Fanya haya kuokoa maisha yako kwenye simu

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
fanya haya kuokoa maisha yako kwenye simu

Wengi wetu siku hizi tunaweka password / pattern katika simu zetu kwa ajli ya kuweka ulinzi katika simu, hali hii humpa mtu wakati mgumu wa kufungua simu yako bila ruhusa yako.

lakini umeshawahi kujiuliza vip siku umepata ajali , umepoteza simu , unaumwa mpaka ukisha simu umeshindwa au hata umekufa watu watatoaje taarifa zako.

siko hapa kusema/ kukuombea kufa lakini binadamu matatizo ndo maisha yetu hatuwezi kuyaepuka Ila ni vizuri kuweka vitu vyako ulinzi

lakini fikiria siku umetokewa na tatizo huko eneo la public uwezi kushika Wala kuongea kwenye simu yako watu wanataka kukupa msaada lakini hawawezi kutokana simu yako kuweka password / pattern.

Leo nimeamua kuwapa Elimu ambayo itasaidia kuokoa maisha yetu wakati unapopatwa na tatizo simu yako unaweza kukuokoa we fanya kusoma guy ujumbe

ikiwa simu yako huko kwenye locked kwa kawaida hukuambia weka password hili kuweza kuanza kutumia lakini chini yake Kuna neno EMERGENCY

nimeandika kwa herufi kubwa hili huweze kuliona vizuri sawa . sasa fanya hivi hili kuokoa maisha yako sawa .

kwenye emergency gusta ingia humo alafu utaona neno EMERGENCY information gusa mara mbili (2 times) utaona pencil icon juu upande wa kulia ingia hapo

Kisha bonyeza sehemu ya edit alafu baada ya hapo bonyeza sehemu ya contact ambayo unataka kusave namba muhimu ambazo uta save pale unapopatwa tatizo basi watu wataweza kuwapigia watu wako.

nakushauri hakikisha unaandika namba ambazo zikoo active mean zinapatikan mda wote na anapokea maana hitakusaidia kutoa taarifa haraka kwa ndugu zako au rafiki zako.
maana unaweza kusave namba nyingi sana wewe.

Kumbuka
kupiga namba kwenye emergency ni rahisi ikiwa kwenye lock simu yako gusa kwenye emergency alafu emergency information baada ya hapo utaona namba zote ulizo zi save hapo kwaiyo utapiga bila ku unlock simu ya muhusika.

roho ya mtu inaweza kusaidiwa kwa kufanya hivi

Free to share unaweza kuokoa maisha ya mtu

kwa masuala mbalimbali kuhusu teknolojia kwa lugha ya kiswahili karibu katika page zetu ujifunze Bure

Instagram

YouTube

Facebook

Twitter
IMG_20210521_223221_425.jpg
 
Back
Top Bottom