Fao la kujitoa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kurudishwa

GEPF ni Provident Fund ambayo kitaalamu inaruhusiwa kutoa fao hilo. Hata hivyo ni sawa Pensheni Funds kutotoa withdrawal Benefit ila Mi nafikiri Hizo Pensheni funds zinatakiwa kuwahamishia hao wanachama katka Provident Funds like GEPF ili waweze kufikia malengo yao ya kupata fao la Kujitoa.
Since even Provident Fund are technically not allowed to pay Pension to its members
 
Mtoa mada anamasikio lakin hasikii ana macho lakin haoni, achakukulupuka bwana, huumtandao wawasomi, kamaulikwepa umande nenda facebook kwawatoto wenzako, usitupotezee mda! talk logic and fact!
 
Magori sio Bunge bhana....Huyu jamaa alikuwa anafundisha CBE miaka ya mwishoni mwa 90's, yuko vizuri sana kuelezea mambo na kama hujajipanga utashangaa umelowa tope...Kwenye kile kipima joto alijielezea vizuri sana na ni kazi yake sijamshangaa hata kama ningekuwa mie! Ila jambo la msingi na ambalo amekwepa kutueleza ni kwa vipi mabilioni ya pesa yalitoka kwa ajili ya mradi wa daraja la kigamboni kuwa na mkataba? Hata kama serikali ni garanta kama alivyosema yeye ameshindwa kuelezea uwazi uliopo kwa wawekezaji wanaotaka kukopa pesa pale kwa ajili ya miradi utaratibu ukoje?

Kucheleweshwa kwa malipo toka serikalini nimemshangaa kidogo kutetea hoja hiyo, mie naelewa bank wakikukopesha pesa na ukashindwa kulipa kwa wakati mwezi mmoja tu cha moto utakiona, sasa hawa jamaa wanatuelezea nini kama serikali imeshindwa kulipa kwa miaka miwili ama zaidi.

Magori anafahamu fika suala la value of money today, anajua anashauri vipi mtu kama hana kitu cha kufanyia hela asichukue hivi ni kweli kuna mtu ambae hana haja na matumizi ya hela? Mimi nasema umefika wakati watu waheshimu misingi ya utu wa mtu, pesa zile ni zangu sasa nashangaa sana mtu anapofika mahali atake kunikopesha fedha hizo alafu nimpe na riba kwa mlango wa saccos kweli tumefikia hapo?

Kulalamika kuwa hakuna mtu anayeweza kuwekeza katika miradi ya mabilioni ya fedha Magori katudanganya. Yapo makampuni makubwa na wazalendo wenye uwezo wa kukopa fedha hizo na wakafanya makubwa kama Mzee Mengi, Yule mweye Mount Meru Hotel, Mwenye Ngurudoto, Mwenye Caspian n.k NSSF haijawahi kuonyesha utashi wa aina yoyote wa kutoa mikopo kwa uwazi, hapa ndio maana tunahisi kwamba tunahujumiwa, watuelezee kinagaubaga ni fomula ipi wanayotumia kukokotoa mafao yetu kwa mkupuo?

Maelezo ya fao la bima ya afya kwamba yanaongeza thamani na kumtolea mfano mwanamke aliyenufaika na fao la uzazi ningependa kumweleza Magori asijidanganye kutufikirisha kuwa huo ni upendeleo maalum, actually fao hili ni tunda la uwekezaji wa fedha zake. Hapana shaka yoyote leo kuna mahospitali kadhaa hayajalipwa kwa wakati na kusababisha wanachama tukaingia mfukoni kutibiwa kwa fedha zetu. Aidha hajasema wazi kuwa kuna ukomo wa gharama katika matibabu flan flan hii sio sawa. Mafao ya mazishi, Matibabu , kuumia kazini n.k isichukuliwe kama tunaonewa huruma ama tumependelewa ni haki yetu.

Labda kwa taarifa nimeshachukua mafao yangu kama mara tatu hivi na faida haikufika hata laki moja kwa pesa zangu mlizokaa nazo miaka miwili. Mimi nadhani tumeshaibiwa vya kutosha tupeane chetu tuachane kizungu...!
 
Haitasaidia sana kushusha magorofa kwa sababu real estate investment walizonazo NSSF (including hayo magorofa unayoyaona wewe) ni 8% tu of their total investment...
 
Ni vigumu serikali kukubali fao la kujitoa NSSF kwani ndio wallet ye serikali ,hebu fikiria inadaiwa zaidi 336 Billion hizo zilitakiwa ziwe zimeshalipwa bado serikali haijalipa acha hizi mpya inazokopa tena.
 
Magori hana uwezo wa kutusemea sisi.Ashangaa tarehe nane siku ya mswaada tunaingia mjengoni kuitetea haki ye wenyewe . Na ole wao wathubutu kutunyima haki patachimbika.
 
Hakiya Mungu katika maisha nilikuwa nikiona watu wakiandamana nawaona hayawani sasa yamenifika, natamani hata leo tulianzishe maana nina hasira sana na hawa wapuuzi wabunge wote waliopitisha huu mswada, sina haja ya kuwalaumu NSSF ila nawalaumu viongozi wetu njaa waluiojaa unafiki na fitina.

Hivi wao wengi wao wanavougua viharusi na maradhi mengine hatarishi wana uhakika wa kufikisha miaka 55. Haya shime sasa wafanyakazi tujipange kujikomboa na ukombozi ni sasa maana tukiendelea kumchekea nyani tutavuna mabua for sure"

Jamani ifike mahali tusije tukabaki tunalaumu kama huyu ndugu Martin Niemöller (1892–1984) ambae mwishowe alibaki peke yake "First they came for the communists,and I didn't speak out because I wasn't a communist. Then they came for the socialists,and I didn't speak out because I wasn't a socialist. Then they came for the trade unionists,and I didn't speak out because I wasn't a trade unionist. Then they came for me,and there was no one left to speak for me.
 
Je wafanyakazi tumejipanga vipi, tumewasiliana vipi, ni lazima tuunganishe mawasiliano na grass roots ili kama tukiitisha maandamano iwe rahisi kutumiana message hata kwa simu ama twitter ama facebook
 
Naona baadhi ya wadau humu wanalalama sana. Kikao cha Bunge kinaanza kesho, na jambo mojawapo la msingi litakalojadiliwa ni hoja iliyopelekwa Bungeni na Mbunge wa Kisarawe, Ndugu jafo, kuwa fao la kujitoa lirudishwe. Kuna mawili hapa.
1. Hali ya sasa ni tete kisiasa na hata kiuchumi. kisiasa kwa maana kwamba chama tawala chenyewe knapitia hali ngumu na mbaya sana ya kuchukiwa na kukataliwa. Ili kupooza machungu ya wananchi (kiuchumi), serikali kupitia kikao cha Bunge kinachoanza wataridhia fao la kujitoa.

2. Mleta hoja Bungeni ni mwanaccm. Hii ni tiketi tosha kabisa kuwa hoja hii itapitishwa na fao kurudishwa. Tusubiri tuone
 
Hawa jamaa hawana mpango wa kutulipa hizo pesa zetu, wanacho fanya ni kutaka kutugawanya 'divide and rule' kati ya nssf na staffs wa mifuko mingine. Kitendo cha kuweka PPF ktk mswada kujadiliwa ktk bunge linaloendelea pasipo kugusia nssf ni kutaka kuwapa matumaini staffs wa PPF ili wajione wao pesa zao ziko salama.

Wazee wa magamba wanatechnics kibao za kuplay na minds za wabongo na mara nyingi hua wanafanikiwa. Tuwe makini kwa hizi mbinu zao chafu......! Wao wanadai wanatekeleza miongozo ya ILO ambayo inazuia wanachama kukomba mishiko yao kabla ya umri wa kustaafu, hao wa GEPF wanaochukua na hao wa PPF kama kweli wanataka kuwaruhusu wao hawatazeeka na kuhitaji pensheni? Waache upuuzi.....!
 
Lazima nichukue hela yangu naacha kuajiriwa mwezi ujao,nitaenda hadi ILO lazima kieleweka,mbona wabunge wanachukua chao mapema pale miaka 5 ikiisha?
 
Lifuatalo ni tangazo la mamlaka ya usimamizi na udhibiti wasekta ya hifaji ya jamii (ssra)...limetolewa leo (copy ninayo) na kusambazwakwa vyombo vya habari hapa bungeni dodoma...

Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi yajamii (ssra), inapenda kuufahhamisha uma kufutwa kwa tanzano lililotolewa mweziagosti 2012 kwenye vyombo mbali mbali vya habari lililohusu kusitishwa kwa faola kujitoa.

Maamuzi haya yanaenda sambamba na hatua ya serikalikuendelea na utekelezaji wa azimio la bunge tukufu la jamuhuri ya muungano watanzania katika kikao chake cha nane kilichoazimia pamoja na mambo menginekuirejea sheria ya hifadhi ya jamii (the social security laws amendments act no.5 of 2012).

My take:

sasa swali...je! Unadhani hatua hii ina unafuu wowote kwawafanyakazi! Je! Huku si kuuhadaa umma! Kwani kuondoa tangazo kunabatilishauhalali wa sheria! Tafakari na chukua hatua….
 
Back
Top Bottom