Fao la kujitoa: Nimeamini kweli Zitto Kabwe anauma na kupuliza !

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Haya kile kilio chetu wafanyakazi kumbe yupo yule anayezidi kukipigilia misumali

Sina mengi nyie wenyewe mtaamua kama huyu kijana ni mtu mzuri

mmeshindwa kurudisha pesa zilizo kwenye mabenki ya nje bado mnataka hela zetu


Source :The Citizen Friday|By Zephania Ubwani


The Citizen Bureau Chief Arusha. Stakeholders at a meeting here have warned that pre-mature withdrawals from social security schemes could end up strangling the funds.The trend by members opting out could also impact on the economy as it may be necessary to increase taxation in order to manage paying pensioners whose number keeps rising.

"If we allow withdrawals there would be no social security in the country", warned the Kigoma North MP (Chadema) Zitto Kabwe in his presentation at the stakeholders conference of the National Social Security Fund (NSSF). He wondered what the fate of thousands of social security members would be after retirement if they were to be encouraged to withdraw their benefits while still working and how the pension funds would operate profitably.

The outspoken opposition legislator cautioned that the social security schemes in Tanzania were still fragile and that proposals to allow total withdrawals should be discouraged for the time being. "We are at a crossroads," he cautioned, noting that although some people favoured voluntary withdrawals, there were dangers both to the pensioners and the country's economy.

The MP -- who until recently chaired the disbanded Parliamentary Parastatal Organisations Accounts Committee (Poac) -- further warned that the pension sector would face serious crises in future due to a myriad of problems. He observed that many people were opting out of the social security schemes because of the little trust they have in them, as funds use the money to invest in areas that do not seem to benefit members in tangible ways.

Despite the myth held by many people, the social security bodies combined injected only 22 per cent of their investments in commercial buildings, which have shorter pay-back periods. The rest is invested in Treasury Bills and Bond and financing of mega government projects whose returns take a long time. He cited the government financing of construction of universities, saying the flow of recovered funds for the loans extended was slow.

Mr Kabwe challenged the social security institutions to direct their investments to projects which would create employment. This will not only spur economic growth but also increase membership.


Kigoma North MP (Chadema) Zitto Kabwe

==========================================
Mjadala wa Zitto Kabwe juu ya mada aliyotowa akiwa Arusha
==========================================


Hifadhi ya Jamii njia panda: Madhara ya kujitoa kwenye mafao[1]


Inafahamika kuwa mfumo wa mafao ya uzeeni ni moja ya bima ndani ya mfumo mzima wa hifadhi ya jamii duniani.Madhumuni makuu ni kuzuia mtu kupoteza kabisa kipato na kulinda dhidi umasikini katika uzee, ulemavu na kifo (kwa wategemezi).

Kwa upande wa Tanzania pensheni hufadhiliwa kwa mfumo wa kwamba wafanyakazi wa leo wnanalipia pensheni wafanyakazi wa zamani. Pamoja na kwamba hapa nchini kuna mfumo wa ‘provident' lakini pia mafao ya wachangiaji yamewekwa kwenye sharia kabisa. Katika kama za Ulaya, kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wazee kuliko vijana kuna mijadala mikali ya kufanya mageuzi makubwa kwenye mfumo wa hifadhi ya jamii. Mwaka 1991 Sweden walifanya mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo wa Pensheni ambapo licha ya mafao kujilikana, lakini pia michango ya wanachama inapaswa kuendana na hayo mafao.

Nchi nyingine za Ulaya zinaanza kuiga mabadiliko yaliyofanywa huko Sweden. Hapa nchini kwetu hivi sasa kuna changamoto kubwa ya wananchi kutaka kujitoa kwenye mafao (kama inavyoitwa ‘fao la kujitoa') na wengi ni vijana wenye uwezo wa kufanya kazi sasa. Hatari iliyopo ni kwamba huko mbele watakapokuwa wamezeeka hapatakuwa na namna ya kuwapa hifadhi ya jamii tofauti na kuongeza kodi zaidi kupata fedha za kuhudumia wazee.

Kwanza jambo la msingi (fundamental) la kufahamu ni kwamba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hifadhi ya jamii ni haki ya kikatiba. Lakini pia hifadhi ya jamii ni wajibu wa kila raia. Hivyo Bunge lilitunga sheria mbalimbali ili kuwezesha haki na wajibu huu wa hifadhi ya jamii kutekelezwa. Mjadala wowote wa hifadhi ya jamii lazima pia uzingatie hitaji hilo la kikatiba la haki na wajibu.

Kutokana na hali hiyo ndio maana baadhi ya wabunge wamekuwa wakiisukuma Serikali kuanzisha pensheni ya lazima kwa wazee wote nchini. Wazee hawa wawe wamechangia au hapana wapate kiasi kidogo cha fedha kuwezesha kukidhi haja Fulani Fulani za maisha ya kila siku. Hivi sasa kuna wazee 2.4 milioni nchini ambao hawana mfumo wowote wa hifadhi ya jamii.

Wadau mlipo hapa pia mjue hivi Tanzania ni Taifa la watoto kwani asilimia 50 ya Watanzania wote wapo chini ya umri wa miaka 17. Vile vile asilimia 70 ya Watanzania hivi sasa wapo chini ya umri wa miaka 29 na asilimia takribani 63 wapo chini ya umri wa miaka 40. Hivyo kundi kubwa linafanya kazi hivi sasa (nguvu kazi ya nchi) ni dogo sana ambalo baada ya miaka 30 -50 ijayo kundi hili litakuwa ndio wazee.

Tunapojadili masuala ya hifadhi ya jamii ni lazima kama Taifa kuangalia kwa umbali huo. Lazima kujua maamuzi ya sasa yataathiri vipi uhai wa Taifa siku za usoni. Ni vema pia kujua kwamba, wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, mifuko yote, wapo 1.04 milioni pekee. Mjadala kimsingi unapaswa kuwa ni namna gani tunaongeza wanachama wa mifuko ili kufikia japo asilimia 10 ya Watanzania wote badala ya kujadili ni namna gani kuruhusu watu kutoka kwenye mfumo wa hifadhi ya jamii.

Ni vema pia niseme kwamba mfumo wa hifadhi ya jamii ni pembe tatu - Michango, uwekezaji na mafao. Ni lazima kuwe na wachangiaji ambao fedha zao zitawekezwa kwa ajili ya kutunza thamani ya fedha na kuongeza shughuli za kiuchumi ili kuongeza wachangiaji na kasha kulipa mafao ya wanachama. Mafao ni pamoja na yale ya bima ya afya, ulemavu, kujifungua na maafa.

Pembe tatu hii lazima isimame muda wote na hivyo ni lazima michango iendelee, uwekezaji uwe na ufanisi na mafao yawe bora kwa wanachama. Hivi sasa kwa mfano kuna malalamiko mengi sana kwamba uwekezaji wa mifuko hauna tija kwa wanachama. Nikiwa mbunge niliyekagua mahesabu ya mifuko hii kwa miaka mine nakubaliana kabisa na malalamiko hayo ya wananchi.

Pia pensheni ya kima cha chini bado ni ndogo sana kwa mifuko mingi, mfano NSSF wanalipa tshs 80,000 wakati mifuko mingine inalipa shs 50,000 na hata shs 20,000 kwa mwezi. Ni vema mdhibiti wa mifuko aweke mazingira kwa mifuko katika michango na pia mafao. Angalau pensheni iwe kima cha chini cha mshahara kwa watu wanaopata pensheni ya chini kabisa.
Fao la kujitoa au kujitoa kwenye mafao?

Wafanyakazi wa maeneo mbalimbali nchini, na hasa migodini, walipiga kelele wakipinga uamuzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuzuia fao la kujitoa. Wananchi wengi sana tulikubaliana na hasira zao hasa ukizingatia mazingira yao ya kazi.

Wafanyakazi wa migodini nchini wanafanya kazi kwenye mazingira magumu. Wengi hawana usalama wa kazi zao. Wanafukuzwa hovyo kazi. Tumeambiwa kuna watu wamefukuzwa kazi kwa kosa la kuzungumza Kiswahili tu. Inasikitisha kwamba wakati mwingine wanafukuzwa kazi kwa kupitia ‘radio call' tu. Hivyo wanasema, unapozuia kuchukua fedha zao walizochanga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na zile walizochangiwa na waajiri wao unawaonea.

Pia wafanyakazi wa migodini wanapata magonjwa na ulemavu wa kila namna na hata wakati mwingine kushindwa kufanya kazi. Vijana wa Kitanzania walionyesha mbele ya Kamati ya Bunge ya Kazi na Ajira, magonjwa wanayoumwa na yasiyotibika kutokana na vumbi huko migodini. Tunaambiwa hata taasisi yetu ya OSHA ikienda migodini kukagua mazingira ya kazi wanaishia kwenye ofisi za wenye migodi na hawaendi maeneo ambayo Watanzania hawa wanafanyia kazi. Kutokana na hali hii, wanasema, hawawezi kusubiri kutimiza únits' za pensheni ili waweze kupata fedha zao. Hawana uhakika wa kuishi muda mrefu. Hivyo ni bora wachukue fedha zao wapange maisha yao.

Mfumo wa Hifadhi ya Jamii kokote duniani unapaswa kujibu hoja hizi za Wafanyakazi wa Tanzania. Wakati mfanyakazi anapokuwa anachangia kwenye mifuko (kwa wale wa NSSF, PPF na LAPF huchangia asilimia 10 ya mshahara na mwajiri huchangia pia asilimia 10. Kwa wafanyakazi wa umma mwajiri huchangia asilimia 15 na waajiriwa asilimia 5) kuna mafao mwanachama hupata.

Mfano ni mafao ya afya kwa shirika kama NSSF na elimu kwa shirika kama PPF. Mafao mengine ni kama ujauzito, ulemavu na maafa. Mfumo wetu wa Hifadhi ya Jamii hauna fao la usalama wa kazi ambalo hutolewa kama unemployment benefit kipindi ambacho mwanachama anapokuwa amekosa ajira sehemu moja na anatafuta ajira sehemu nyingine. Hata hivyo, mwanachama anapochukua mafao yake yote maana yake ni anajitoa kwenye mafao yote mengine.

Fao la ulemavu linajibu kabisa changamoto ya kuumia kazini ambayo wafanyakazi wa migodi wanayo. Hivyo iwapo mwanachama atajitoa kwenye mafao au akiwa katika mfumo wa ‘provident fund' maana yake ni hataweza kulipwa fao hili la ulemavu. Masuala ya magonjwa yasiyotibika nayo yaweza kuwa sehemu ya fao la afya kwa wafanyakazi.
Kila changamoto ina majibu ndani ya mfumo wa hifadhi ya jamii isipokuwa pale ambapo mwanachama anapofukuzwa kazi au kuacha kazi.

Ni muhimu kutengeneza mfumo wetu wa hifadhi ya jamii ambao unaendana na mazingira yetu. Kwa mfano tunapaswa kuwa na fao la kutokuwa na ajira, fao la elimu kwa wanachama na fao la afya kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii hapa nchini. Fao la kutokuwa na ajira ni la lazima katika mazingira ya sasa ambapo vijana wengi wanafanya kazi za mikataba au usalama wa kazi unakuwa ni mdogo.

Kujitoa kwenye mafao yaweza kuwa suluhisho tamu kwa sasa na hasa kwa vijana lakini ni suluhisho litakaloleta matatizo makubwa sana kwa nchi siku za baadaye kwani tutashindwa kuhudumia idadi kubwa ya wazee nchini. Wakati tunataka kuwapo pensheni kwa wazee wote nchini, iwapo tukiruhusu watu kujitoa kwenye mafao nchi haitaweza kuhudumia wazee wote nchini. Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, baada ya miaka 50 Tanzania itakuwa na wazee wengi sana wanaohitaji huduma ya hifadhi ya jamii. Hivyo maamuzi yetu ya sasa hayawezi kudharau huko tuendako.

Watu wengi wanazungumzia wastani wa maisha ya Mtanzania. Takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa maisha ya Mtanzania ni miaka 58. Kutokana na hali ilivyo hapa nchini wastani wa maisha utaongezeka zaidi na hivyo idadi ya wastaafu nchini kuwa kubwa sana.

Kiongozi yeyote anayeangalia mbele hawezi kukubali wananchi wake kujitoa kwenye mafao. Bali ataweka mazingira mazuri kwa wananchi wake kufaidika na mfumo wa hifadhi ya jamii. Kiongozi lazima awe na uwezo wa kuwaambia wananchi wake ukweli hata kama ni ukweli mchungu na kuwapa majawabu ya namna ya kukabiliana na changamoto badala ya kukimbilia kutoa uamuzi wa haraka haraka kufurahisha watu.

Hata hivyo, wakati tunasema pasiwepo na kujitoa kwenye mafao, lazima kujiuliza ni kwa nini vijana wanataka kujitoa kwenye mafao? Jibu ni dhahiri kwamba serikali haiaminiki. Mifuko haiaminiki. Kumekuwa na malalamiko makubwa ya wananchi kuhusu uwekezaji wa mifuko na kiwango cha pensheni ambacho wananchi wanalipwa. Ninaangalia hesabu za mifuko yote hapa nchini kila mwaka. Serikali inadaiwa mno na mifuko hii.

Mradi wa Chuo Kikuu cha Dodoma pekee, serikali inadaiwa zaidi ya shilingi trilioni 1.2 na mifuko yote nchini. PSPF wanaidai serikali zaidi ya shilingi trilioni tatu kutokana na kulipa mafao kwa watumishi waliostaafu lakini hawakuchangia katika pensheni. Serikali hailipi madeni yake katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Hivi karibuni iliyokuwa kamati ya POAC ilitoa agizo la jumla kwa mifuko yote ya pensheni nchini kwamba ni marufuku kuipa serikali mikopo bila mikataba kama ilivyo sasa.

Serikali ilipe madeni yake na mifuko iwekeze kwenye maeneo yenye kukuza uchumi, kuzalisha ajira na kuongeza thamani ya pensheni. Asilimia 70 ya mali za mifuko ambazo sasa ni shilingi trilioni 4.7 ni dhamana za serikali, asilimia 22 kwenye majengo na asilimia nane hisa kwenye kampuni mbalimbali. Mifuko iwekeze kwenye miradi ya kukuza uchumi kama kilimo, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme. Bila kujenga imani ya wanachama kuhusu michango yao, watataka kujitoa tu potelea mbali madhara yake ya kukosa pensheni uzeeni au mafao mengine kabla ya hapo.



Mifuko inapaswa kuboresha huduma zake kwa wanachama. Haina maana kuwa na fao la bima ya afya wakati wanachama wanapotaka kupata huduma hiyo inakuwa shida sana. Katika mahesabu ya NSSF ya mwaka unaoishia Juni 2011, Kamati ya mashirika ya umma ilikuta shirika limeshindwa kutumia zaidi ya asilimia 50 ya bajeti yake ya fao la matibabu. Kuna sababu mbili tu za kuelezea hali hii, moja wanachama hawajui huduma hii au mfuko unaweka utaratibu mbaya unaosababisha wanachama kuona ugumu wa kupata fao hili. Mifuko ni lazima iboreshe huduma kwa wanachama ambao kimsingi ndio wenye mfuko.

Pia Tanzania ina mifuko mingi sana yenye mafao tofauti tofauti. Imefika wakati wa kuunganisha mifuko hii na kubakiza mifuko mwili tu – mmoja kwa sekta ya umma na mmoja kwa sekta binafsi. Mafao yote yaliyopo kwa mujibu wa sheria yafanane kwa mifuko yote ili kuondoa tofauti kwa wanachama wa mifuko.

Wanachama wanataka kujitoa kwenye mafao kwa sababu imani kwenye mfumo mzima wa hifadhi ya jamii ni ndogo. Ni wajibu wa mifuko kujiangalia na kupata suluhisho kwa kuongeza imani ya wanachama wake kupitia huduma kwa wanachama na uwekezaji bora utakaohakikisha thamani ya michango, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira nchini. Kujitoa kwenye mafao ni kuangamiza nchi, lakini pia huduma mbovu za mifuko ni kichocheo cha wimbi hili la kujitoa.

Suluhisho la changamoto zilizopo kwenye mfumo wa hifadhi ya jamii nchini ni kuboresha mafao ikiwemo kuongeza fao la kukosa ajira (unemployment benefit) kwa wanachama wanapokuwa wanatafuta kazi nyingine, kuboresha fao la elimu ikiwemo kuruhusu wanachama kutumia michango yao kujiongezea elimu, fao la mikopo ya SACCOS za wanachama na fao la kutumia michango kama dhamana ya kupata mikopo ikiwemo mikopo ya kujenga nyumba nk.

Mifuko pia iongeze juhudi za kuandikisha wanachama ili kuongeza idadi ya watanzania wenye kufikiwa na mfumo a hifadhi ya jamii. Mfano wa wakulima wa kahawa kule Kigoma Kaskazini ambao sasa wanajiunga na NSSF kwa ajili kujiwekea akiba ya uzeeni na kupata mafao kama ya uzazi na bima ya afya ni mfano unaopaswa kuigwa nchini kote na hasa yale maeneo yenye mazao ya biashara.

Hifadhi ya jamii ni haki na wajibu wa kikatiba. Kuruhusu kujitoa kwenye mafao ni kufurashisha kizazi cha sasa kwa mzigo utakaobebwa na kizazi kijacho. Changamoto za wanachama wanaotaka kujitoa kwenye mafao zijibiwe ndani ya mfumo wa hifadhi ya jamii ulioboreshwa na wenye uwekezaji wenye tija na huduma bora kwa wanachama.



[1] Key note paper at Third NSSF stakeholders' Forum in Arusha, February, 2013.
 
Ukizunguka dunia nzima hakuna fao la kujitoa kwa mwananchi wa kawaida lakini kuna FAO LA KUJITOA LA WANASIASA KILA BAADA YA MIAKA MITANO
 
Haya kile kilio chetu wafanyakazi kumbe yupo yule anayezidi kukipigilia misumali Sina mengi nyie wenyewe mtaamua kama huyu kijana ni mtu mzuri mmeshindwa kurudisha pesa zilizo kwenye mabenki ya nje bado mnataka hela zetu The Citizen Friday 15-02-2013 View attachment 83220
ndio maaana yake ... anavaa gwanda cku hizi sio suti tena
 
Haya kile kilio chetu wafanyakazi kumbe yupo yule anayezidi kukipigilia misumali

Sina mengi nyie wenyewe mtaamua kama huyu kijana ni mtu mzuri

mmeshindwa kurudisha pesa zilizo kwenye mabenki ya nje bado mnataka hela zetu

The Citizen Friday 15-02-2013

View attachment 83220
Ndio wana siasa wetu wa leo hao! Hakuna wanachikiamini na hivyo kukosa uelekeo usio yumba yumba!
 
Salam wanajamvi

Nimesoma gaazeti la citezen zito zuberi kabwe anapinga wanachama kuchukua pesa zao kwenye mifuko ya hifazi ya jamii, sababu kubwa kwake ni kufilisika kwa hii mifuko pindi wanachama watakapochukua pesa zao.
Zito anashindwa kuelewa kuwa hizo pesa ni za wanachama na wana haki ya kuchukua akiba yao wanapo staafu au kuacha kazi kwa sababu yoyote ile.
Mifuko ya hifadhi kufilisika si kwa sababu ya wanachama kuchukua pesa zao ni uwekezaji mkubwa waonfanya.
Kitu cha kushangaza zito alikuwepo bungeni wakati hoja ya mbunge wa kisarawe inawasilishwa lakini cha ajabu hakuyasema haya, leo anaibukia Arusha na kuanza kurudia yaleyale.
Zito sio lazima wote wanao acha kazi watarudi kuajiriwa tena, wengine wanamipano ya kuachana na ajira na kujiajiri kwa kidogo walichovuna wakiwa kazini.
Ukumbuke huu ujira tunaoupta tukiwa kazini hautoshelezi kuweka akiba ya baadae, karibu walisilmi 90 ya wafanyakazi wanategemea akiba ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya kuendesha maisha baada ya kazi.
Ni bora ungewashauri hao wenye dhamana ya hiyo mifuko wakatafuta njia nyingene ya kuboresha hiyo mifuko na sio kuzuia fao la kujito.
 
Wanasiasa wawaache wafanyakazi na fao lao la kujitoa mbona zao wanazichukua kila baada ya miaka mitano? Mkuu Zitto, kazi zetu sisi si sawa na huo ubunge wenu!! Waoneeni huruma wafanyakazi jamani.
 
Yawezekana kabisa kwamba fao la kujitoa ni tatizo mojawapo katika maendeleo ya mifuko ya penseni lakini sii tatizo kuu. Tatizo la msingi kwenye hii mifuko ni kitendo cha wastaafu wa serikalini( haswa ngazi za makatibu wakuu, madirector, makamishna) kulipwa mafao ambayo ni makubwa sana ukilinganisha na michango yao halisi kwa mifuko hii. Sisi wa kima cha chini na kati tunapoamua kujitoa kwenye mifuko hii, malipo yetu ni sawa kaisa na ichango tuliyokuwa tukikatwa. Kwa mweenye takwimu, atuambie mafao ya katibu wa wizara au kamishna wa idara fulani anapostaafu. Kama kweli tunataka mifuko ya pension isife, inabidi mafao ya watendaji wa kuu wa serikali yaangaliwe upya sambamba na kutafuta suluhu kwenye hii habari ya fao la kujitoa.
 
Nchi zote zilizoendelea duniani zina mfumo wa Social Security Funds
Tena clients hawana ruhusa ya kujitoa kwenye mafao hadi wa-qualify!
Hivi hua unajiskiaje ukikuta mtu aliekua anajiweza kawa ombaomba?
Ni jukumu la serikali kuhakikisha kua wananchi wanasave for their old days.

Leo population ya Ulkaya imezeeka. In France the average age is >40
Serikali ingeshindwa kuwa-convince wananchi kuchangia leo ingekuaje?
 
He cited the government financing of construction of universities, saying the flow of recovered funds for the loans extended was slow.
Mr Kabwe challenged the social security institutions to direct their investments to projects which would create employment. This will not only spur economic growth but also increase membership.


Kigoma North MP (Chadema) Zitto Kabwe

Mimi naona hoja ya maana sana iko hapa, hiyo ya fao la kujitoa timeishaongea sana humu JF na kwenye media zote. Kuna mitazamo tofauti sana kuhusu fao la kujitoa, na kila mtu ana wazo lake.
 
Huyu zitto ni kichaa fulani hivi na huyu ndiye huwa anataka kuwa rais wetu na kujilaumu eti umri ndiyo kikwazo wa yeye kuwa rais.Huyu hata umri tukiurdisha miaka 30 si wakuwa rais.Kina Nyerere alikuwa rais kijana kwa sababu alikuwa na akili nyingi lakini siyo huyu juha.Na CHADEMA huyu jamaa anawaharbia sana
 

Attachments

  • 20130215_Newspapers clippings_Friday 7.pdf
    679.2 KB · Views: 113
mmeshindwa kurudisha pesa zilizo kwenye mabenki ya nje bado mnataka hela zetu

"If we allow withdrawals there would be no social security in the country", warned the Kigoma North MP (Chadema) Zitto Kabwe in his presentation at the stakeholders conference of the National Social Security Fund (NSSF).
He wondered what the fate of thousands of social security members would be after retirement if they were to be encouraged to withdraw their benefits while still working and how the pension funds would operate profitably.
The outspoken opposition legislator cautioned that the social security schemes in Tanzania were still fragile and that proposals to allow total withdrawals should be discouraged for the time being. "We are at a crossroads," he cautioned, noting that although some people favoured voluntary withdrawals, there were dangers both to the pensioners and the country's economy.
Kigoma North MP (Chadema) Zitto Kabwe
Sioni kibaya katika hii kauli ya Zitto! Binafsi nafikiri ana mtazamo chanya dhidi ya hizi security funds. Lakini zaidi ya yote, kama zile fedha zinaitwa mafao ya uzeeni, kwanini mtu atake kuyachukua leo au kesho kabla hajastaafu? Binafsi naungana na Zitto katika hoja hii!
 
Nchi zote zilizoendelea duniani zina mfumo wa Social Security Funds
Tena clients hawana ruhusa ya kujitoa kwenye mafao hadi wa-qualify!
Hivi hua unajiskiaje ukikuta mtu aliekua anajiweza kawa ombaomba?
Ni jukumu la serikali kuhakikisha kua wananchi wanasave for their old days.

Leo population ya Ulkaya imezeeka. In France the average age is >40
Serikali ingeshindwa kuwa-convince wananchi kuchangia leo ingekuaje?

Umeisha sema nchi zilizondelea kwani Tanzania ni moja ya hizo nchi fanya upembuzi kwanza unapojibu hoja.
Hizo nchi unazozisema wafanyakazi wanabefeiti kibao na hiyo mifuko na hata ajira zao pia.
Sio sie hapa ajira mkononi hujui kesho itakuaje.
 
Huyu zitto ni kichaa fulani hivi na huyu ndiye huwa anataka kuwa rais wetu na kujilaumu eti umri ndiyo kikwazo wa yeye kuwa rais.Huyu hata umri tukiurdisha miaka 30 si wakuwa rais.Kina Nyerere alikuwa rais kijana kwa sababu alikuwa na akili nyingi lakini siyo huyu juha.Na CHADEMA huyu jamaa anawaharbia sana
Mwishowao, naona unatumia maneno makali sana dhidi ya Zitto bila ya kujenga hoja! Hebu sema ujuha wa Zitto kwenye jambo hili upo wapi? Na kama wewe unapingana na Zitto, je mtizamo wako ni upi? Upewe hiyo pesa yako wakati bado upo kazini, na ukiwa bado una nguvu zote na mshahara unaendelea kupata? Halafu utakapostaafu au kuzeeka utajitunza vipi na hali nguvu utakuwa umeishiwa? By the way, kama ikitokea leo watu wote wakajitoa kwenye hii mifuko, unafikiri itabaki na nini? Binafsi sioni tatizo katika hoja yake. Labda mnaoipinga leteni utetezi wenu.
 
Last edited by a moderator:
Nimeamini wanasiasa hawaongei kwa mioyo yao, nimegundua wanatumia ubongo wa nyuma,
 
Nchi zote zilizoendelea duniani zina mfumo wa Social Security Funds
Tena clients hawana ruhusa ya kujitoa kwenye mafao hadi wa-qualify!
Hivi hua unajiskiaje ukikuta mtu aliekua anajiweza kawa ombaomba?
Ni jukumu la serikali kuhakikisha kua wananchi wanasave for their old days.

Leo population ya Ulkaya imezeeka. In France the average age is >40
Serikali ingeshindwa kuwa-convince wananchi kuchangia leo ingekuaje?
Utakuwa unaumwa ule ugonjwa wa kuigaiga kila kitu, huna tofauti na kilaza wa kule the commedy orijino, Kukopi na kupesti..!
 
Umeisha sema nchi zilizondelea kwani Tanzania ni moja ya hizo nchi fanya upembuzi kwanza unapojibu hoja.
Hizo nchi unazozisema wafanyakazi wanabefeiti kibao na hiyo mifuko na hata ajira zao pia.
Sio sie hapa ajira mkononi hujui kesho itakuaje.

Kwa namna umejieleza ni kama kwa sababu Tanzania haijaendelea
haina maana kujipanga kama nchi zilizo endelea/ Is that what you say?
Hizo benefit unasema watu hawapati umechunguzia wapi?mbona wanapata?
Kama tatizo ni ajira, basi tutoe maoni on how to improve on that first
Sio kuona tatizo moja and reject the whole idea (throwing the baby with his bath water)
 
Utakuwa unaumwa ule ugonjwa wa kuigaiga kila kitu, huna tofauti na kilaza wa kule the commedy orijino, Kukopi na kupesti..!

Utakua unaumwa na ugonjwa wa stagnation wewe
Huna tofauti na funza wa chooni ambae hataishi kua kipepeo one day!
 
Back
Top Bottom