Fanya hivi kuepuka kibarua kuota nyasi kama unafanya kazi kwa ndugu

Tatizo la Fikra za Kimasikini ndio hilo. Mtu anakufanyia kazi zako zinakwenda vizuri, mpe muda wa kuyafurahia maisha pia ili apate munkari wa kupiga kazi zaidi. Sio unamfanya mtu mtumwa ashindwe hata kupendeza
Anakubana mwanzo mwisho hakuachi upumue hata kidogo eti anaogopa kuibiwa.Akikuona umependeza ni kosa kubwa hata kama hatakuambia ila huo mdomo atakavyovuta au huo uso ataukunja kweli kweli akihisi ameibiwa na ukiona hivyo jiandae kufukuzwa au kutangazwa vibaya kwamba wewe mwizi.
 
Huo Utumwa tena wa mkoloni mweusi!!!!
Baada ya kuwa jobless muda mwingi niliamua kurudi nyumbani na kufanya kazi kwenye miradi ya baba yangu (biological father). Matusi, maneno, majungu yalinifanya niache sababu hakutaka nipate maendeleo yoyote yale aisee niliamua nijiongeze kwenda upande wa kushoto tu.
 
Hahaha nimekumbuka nilikuwa naishi kwa aunt yangu ukijipulizia unyunyu ni kosa Kama la kukutwa na bangi anasema iweje baba mwenye nyumba hatumii unyunyu afu we kijana unatumia whaaaay? Haha haha afu in while ukikatiza anasema unanuka kwapa hahaha
duh
 
7:iba kijanja kama no duka LA wholesale na retail Ukiuza kitu retail unaandikia wholesale
 
Juzi sis kanitumia iPhone 6+ manyanyaso yameongezeka sina hamu na kazi nimekaa NAYO miezi 3 nimeona niiuze tuu maana nlisikia shemeji akimwambia bro huyu mdogo wako atakuwa anakuibia
 
Umenikumbusha Kuna kijana alikuwa tempo Basi bosi wake injinia alikuwa mtu wa viwanja balaa.Siku wamekutana viwanja tempo akang'oa mhudumu aliyekuwa anatakwa na boss.Kesho yake kila kazi aliyoleta anadai kakosea
Nikamuuliza vipi mbona hivyo akasema boss kamwagwa Basi ndiyo visa hivyo.
 
MWAKA 2005 NILIKUWA NAFANYA KAZI NIKIWA NA KA-ADVANCED DIPLOMA YA T.I.A, BOSI WANGU ALIYENIPA MCHONGO WA KAZI TENA ANA MBA YA MZUMBE ALIPOONA NAANZA KUPATA MAENDELEO AKAANZA KUNILETEA ZENGWE HADI NIKAACHA KAZI KWA MAJUNGU YAKE TENA MSHAHARA WAKE ULIKUWA MARA 2 YANGU TENA ALIKUWA NA MAPOSHO NA MASAFARI KIBAO...WAAFRIKA NI KIZAZI CHA JEALOUS SANA..WIVU, CHUKI, MAJUNGU VINATUTAFUNA SANA.
2005 dah!! Mim ndo niko darasa la pili...

Ila umetisha sana mze baba...



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom