I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,892
- 10,643
- Weka umakini katika rangi ya moto wa gesi uliopo kwenye jiko lako.
* Kama moto una rangi ya bluu inamaanisha kila kitu kipo vizuri na joto linalozalishwa na huo moto ni nyuzi joto kuanzia 1,500°C hadi 1,700°C
* Kama moto wako ni mwekundu au rangi ya chungwa, hii (inawezekana*) umeuziwa gasi iliyochanganywa na gesi ya Oksijeni kwa kiwango kikubwa hali hii itakupa uzito ule ule wa mtungi ila itakupelekea kupata moto wenye jororidi ndogo au pungufu kwa nyuzi joto 900°C hadi 1,200°C. Hii ina maana gani? Ni kwamba utahitaji kufungua gesi zaidi kwenye valvu yako, matumizi yatakuwa makubwa kuliko uhalisia na kukufanya umalize gesi kwa muda mfupi.
#Lakini pia tambua: Upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye chumba unacho-pikia inaweza kusababisha gesi yako kubadilika rangi. Sehemu unapopikia hakikisha kuna mzunguko mzuri wa hewa ya oksijeni ili kurahisisha uchomaji mzuri wa gesi ya kupikia.
Endapo gesi hii isipochomeka vizuri basi huweza kusababisha uzalishaji wa hewa sumu inayojulikana kama Carbon monoxide.
KUMBUKA: Unatakiwa kila mara kufungua milango na madirisha sehemu unayotumia kupikia ili kuruhusu mzunguko wa oxygen ndani.