Fao la kujitoa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kurudishwa

Hii maana yake nini wakuu ''Sasa ni rasmi fao la kujitoa larejea kwenye mifuko ya jamii''

Nombeni munipe maana halisi. KUjitoa kwenye mfuko wa jamii?!!

Naomba nijue kwanza, wewe ni mwanachama wa mfuko wowote wa kijamii? if yes, mfuko gani? nianzie hapo kukuelewesha
 
Ukiona hivyo ujue dili hilo limeharibika, lakini tusilegeze kamba tuwashinikize hawa jamaa warekebishe sheria yote sio tu kutoa tangazo. Hawa magamba hawaaminiki kuendelea kuwaachia wakae ni hii sheria yao waliojitungia ili waibe ni sawa na wanachama kutembea na kamba ya kujinyongea shingoni mwetu, ikumbukwe kuwa hawa jamaa hawana hela ila wanajibaraguza tu na uchaguzi wa 2015 unakaribia wanaweza kuibuka ghafla tena na kijarida chao hiki cha sheria ya kifisadi na kuanzisha zogo upya ili wapate pesa za bure bure za kununulia kanga za kuwagawia akina mama wawape kula hiyo 2015.
 
Lakini mbona tangazo hili limekaa kihuni, hivi kweli taasisi kubwa kama ya SSRA haina hata mhuri wa kuchonga, tangazo muhimu kama hili linatolewa kama vile limetoka kwa balozi wa nyumba kumi kumi lakini nafikiri na hawa mabalozi huwa na mihuri yao.

530781_498119836878641_1408481086_n.jpg

Miezi miwili, serikali yafuta tangazo lake. Sasa ni rasmi fao la kujitoa larejea kwenye mifuko ya jamii
 
Tangazo limewekwa kwenye 'headed paper' ya SSRA, inapunguza umuhimu wa muhuri.

Imekua faraja kurudisha uwezekano wa mwanachama kujitoa katika mifuko hifadhi ya jamii.

Lakini mbona tangazo hili limekaa kihuni, hivi kweli taasisi kubwa kama ya SSRA haina hata mhuri wa kuchonga, tangazo muhimu kama hili linatolewa kama vile limetoka kwa balozi wa nyumba kumi kumi lakini nafikiri na hawa mabalozi huwa na mihuri yao.
 
Asante nimekuelewa lakini dah!! office formalities kama zipo timiza tu zote usifanye kama shingo upande kwa kuwa umelazimishwa.

Tangazo limewekwa kwenye 'headed paper' ya SSRA, inapunguza umuhimu wa muhuri.

Imekua faraja kurudisha uwezekano wa mwanachama kujitoa katika mifuko hifadhi ya jamii.
 
sheria za tanzania sijui wanaozitunga huwa hawafikirii au kwa vile wengi wako bungeni bora liende au wanasinzia sana
 
Kama ni kweli huyo bibi mkomao irene isaka kaumbuka na mbwembwe zake.

Lakini bado hawaweka tangazo hilo kwenye tovuti yao, kwahiyo inawezekana mleta uzi ni mfanyakazi wa ssra,anapata chamotomoto toka jikoni.

Tusubiri
 
Mimi hadi nione wamewaandikia barua mameneja wa mifuko husika, kuna mgodi mmoja huyu mama alikwenda kutoa kitu kinacho itwa elimu ya kufutwa fao hilo, interijensia yake ilimuonesha kua hata toka salama, ilibidi aombe vyumba viwili kwenye gest house tofauti huko na wala hakutia timu ndani ya huo mgodi badala yake alimtuma men mmoja aende on her behalf, mwishoe alitoa tangazo linalofanana na hili, hadi leo still watu hawajalipwa, so mi staki kuamini hadi nione watu wameanza kuchukua, magamba kwa vitina ndio wenyewe!
 
Again Dr jk amethubitisha yeye ni kiongoizi bora kwa kusikia kilio cha watanzania
 
Hela ya uchaguzi itatoka kwenye dawa za waathirika wa ukimwi....kile kiwanda ni mrija mwingine mzuri sana sana...wenyewe wanakufuru wanasema hata iweje watakuja kufa tu,acha tuwaongezee muda kidogo!!sasa ule ndio mradi wao kwa sasa!!Mifuko ya jamii ilikuwa deal zuri sana kwao ila kwa sasa wamekomba mboga zoote,wangeweza kuzuia kwa miaka 2 iliyobakia kabla uchaguzi,mifuko ingekuwa safi tena kabla hapo mwanzo!
 
Again Dr jk amethubitisha yeye ni kiongoizi bora kwa kusikia kilio cha watanzania

Hili sio suala la kilio bali presha toka ngazi mbalimbali katika jamii yetu. Wao lao ni kupima upepo. Kama una nguvu (kama ilivyo hoja hii ya sasa) basi huwa wanakubali kwa kisingizio cha kuridhia matakwa ya wananchi
 
Sijawahi ona chama cha kipumbavu kama ccm! Walete pesa zetu haraka, hatutaki ngonjera!
 
Hili sio suala la kilio bali presha toka ngazi mbalimbali katika jamii yetu. Wao lao ni kupima upepo. Kama una nguvu (kama ilivyo hoja hii ya sasa) basi huwa wanakubali kwa kisingizio cha kuridhia matakwa ya wananchi

Nakubali ni sauti ya watanzania na kuwa na solidarity kuhusu ishu hii.
 
lakini mbona tangazo hili limekaa kihuni, hivi kweli taasisi kubwa kama ya ssra haina hata mhuri wa kuchonga, tangazo muhimu kama hili linatolewa kama vile limetoka kwa balozi wa nyumba kumi kumi lakini nafikiri na hawa mabalozi huwa na mihuri yao.....

Halafu halina tarehe.
 
Back
Top Bottom