Fao la kujitoa bado ipo LAPF, meneja wake asema sheria ya kuliondoa ilihusu mfuko mmoja tu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
LAPF imewatoa hofu wanachama wake kuwa faomla kujitoa bado linatolewa na mfuko huo kisheria
Meneja wa mafao wa mfuko huo Mkeyenge Ramadhani amesema ili kutoa kitu chochote ambacho kipo kisheria ni lazima upitie mchakato wa kisheria ili kukiondoa.



Amesema mchakato uliofanyika bungeni ulikuwa ukihusu mfuko mmoja tu kufuta fao hilo
Pia amesema imejipanga kutekeleza vyema sera ya viwanda na sasa bodi yake ya wadhamini imeadhinisha uwekezaji kwenye viwanda viwili ikiwemo kiwanda cha nyama Morogoro na kiwanda cha nguo Musoma.

Amesema kuna changamotoya waajiri kuwalazimisha wafanyakazi waokujiunga na mifuko mingine japokuwa sheria hairuhusu hilo
 
Ramadhani Mkeyenge, namkumbuka sana huyu kaka, moja ya watu waliobarikiwa usikivu mnoo na moyo wa kusaidia wengine binafsi alinisaidia sana Kipindi naanza kazi, yaani mpaka hii Leo I wish nikutane nae nimzawadie hata shati M/Mungu amjaalie katika shughuli zake za Kila siku
 
Ilihusu NSSF kwa sababu wanaochangia huko ni kwa lazima na ni makampuni binafsi ambayo wafanyakazi wao wengi hata mikataba hawana na huacha kazi mara kwa mara kwa hiyo hawana muda wa kujuwa haki yao ni ipi au kufuatilia sh 153,232/55 kwa muda wa miaka 30 haupo hivyo wameamua kudhulumu.
 
Ilihusu NSSF kwa sababu wanaochangia huko ni kwa lazima na ni makampuni binafsi ambayo wafanyakazi wao wengi hata mikataba hawana na huacha kazi mara kwa mara kwa hiyo hawana muda wa kujuwa haki yao ni ipi au kufuatilia sh 153,232/55 kwa muda wa miaka 30 haupo hivyo wameamua kudhulumu.
Hiyo LAPF wengi pia ni binafsi, 70 %
 
Wakuu nimesoma kwenye mwananchi kwamba Mfuko wa LAPF wao fao la kujitoa lipo. kumbe basi hawa NSSF ni wao wameamua kuzuia mafao ya watu
b8cc212d96c85c2930cd3e504be91bad.jpg
 
Inabidi watu wahamie LAPF na kama kuna kuhamisha pesa kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine niambiwe
 
wakuuu naomba kuuliza .. kwa kauli ilotoka jana bungeni kuzuia fao la kujitoa..je lapf wataendelea kutoa fao hilo?
 
KADADADEKI ZAO NSSF

SIJUI KITU GANI KILINITUMA HUKO....................... WAPUUZI SANA
 
Back
Top Bottom