Fao la kujitoa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kurudishwa

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Hii ni kwa mujibu wa ndugu Magori (DO – DIRECTOR OF OPERATIONS) katika kipindi cha kipimajoto wakati anamalizia kuzungumza. Amesema kuwa fao la kujitoa, serikali haina tatizo. Inaweza kutoa wakati wowote na kwamba amewapanga mameneja wake tayari kwa kazi hiyo.

Ila ametoa angalizo: Kama huna mpango sahihi na hela hizo bora uziache. Ukiacha kazi, usichukue fedha zako bali tafuta nyingine na uendeleze kuweka akiba ili uje kufaidi pensheni.

Kiujumla kajitahidi kujitetea, ila lililokuwa likisubiriwa ni hiyo kauli yake ya mwisho.

----------
UPDATE - October 30, 2012

530781_498119836878641_1408481086_n.jpg
 
Huo muswada wenyewe wa mabadiliko mbona wameweka PPF tu NSSF hawapo?tusubiri kwanza wao si watunga sheria, wao ni watekelezaji wa sheria zilizotungwa na bunge hata waseme nini kama bunge halijapitisha hawawezi fanya kitu
 
Acha kukurupuka mkuu......jamaa hana mamlaka ya kutamka hivyo....kasema kama magamba wakirudisha walichotaka kutupora eti wapo tayari kuylipa.....tutajua mbivu na mbichi baada ya kikao cha bunge lijalo.....
 
Habari ndio hiyo kuwa serikali itaridhia fao la kujitoa. Hii haimaanishi kuwa kila mwanachama atajitoa. Na ukweli ni kuwa presha iliyopo kwa sasa, serikali haina mbadala katika hilo. Suala jingine ni kuwa GEPF inalo fao la kujitoa. Mkataba wako ukiisha unachukua hela zako. why not nssf?
 
NSSF hawana nia hiyo..huyo jamaa yako huyo uliyemsikia nadhani au hukumwelewa au amejichanganya!!!.....wanataka kucheza na maisha ya watu hawa.....
 
Uuuwiiiiiiii, Uwiiiiii weziiiiiii

MIGOMO NA MAANDAMANOO. TANZANIA LAZIMA SASA TUSEME BAASI. UVUMILIVU NA WOGA BASI.

HAKUNA WA KUZUIA MAANDAMANO WAFANYAKAZI NI WENGI SANA, POLISI NA JWTZ NI WATOTO WETU, WAJOMBA ZETU, DADA ZETU, KAKA ZETU. ILA HAO VIBARAKA WACHACHE TUTAWADHIBITI TUKIUNGANA TUNAWEZA.

TUTASHUSHA HAYO MAGHOROFA ya kifisadi, udom, machingwa complex, daraja la kigamboni. HAYO NI MIRADI YA KISIASA NA KIFISADI KUINUFAISHA SERIKALI YA CCM.

Sasa tuanze kuhamasishana na kutaarifiana, tujiandae sasa. Mtumie huu ujumbe mfanyakazi mwenzako.

"ndugu yangu mfanyakazi, akiba yako ya NSSF inachezewa na mafisadi, je wewe una uhakika gani na ajira yako? Mshahara wako unakutosha ama unanyonywa!!! Je ukiacha kazi ama ukiachishwa utaishiji ili ufike miaka 55? Una akiba ya kutosha kujikimu kusomesha ana kulisha familia? Una uhakika wa kuishi hadi miaka 55? Majibu unayo, jiandae na acha woga. tetea haki yako. uwe tayari kwa maandamano yatakatoitishwa na wanaharakati ama mpango mzima"
 
Hizi ni baadhi ta nukuu toka kwa Magori kwa mujibu wa Mh. Mnyika

'Ushauri wangu;wananchi wasichukue tu bora kuchukua pesa za fao la kujitoa.Zinaweza kuisha muda mfupi.Wajue wanafanyia nini-Magori'

Ushauri wangu;wananchi wasichukue tu bora kuchukua pesa za fao la kujitoa.Zinaweza kuisha muda mfupi.Wajue wanafanyia nini-Magori

"Maamuzi yote ya NSSF hufanywa na Bodi"-Magori

Na hizi nyingine ni nukuu za waliobakia

"Kuna watu wengi wameathirika kwa kukatishwa kwa fao la kujitoa.Naomba ajenda ije mezani.Kila mtanzania apate haki-Jafo (Mbunge)

"Serikali iheshimu fao la kujitoa.Irudishe fao la kujitoa.Mwananchi anafaidika kwa fao la kujitoa"-Sungusia (mwanaharakati)

"Tutazame serikali kwa jambo pana.Iruhusu fao la kujitoa.Kisha tuangalie namna ya kuboresha mifuko yetu"-Mnyika
 
Hatuhitaji mpira wa danadana wala chenga, tunahitaji magoli, SSRA WATOE TAMKO WATU WAKACHUKUE PESA ZAO FASTA. HII NDIO KAULI YETU.
 
Kauli za kupitia kipima joto si rasmi, kwa hiyo tusiliwaze. Tuendeleze mapambano dhidi ya sheria kandamizi, kila mmoja kwa nafasi yake.
 
Kauli za kupitia kipima joto si rasmi, kwa hiyo tusiliwaze. Tuendeleze mapambano dhidi ya sheria kandamizi, kila mmoja kwa nafasi yake.

mapambano yanaendelea ila kwa kiongozi wa taasisi kukaa pale na kuzungumza ni kuwa anaiwwakilisha taasisi yake. Ndio maana wakati mwingine wanaoalikwa huwa hawafiki kwa kuhofia kutoa matamko
 
NSSF ni kisima cha kuchezea cha wana siasa wakitaka saa yeyote wanachota na kuzitumia hataulizwa kamwe na milele ndio imetoka hiyo!
 
Back
Top Bottom