Fao la kujitoa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kurudishwa

Ningeshangaa kwa nondo za JJ.Mnyika na Sugusia kwenye kipima joto ijumaa iliyopita kama
wangehimili ningewaona wao ni zaidi ya wanaume.
 
Hili sio suala la kilio bali presha toka ngazi mbalimbali katika jamii yetu. Wao lao ni kupima upepo. Kama una nguvu (kama ilivyo hoja hii ya sasa) basi huwa wanakubali kwa kisingizio cha kuridhia matakwa ya wananchi

huna tofauti na wale wanaochukia umeme ukikatwa na kushangilia unaporudishwa!

i know hiki ni kidonge kichungu kumeza vumilieni tu ... lakini Dr. JK anastahili pongezi kwa kusikia kilio ... Dr JK anafanya mengi sana mazuri kwa ajili ya hii nchi..waliomtangulia wote walishindwa kuanzia awamu ya kwanza... mwenye macho hana haja kuambiwa tazama
 
Hii ni kwa mujibu wa ndugu Magori (DO – DIRECTOR OF OPERATIONS) katika kipindi cha kipimajoto wakati anamalizia kuzungumza. Amesema kuwa fao la kujitoa, serikali haina tatizo. Inaweza kutoa wakati wowote na kwamba amewapanga mameneja wake tayari kwa kazi hiyo.

Ila ametoa angalizo: Kama huna mpango sahihi na hela hizo bora uziache. Ukiacha kazi, usichukue fedha zako bali tafuta nyingine na uendeleze kuweka akiba ili uje kufaidi pensheni.

Kiujumla kajitahidi kujitetea, ila lililokuwa likisubiriwa ni hiyo kauli yake ya mwisho.

----------
UPDATE - October 30, 2012

530781_498119836878641_1408481086_n.jpg
nahisi kama hiyo doc imekuwa forged. mbona signatory ni mmoja tu? alafu hakuna muhuri wowote
 
believe me not, hakuna kitu kimeniuma kama hiyo pesa ya NSSF, nilikuwa sielewi nitaisubirije eti mpaka nifikishe 60yrs! who ever spoke of that is mad nakwambia!

Nimesikia Makinda akikonfirm kuhusu fao la kujitoa ...ila mmh
 
nahisi kama hiyo doc imekuwa forged. mbona signatory ni mmoja tu? alafu hakuna muhuri wowote

Acha kukurupuka, barua yenye header haihitaji muhuri, hio ni kutokana na KANUNI ZA KUDDUMU ZA UTUMISHI WA UMMA, toleo la tatu, 2009. Vile vile haihitaji sahihi zaidi ya moja hiyo siyo Vitabu vya kufunga mahesabu.
 
wamefuta matamko ya ssra ya kuzuia fao la kujitoa, hawajafuta kifungu cha wizi kwenye sheria yenyewe, ina maana sheria iko pale pale!

Tunataka kifungu kifutwe pia ndiyo mtuletee elimu ya kutuibia-mtakuwa na kazi ya kutu-convince kutuibia! Tumesikia eti kikosi kazi kilizunguka kukusanya maoni-labda walikusanyia kwenye sturi ndefu lakini makazini hatujawaona!

Wafanyakazi tuwe macho na mafisadi yaliyofilisi mfuko wa nssf.

wamefuta matamko ya ssra ya kuzuia fao la kujitoa, hawajafuta kifungu cha wizi kwenye sheria yenyewe, ina maana sheria iko pale pale!

Kama haujui jinsi bunge linavyoendeshwa si vibaya ukauliza,rais katoa tamko fao lirudishwe,ssra wametengua zuio lao,waziri ametoa kauli bungeni ya kuruhusu fao la kujitoa sasa wewe unataka wafute nini? Tuwapongeze tu kwa kusikiliza vilio vya wananchi.....
 
Na hongera zaidi kwa mbunge wa kibaha kwa kuchukua hatua za haraka na kuwasilisha hoja binafsi bungeni,hoja ambayo imesaidia kufutwa kwa kifungu cha kukataza kuchukua mafao ukiacha kazi ....
Bado tuna imani na serikali hii sikivu ya ccm...
 
Haya wananzengo fao la kujitoa limerudishwa, tunaofanya kwa wahindi ukifukuzwa tu fasta nssf/ppf unachukua mkwanja wako
 
Yaani kusema ukweli sina jinsi ya kushukuru sijui ni CHADEMA imefanya, sijui ni CCM imefanya kwangu mimi ni shukrani tele
 
upo kijiji gani nije nikupongeze kwa uwezo wa elimu yako ....yaani umnyime mtu dawa akikaribia kufa ndio umpeleke hospital alafu umshukuru dakitari.....huna tofauti na wanaomshukuru makufuli kwa kujenga barabara utafikiri ni pesa zake kumbe kodi yako looooooooooh
 
Na hongera zaidi kwa mbunge wa kibaha kwa kuchukua hatua za haraka na kuwasilisha hoja binafsi bungeni,hoja ambayo imesaidia kufutwa kwa kifungu cha kukataza kuchukua mafao ukiacha kazi ....
Bado tuna imani na serikali hii sikivu ya ccm...

Imani na CCM unayo mwenyewe mkuu..... binafsi nawapongeza watanzania wote waliojitoa kwa hali na mali kuhakikisha serikali hii korofi inatengua uamuzi wake ilioutoa kwa kukurupuka,shukrani za pekee ziwaendee WAFANYAKAZI WA MIGODINI NA WANAHARAKATI kwa kulifanikisha hili bila mashinikizo mandamano na matamko selikari ya CCM haisikii
 
Na hongera zaidi kwa mbunge wa kibaha kwa kuchukua hatua za haraka na kuwasilisha hoja binafsi bungeni,hoja ambayo imesaidia kufutwa kwa kifungu cha kukataza kuchukua mafao ukiacha kazi ....
Bado tuna imani na serikali hii sikivu ya ccm...

Tushakuchoka na thread zako zisizo na maana, sasa ni nani aliyetishia kuliondoa??

Mtu anapotishia kutofanya wajibu, then ajirudi na kufanya(kwa kugundua amepotoka) unampongeza kana kwamba hakupaswa kufanya??!..

Akili na watu waliochoka kufikiri kama wewe bado wanaturudisha nyuma, wakidhani watu wakifanya wajibu tunapaswa kuwazawadia!!

This shows, highest degree of irresponsibility, attention in dealing with important matters!
 
Kama haujui jinsi bunge linavyoendeshwa si vibaya ukauliza,rais katoa tamko fao lirudishwe,ssra wametengua zuio lao,waziri ametoa kauli bungeni ya kuruhusu fao la kujitoa sasa wewe unataka wafute nini? Tuwapongeze tu kwa kusikiliza vilio vya wananchi.....

Kutoa tamko ndiyo kufuta/kutunga sheria? Au elimu ya kata ina eleza kuwa matamko ni Sheria! Wao i-process na kui-implement sheria kihuni na wameyaondoa matamko yao kwa njia hiyo hiyo.

Kwa ulivyopungukiwa na hekima, hapa wa kupongezwa Rais, Bunge, Mnyika, Jafo au wafanyakazi wenyewe waliokomaa mpaka wakapata haki yao.

Kama mwizi akikuibia kisha akakimbia na kitu chako, ukaanza kupiga kelele, akikiachia alichoiba ili asije "uawa na wananchi wenye hasira kali?" uta anza kumpongea au utasema bahati yake mwanaharamu huyo!
 
Na hongera zaidi kwa mbunge wa kibaha kwa kuchukua hatua za haraka na kuwasilisha hoja binafsi bungeni,hoja ambayo imesaidia kufutwa kwa kifungu cha kukataza kuchukua mafao ukiacha kazi ....
Bado tuna imani na serikali hii sikivu ya ccm...

hatuna imani nao kabisa! Walitaka kutuibia sema kosa walilofanyama walipima kina cha bahari ufukweni. Walipofika kati maji yamewazidi nguvu wamezama.
 
Mi ninachoona hapa, ni kwamba serikali ilichukua kiasi kikubwa mno cha fedha NSSF, ndo maana hawataki NSSF kuruhusu wanachama kuchukua mafao yao, hivi wanadhani bado tumelala? Lakini, hizi kelele, zitaonekana 2015, sasa hivi acha watupeleke wanavyo taka, lakini bad o aka 2 tu, kitasomeka tu!
 
Wamesema wamerudisha, nilisikia wakati wa kipindi cha Bunge leo asubuhi na usiku wa habari ITV wamerudia... Kesho mapema naanza nao kwani kunasenti zangu jamaa wamezizuia eti mpaka nifikishe miaka 55.. Nasema kesho ntakula sahani moja mpaka kieleweke mbona wafanyakazi wa NSSF wanazichukua za kwao kwa njia haramu kama za mikopo kwa riba nafuu?
 
Back
Top Bottom