Fanya haya ili uweze kuchagua kozi sahihi chuoni

Gwamanga

Member
Jun 25, 2021
66
138
Binafsi nimebahatika kusoma chuo kwa Tanzania kilicho na kozi nyingi za Bachelor Degree kuliko vyuo vingine, Chuo kikuu cha Dodoma, Nilikuwa nasoma Shahada ya kwanza ya Ualimu katika ndaki ya sayansi asilia pamoja na hesabu(CNMS), Hivyo nimebahatika kula, kuishi, kujadili, kuongelea na kulala chumba kimoja na kaka zangu au wadogo zangu wa kozi nyingine.

Mfano nimeishi na watu wa Kozi ya Fizikia, Biologia pamoja na watu wa Aquaculture, nilichojifunza katika kipindi hicho ni kuwa kuna Majuto makubwa kwenye kukosea kuchagua kozi, wengi Tunasoma vitu ambavyo hatujavifanyia tafiti, au hatujui chochote kuhusu kozi hizo au Tunafuata makundi, kiufupi Mtu yoyote aliyemaliza chuo Anasitahili kuyajua haya ili aweze kuchagua kozi sahihi.

1# Uchaguaji wa kozi haupaswi kufuata maoni ya mtu mwingine au kundi la watu Bali hupaswa kufuata ndoto za wewe Unayeomba kozi kwa kuangalia misingi binafsi uliyojiwekea (Malengo binafsi na ndoto zako), watu wengi humshauli muombaji wa kozi kuomba kozi fulani kwa kuangalia sana sana vigezo vya kuweza kupata mkopo wa chuo kikuu, au zamani walikuwa wanaangalia uwezekano wa kuajiriwa serikalini, sasa hivi zama zimebadilika kozi zinazofanya vizuri ni zile unazoweza kuzigeuza moja kwa moja kuwa Fani Bila hata ya kutumia njia mbadala.

2# Kozi sahihi huendana na chuo sahihi, chuo sahihi huendana na mahitaji sahihi, Mahitaji ya miundombinu, mazingira bora ya ujifunzaji na rasilimali nyingine, Akili iliyolelewa Mazingira halisi huwa halisi pia.

3# Kuwa na mentor (Mwalimu ) huyu atasaidia kukuelekeza perspectives za dunia kwani uzoefu wake unatosha kujua jinsi dunia inavyojiendesha, kumbuka Mwalimu Mzuri hukupa perspectives tu Maamuzi yapo juu yako.

4# Uchaguzi wa kozi huendana na ufaulu wako ima wa kidato cha sita au kwa baadhi ya kozi/ vyuo huangalia pia ufaulu wa kidato cha nne. Mfano Chuo kikuu cha Iringa mtu yoyote anaweza somea sheria lakini endapo alifaulu somo la kiingereza kidato cha nne pia ana vigezo vingine kulingana na mashariti ya TCU.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom