Fanya haya kuepuka kuungwa kiholela katika magrupu ya WhatsApp

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Kumekuwa na ongezeko la watu ku-adiana au kuingizwa katika magrupu ya WhatsApp, wakati mwingine wanaofanya hivi hata huwajui na utalazimika kusubiri maelekezo.

Ili kukabiliana na hilo kuna namna ya kufanya. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika whatsApp kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Settings, ikifunguka bonyeza Account kisha Privacy.

Ukibonyeza hapo itafunguka yatakuja maelekezo mengi, wewe bonyeza palipoandikwa Groups, utakuja ukurasa mwingine wenye maelezo ya kukutaka uchague nani atakayeweza kukuingiza kwenye magroupu ya WhatsApp.

Yatakuja Everyone, ambapo ukichagua sehemu hii kila mtu atakuwa na nafasi ya kukuadi.

My Contacts, ukichagua hii utawaruhusu watu wote ulio na namba zao kwenye simu yako kuweza kukuingiza kwenye magroupu ya WhatsApp.

My contacts Except. Ukibonyeza hapa utakuwa na nafasi ya kuchagua ni watu gani au mtu gani mmoja au zaidi wataweza kukuadi kwenye magroupu ya WhatsApp. Pia unaweza kuzuia watu wote kwa kuchagua alama ya tiki iliyopo juu upande wa kulia ndani ya majina yatakayofunguka baada ya kuchagua sehemu hiyo.

Uamuzi ni wako, ila kama hutaki usumbufu chagua hiyo ya mwisho, kwani mtu akitaka kukuingiza atalazimika kukushirikisha kwanza kabla ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom