali. Kwenye masuala ya nishati tunahimiza energy consumption mix ili kupunguza risks. Ni strategy hii pia inatakiwa itumike kwenye kilimo.
 

Kingtox

Senior Member
Sep 13, 2021
185
250
Haina maana kuwa ukiwakilishwa na zao moja huruhusiwi kufanya biashara na mazao mengine

Maana ya wazo hili ni kwamba nchi Kama nchi iwe na zao la kipaumbele

Kwa mfano mnalima mazao yote lakini linakuwepo zao moja linaloitambulisha nchi kimataifa

Kama vile Marekani ni maarufu kwa kilimo cha mahindi duniani haina maana ya kwamba hawafanyi biashara katika mazao mengine
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
49,320
2,000
Siwezi kukubaliana na ushauri huu. Diversity ya ardhi, hali ya hewa hapa nchini inatoa furusa ya kulima mazao mbali mbali. Kwenye masuala ya nishati tunahimiza energy consumption mix ili kupunguza risks. Ni strategy hii pia inatakiwa itumike kwenye kilimo.
Wamesema zao la kipaumbele!
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,415
2,000
Haina maana kuwa ukiwakilishwa na zao moja huruhusiwi kufanya biashara na mazao mengine

Maana ya wazo hili ni kwamba nchi Kama nchi iwe na zao la kipaumbele

Kwa mfano mnalima mazao yote lakini linakuwepo zao moja linaloitambulisha nchi kimataifa

Kama vile Marekani ni maarufu kwa kilimo cha mahindi duniani haina maana ya kwamba hawafanyi biashara katika mazao mengine
Una akili sana. Bravo. 🙏 🙏 🙏
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom