Fanya maamuzi magumu wewe msomi usiye na ajira, utafanikiwa sana

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Habari wasomi wote mnaoteseka na suala la ukosefu wa ajira.

Ushauri: Umehitimu chuo ngazi ya Astashahada, Stashada au Shahada na umehangaikia ajira kwa zaidi ya miezi 24 (2yrs)?.
Kama jibu ni yes. Basi chukua uamuzi mgumu wa kuchoma moto vyeti vyako kisha ingia mtaani au shambani.
Utafanikiwa zaidi kwakuwa wewe utakuwa na maarifa zaidi ya yule utakayemkuta field huko.

Sasa hivi ukiingia mtaani au shambani si rahisi kwako kufanikiwa kwakuwa utakuwa unafanya kazi huku unawazia ajira na shetani anakuonyesha marafiki zako waliopata shavu B.O.T, TRA, NCCA, TANAPA, NEC na TPA mwishobl unabaki kusononeka tu na kuanza kumlaumu mjomba kuwa hajakuvuta TISS.
Ukificha au kuvitupa vyeti vyako mbali kabisa nakuhakikishia utatoboa haraka zaidi ya yule best yako aliyekupa lift juzi na SUBARU yake huku ametinga kombati zake za JWTZ.

Povu linaruhusiwa.
 
Imeongea pointi sana lkn umeharibu hapo kwenye kuchoma vyeti.
Vyeti vihifadhiwe sehemu ambayo sio rahisi kuviona kila siku alafu unaingia kitaa mguu pande mguu sawa.
 
Sichomi vyeti vyangu kwasababu hivi vyeti ni motisha kwa wanangu

nikiwambia nimesoma na bado nafanya hivi waelewe,maana ntakua na mifano hai

nikiwambia tu baba yenu nimesomaga ila siwaonyeshi hata ka certificate ka ushahidi

mitoto ya saivi itanisema kimoyo moyo (baba muongooo,ukute kaishia form 1 B) so

na yenyewe haitosoma,ila kwa mifano hai wakaona vyeti,wakaona Grade za mshua (wataelewa)


Naunga hoja Mkono na miguu na mwili pia Ukipenda vyote naunga hapo.
 
Pia kuna zile shule za international zile unaenda omba kazi ya kushinda na kuwaangalia watoto wakiwa break unaacha lidegree lako kabatini unageuka bata kwa kucheza na watoto mwisho unatoka mkuu
Ndio zipoje hizo kazi.
 
Ndio zipoje hizo kazi.
Mkuu miaka ya nyuma nilienda pale iringa international school ipo gangilonga na degree yangu nikaomba kazi ya kuwa nawapatia uangalizi watoto na kusafisha ofisi yani kazi yako ni kuhakikisha watoto hawapati majanga wanapocheza pia unacheza nao simple as that.....

Hii ni kazi ya mtu ambae hata degree ila niliifanya nikawa vizuri sana kiuchumi ajira ikaja badae badae ila nikiwa nimechomoka na kimtaji kizuri tu
 
Si shauri vyeti kuchomwa kama asemavyo mdau, huwezi jua saa au siku vitakavyokutoa, nimemaliza Chuo 2010 (UDSM) vyeti vimenipatia ajira 2017, Am a living testimony...
 
Back
Top Bottom