“Fanya kazi halisi ili kutangulia mbele” - Rais Xi Jinping wa China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1.jpg

Xi Jinping, Mwaka 1989 alipokuwa Katibu wa Kamati ya Chama ya Eneo la Ningde la Mkoa wa Fujian alishiriki kazi kijijini.

“Maneno matupu yanaleta madhara kwa taifa, juhudi halisi zinastawisha taifa.” Siku 15 tu baada ya kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Bw. Xi alieleza nia yake ya kutimiza ndoto ya China kwa juhudi halisi wakati alipotembelea Maonesho ya “Njia ya Ustawishaji wa Taifa”.

“Fanya kazi halisi, ili kutangulia mbele.” Bw. Xi siku zote anasisitiza umuhimu wa kufanya kazi halisi. Amewaagiza maofisa wazingatie masuala yanayofuatiliwa zaidi na watu na kufanya kazi kadhaa zenye ufanisi halisi. Anaona bila utekelezaji halisi, mpango mzuri wowote ni ndoto tu.

2.jpg

Xi Jinping mwaka 1979 alipofanya kazi katika Ofisi ya

Kamati Kuu ya Kijeshi.

Alipofanya kazi katika Wilaya ya Zhengding mkoani Hebei, Bw. Xi alisema, njia muhimu ya kuondoa umaskini ni kupata watu hodari. Kwa hiyo aliwahi kutafuta mwenyewe watu hodari mara nyingi na kutunga mwenyewe mpango wa kuwatafuta watu hao kote nchini China.

Mwanzoni mwa mwaka 1983 ambapo yalikuwa majira ya baridi, Bw. Xi pamoja na Bw. Cheng Baohuai aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Zhengding, walienda mjini Shijiazhuang kumtembelea mtafiti mmoja wa vipodozi vya kimatibabu. Kwa kuwa hawakujua anwani ya nyumba yake, walipiga hodi nyumba moja baada ya nyingine lakini walishindwa kumpata. Ilikuwa baada ya saa nne usiku, Bw. Xi alikuwa anaita hapa na pale kwa sauti kubwa mpaka ampate. Waliongea hadi alfajiri ya siku ya pili, mtafiti huyo alikubali kuhamia wilayani Zhengding na mradi wake wa utafiti, baadaye mradi huo uliiletea wilaya hiyo faida ya Yuan laki tatu kwa mwaka.

3.jpg

Xi Jinping alipokuwa naibu meya wa Mji wa Xiamen mkoani Fujian alifanya ukaguzi nje ya nchi

Baada ya kufika mjini Ningde mkoani Fujian, Bw. Xi alitatua matatizo mengi kwa kufuata hali halisi. Ningde inajulikana kama “Maskani ya Samaki Wakubwa Wanjano”, ambao ni watamu na wanapendwa na watu. Zamani samaki wa aina hiyo hawakuweza kufugwa. Bw. Xi aliagiza kufanya utafiti kwa hali na mali ambao hatimaye ulipata mafanikio. Ufugaji wa samaki wa aina hiyo uliwaongezea mapato wakulima kwa kiasi kikubwa.

Bw. Xi alisisitiza kuwa ofisi za Chama na serikali zinapaswa kufanya kazi kwa kufuata maslahi ya umma. Alipokuwa mjini Fuzhou, alitaka “mambo maalumu yatatuliwe mara moja na kwa njia maalumu”. Marekebisho ya kazi za serikali yalivutia makampuni mengi ya Taiwan na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa Mji wa Fuzhou. Mwaka 1992, alichagua makampuni 12 makubwa na ya ukubwa wa kati ya kitaifa kuyataka yafuate mfumo wa uendeshaji wa makampuni yenye uwekezaji wa nje. Aidha alihimiza kutunga na kuchapisha “Mwongozo wa Shughuli Mjini Fuzhou” na “Mwongozo wa Utaratibu wa Shughuli za Umma Mjini Fuzhou”, ili kurahisisha shughuli za wawekezaji kutoka nje na maisha ya wakazi wa huko, na kuongeza ufanisi wa kazi.

4.jpg


Mwezi Agosti, 1993, Xi Jinping alipokuwa Katibu wa Kamati ya Chama ya Fuzhou mkoani Fujian aliwapokea watu kwenye Eneo la Taijiang mjini Fuzhou katika siku ya viongozi kusikiliza maoni yao.

Mwezi Agosti mwaka 2002, kupitia vyombo vya habari vya serikali kuu, Bw. Xi alifanya majumuisho na kueneza kwa nchi nzima “Maarifa ya Jinjiang”, yaani “Kufuata mwelekeo wa soko, kuhimiza maendeleo, kwa uaminifu, kutegemea nguvu bora ya Jinjiang, kuimarisha kazi ya serikali ya utoaji wa huduma, kufuata moyo wa kuchapa kazi bila kujali chochote na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa eneo la wilaya kupitia kustawisha makampuni ya binafsi”. Mwaka huo, baada ya kufanya uchunguzi na kuzingatia kwa makini kazi ya Mji wa Nanping ya kuwapeleka maofisa kufanya kazi vijijini, Bw. Xi alitoa tena wazo la “Kuwapeleka maofisa wa ngazi ya juu kufanya kazi mashinani ili kuimarisha msingi wa kazi ya vijiji”, na kuanzisha utaratibu wa kuwapeleka wajumbe maalumu wa teknolojia, makatibu wa matawi ya Kamati ya Chama ya vijiji na wasaidizi wa mawasiliano ya bidhaa wa kufanya kazi vijijini. Uenezaji wa “Utaratibu wa Nanping” mkoani Fujian ulizidisha uhusiano wa karibu kati ya maofisa na watu vijijini, na kuwafanya maofisa wa huko wazoee kufuata mwelekeo wa “kwenda kwenye jamii za mashinani mara kwa mara badala ya kwenda kwenye idara za ngazi ya juu kujipendekeza, na kujitahidi kujipatia ufanisi wa kazi badala ya kutegemea uhusiano mzuri na watu wenye maamuzi”.

5.jpg


Mwezi Disemba, 1995, Xi Jinping alipokuwa Naibu katibu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Fujian na Katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Fuzhou alishiriki kwenye kazi ya kuimarisha boma la kuzuia mafuriko katika eneo la mtiririko wa chini wa Mto Minjiang wilayani Minhou.

Alipofanya kazi mkoani Zhejiang, Bw. Xi alisukuma mbele ujenzi wa “Zhejiang yenye usalama”, “Zhejiang inayolinda mazingira”, “Zhejiang ya kiutamaduni”, “Zhejiang inayotawaliwa kisheria”, na ujenzi wa mkoa wenye nguvu ya uchumi wa bahari”. Njia pekee ya kutimiza malengo hayo ni kufanya kazi halisi.

Bw. Xi alitilia mkazo kutunga mpango kwa kufuata hali ya jumla, huku akienda kwenye jamii za mashinani kufanya utafiti, akachagua Kijiji cha Xiajiang cha Tarafa ya Fengshuling ya Wilaya ya Chun’an kilichoko kwenye eneo lililoko nyuma kimaendeleo la kusini magharibi mwa Mkoa wa Zhejiang kuwa kituo chake cha kufanya mawasiliano.Ndani ya miaka miwili, Bw. Xi alikwenda katika kijiji hicho mara tano, alikichukulia kuwa ni dirisha la kufahamishwa hali ya utekelezaji wa maamuzi ya serikali ya mkoa katika jamii ya mashinani. Kijiji cha Xiajiang kiko sehemu ya milimani, umbali wa kilomita zaidi ya 60 na Mji wa Wilaya, hali ya mawasiliano ya huko ilikuwa ni ngumu. Kila alipoenda kufanya uchunguzi na utafiti, Bw. Xi alifika nyumbani kwa wakulima na mashambani kusikiliza maoni yao.

6.jpg


Mwezi Septemba, 2007, Xi Jinping alipokuwa Katibu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Shanghai alitembelea Shule ya Qiyin ya Mtaa wa Minhang, akiongea kwa upendo na wanafunzi wenye matatizo ya usikivu.

waka 2007, Bw. Xi alianza kufanya kazi mjini Shanghai. Mwezi mmoja baada ya kushika madaraka, alifanya utafiti bila mapumziko kuhusu maisha ya wakazi na maendeleo ya uchumi wa mji huo, Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai, na mapambano dhidi ya ufisadi.

Alikuwa na mazungumzo na maofisa wengi, na kusikiliza maoni ya wakazi wengi mjini humo, baadaye akaitisha kwa mafanikio Mkutano wa 9 wa Wajumbe wa Chama cha Kikomunisti wa Mji wa Shanghai, kutuliza hali ya mambo ya mji huo kwa wakati huo, kuwafanya maofisa na wakazi waongeze ari ya kuchapa kazi, na kujenga upya sura ya Shanghai, hayo yote yamewaoneshea watu mpango mpya wa maendeleo ya mji huo katika miaka mitano ijayo.

“Katibu wa Kamati ya Chama ya wilaya ni lazima atembelee vijiji vyote, Katibu wa Kamati ya Chama ya mji ni lazima atembelee tarafa na wilaya zote, na Katibu wa Kamati ya Chama ya mkoa ni lazima atembelee wilaya zote na miji yote.” Alipofanya kazi wilayani Zhengding, alitembelea vijiji vyote vya wilaya hiyo; alipokuwa mjini Ningde, alitembelea wilaya 9 zote ndani ya miezi mitatu; alipofanya kazi mkoani Zhejiang, alitembelea wilaya na miji yote 90 katika mwaka mmoja na zaidi. Baada ya kufika Shanghai, alitembelea maeneo na wilaya zote 19 ndani ya miezi saba. Na baada ya kuanza kazi katika Kamati kuu ya Chama, ametembelea miji ya mikoa 31 ya China.
 
Ukiongea sana unaziba nafasi ya kutenda. Watu wanaoelewa wanataka Nini kwa muda fulani huwa hawaongei sana, wao washajua kuwa ulimwengu haumzawadii mropokaji bali mtendaji, ndiyo maana wenzetu wametuweka kwenye mtego wa kutuletea headline nyingi za matukio mengi ili kutuzubaisha kwani wanatujua ni wazee wa porojo huku wao wakifanya kazi.
 
Back
Top Bottom