FAO LA KUJITOA! Rais Sema neno vijana wapate kujiajiri

Mh rais asithubutu kuruhusu FAO la kujitoa, vinginevyo tutakuwa na janga la wazee wasio na kitu miaka 10 ijayo.

Taifa litakuwa na mzigo mkubwa Sana wa kulea wazee miaka 10 ijayo.

FAO maana yake ni fedha ya kumlinda mtu atakapokuwa mzee. Kujitoa ni dhambi
Si kweli hata kidogo! Wabaki na asilimia 30 watoe 70, kufika miaka sittini si kazi rahisi na akili inakuwa ishachoka
 
Mh rais asithubutu kuruhusu FAO la kujitoa, vinginevyo tutakuwa na janga la wazee wasio na kitu miaka 10 ijayo.

Taifa litakuwa na mzigo mkubwa Sana wa kulea wazee miaka 10 ijayo.

FAO maana yake ni fedha ya kumlinda mtu atakapokuwa mzee. Kujitoa ni dhambi

walioajiliwa ni asilimia ndogo sana ya idadi ya watanzania waliojiajiri ambao hawana hizo pension... JE HAO WALIOJIAJILI WAKIFIKISHA 60yrs WANAMSUMBUA NANI?
 
Nchi ina mifumo ya hovyo sana hii kwa nn ulazimishe kumlipa mtu pension anapofikisha miaka 60
Kwa nn kusiwe utaratibu mtu akifikisha miaka zaidi ya 10 kazini iwe ni haki kuchukua asilimia fulani ya pesa alizowekewa na mwajiri wake.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
North Korea ni afadhali kuliko Tanzania
 
Mh rais asithubutu kuruhusu FAO la kujitoa, vinginevyo tutakuwa na janga la wazee wasio na kitu miaka 10 ijayo.

Taifa litakuwa na mzigo mkubwa Sana wa kulea wazee miaka 10 ijayo.

FAO maana yake ni fedha ya kumlinda mtu atakapokuwa mzee. Kujitoa ni dhambi
Unaishi nchi gani?
 
Kwajinsi wazee wanavyosumbuliwa na wengine kufa bila kupata fao lake bora upewe chako mapema!
 
Lengo syo kupewa pesa ukiwa na nguvu bali kupewa pesa pale nguvu zinapokua hakuna zikusaidie
Mna uhakika gani kama nitafika hiyo miaka 60? Hii sera nzima ya mifuko ya jamii imekaa kinyonyaji zaidi hasa kwa watu ambao hawajaajiriwa na serikali.
Mtu unapata kazi kwenye kampuni flani, baada ya miaka kadhaa kampini linafunga operarions zake na kuondoka na hapo wafanyakazi wote mnajikuta jobless. Kwanini wasipewe chao wakaanza kupambana kivingine?
 
Waasalam,

Mada za fao la kujitoa sio ngeni hapa jukwaani. Mei mosi ndio siku MH SSH atazungumza na taifa hasa masuala ya ajira, kujiajiri na mustakabali mzima wa taifa hili kwa hali ya sasa ambapo maisha yamepanda ghafla.

FAO LA KUJITOA linaweza kuwa suluhu ya vijana kujiajiri. Hii ni mitaji yao, kama tukirudisha sera ya hili fao, nina imani kwa kiasi fulani vijana baadhi watatumia kama mitaji na kuanzisha biashara ambazo nao wataajiri vijana wengine.

Ni lazima serikali iwafikirie “wawekezaji” hawa ambao mitaji yao inakaa NSSF pasipo kuwanufaisha na inachochea rushwa kwani kupata hata kiasi kidogo cha pesa hii ni lazima afisa apewe pesa ili “mchongo” ufanyike. Yaani pesa ya kwako na kuipata lazima utoe rushwa kwa mtu wa kati ambaye ni muajiriwa wa serikali.

Fao hili ni muhimu sana, kwani hata kwa wenzetu watu wana “cash out” mafao yao na kufungua miradi. Kwanini hapa ambapo ujira ni mdogo na kazi zenyewe hazina security nzuri tusiweze ku-cash out mafao yetu?

Nawasilisha!
Hili jambo kwangu ni la muhimu sana.
 
Eti hoja wanayotumia kuwanyima fao hili la kujitoa ni kwamba wanaku- cover usje kusumbua watu uzeeni!
Nauliza wale ambao hawana ajira huko uzeeni nani atawa- cover ili wasisumbue watu?!
Private sector unapoachishwa ajira au Mkataba unapoisha ndio Tayari umestaafu! Sasa hiyo miaka 60 wanayokusubirisha ni Kwa ajira ipi!? Hii miaka 60 ni Kwa watu pensionable, ambao ukiajiriwa tayari unauakika WA ajira hadi ufike miaka 60, Tuje Kwa ndugu zetu wanasiasa wao wanajiwekea Mazingira mazuri na wanajisemea Sio ajira ya Kudumu!! Sasa Kwa nini watu wenye ajira za kuunga unga (private sector) haiwi hivyo!? Ndio dhuluma inapoanzia!!
 
Tupe mfano wa nchi inayofanya kama unavyofikiri
Sasa kama wanaweza kumgarantii mtu ajira hadi miaka 60 Watuambie, Kwani Naona kama miujiza na uonevu kumshikia mtu Hela zake huku Hana ajira yenye uhakika
 
Halafu wabunge wakimaliza miaka 5 wanapewa halafu wengine eti mpaka wazeeke, huu ni uonevu.
 
Wakianza kulipa vijana fao la kujitoa mifuko itakosa hela ya kujiendesha, inabidi malipo yawe mpaka mfike miaka 60 ili kupunguza uwezekano wa kulipa watu hela kwa sababu:
  • Kuna wengine watachangia na kufa kabla ya kuanza kulipwa.
  • Kuna wengine watacheleweshwa kupewa mafao ili wapate stress na kufa.
  • Wale watakaofanikiwa kulipwa mafao yao tunategemea baada ya muda mfupi wapo watakao kufa.
Kiufupi kinachotoka kwenye mfuko lazima kiwe kidogo kulinganisha na kinachoingia. Mojawapo ya risk kubwa kwa mifuko ya hifadhi za kijamii ni high longevity (wanachama wengi kuendelea kuwa hai)
 
Mkuu UMESHIBA tuwache wenye njaa TUDAI HAKI YETU
Njaa haiondoshwi na visenti vya NSSF. Kama umeshindwa kujitafutia na kukuza mtaji mwenyewe mpk unatamani upewe hela ya NSSF, ni dhahili kuwa hata ukipewa hiyo ya NSSF itapotea tu. Kisha utapigika Tena.
 
walioajiliwa ni asilimia ndogo sana ya idadi ya watanzania waliojiajiri ambao hawana hizo pension... JE HAO WALIOJIAJILI WAKIFIKISHA 60yrs WANAMSUMBUA NANI?
Hao wamejijengea uwezo wa kupambana ndiyo maana huwasikii wakililia chochote toka serikalini tangu ujana wao.

Wasomi ni tatizo tangu ujana mpk uzee wao. Ujanani wanapiga kelele kuhusu ukosefu wa ajira na FAO la kujitoa. Ukiwapa FAO la kujitoa uzeeni wanashindwa kujikimu. Wasomi ni janga nchi hii.
 
Hii ndio sababu kubwa na konki inayochelewesha maendeleo ya nchi hii.

Hata muumba mwenyewe anachoka kutushangaa kabisa...
Siku zote mtu anaeshiba hawezi kukutetea mwenye njaa. Inabidi ujitetee mwenyewe. Bahati mbaya Tz wenye njaa wanategemea aliyeshiba awatetee.
 
Back
Top Bottom