Fanya vitu roho yako inavyokutuma

laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
834
1,060
Habari,Ni mtazamo wangu,kuchangia ruksa.Kwenye hii dunia jitahidi kufanya jambo ambalo roho yako inakuambia,jambo ambalo litakufurahisha wewe,ili mradi usivunje sheria,usimuumize mtu,unapokua kazini au mtaani jitahidi kufanya yale yanayokuhusu tuu,usidandie kila jambo,hii imewaletea matatizo wengi-kama ni kumsaidia mtu jitahidi umsaidie kwa kadiri ya uwezo wako na utabarikiwa(mpende jirani yako kama nafsi yako).

Usipende kuingilia maongezi ambayo hukushirikishwa,subiri wakihitaji mchango wako watakuambia,ukifika bar ukakuta watu wamekaa kikundi wanapata vyao,waache wana jambo lao,we wasalimie tafuta kona yako fanya kilichokuleta wakihotaji company yako watakuita.

Sasa kuna wale majamaa wa kukosoa hahaha yaani akiona mtu kanunua gari utasikia duh sasa kanunua gari gani hii inakula mafuta kama nini,si bora angenunua ist,huyu unakuta hata baiskel hana,angehitaji ushauri angekufuata umshauri anunue gari gani.binadamu hutawaweza hakuna zuri kwao refer story ya punda na mwenye punda.

Jipende na penda sana familia yako,familia yako itakua na we we wakati unakazi na wakati huna kazi,the moment umefukuzwa kazi na uezi kuzungusha round ndo utajua aina ya marafiki uliokua nao,ukiumwa watakuletea matunda Siku chache,watachoka,ila mkeo/mumeo na watoto hawatachoka abadani,penda sana familia yako ndugu,wekeza muda mwingi kwao,unakaa bar mpaka saa nane usiku ukirudi hujui wanashida gani,wamekula nini as long as umeacha kodi ya meza asubuhi,una assume every things are okay,sio kweli invest muda wako kwa familia yako, hii inajenga bond nzuri na mkeo na watoto wako.

Wajali wazazi wako wote wawili utapata baraka nyingi sana hapa duniani,ukikosa cha kuwatumia kama wako mbali,wajulie hata salamu,ni faraja kubwa sana kwao,wewe unaeza kuona ni kitu kidogo sana.
 
Kichwa cha habari hakiendani japo ujumbe mzuri sana!
 
Back
Top Bottom