Je, umedondosha simu yako kwenye maji au imeingiwa maji?. Usipate tabu, Ukichukua hatua za haraka unaweza ukaiokoa isiharibike.
Hatua ya kwanza kabisa itoe kwenye maji haraka iwezekanavyo kwani inavyozidi kukaa kwenye maji ndivyo maji yanazidi kuingia na kusambaa sehemu mbalimbali za simu. Ukishaitoa kwenye maji usifanye yafuatayo.

- Usiiwashe
- Usibonyeze button yoyote
- Usiitikise au kuipigapiga kwenye kiganja kwani hii inaweza kusambaza maji zaidi.
- Usiipulize kwani unaweza kusambaza maji zaidi.
- Usiiweke sehemu yoyote yenye joto kama vile kuianika juani, kuiweka kwenye dryer au microwaving.
- Izime kwa kutoa betri ili kuzuia shoti.
- Toa kava, line (SIM card) na memory card.
- Tumia kitambaa au taulo yenye uwezo wa kunyonya maji. Epuka kukausha kwa kufuta kwani unaweza kusambaza maji zaidi.