Fanuel Sedekia ni marehemu!

Nina huyu na ana umaarufu upi?

Nimeipata hii kutoka Michuzi. Naibandika kama ilivyo. Pengine itajibu kidogo swali lako mkuu mwanjelwa.

MWIMBAJI WA INJILI FANUEL SEDEKIA KATUTOKA
HABARI ZA KUSIKITISHA ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA MWIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI, FANUEL SEDEKIA, AMEFARIKI DUNIA JANA KATIKA HOSPITALI YA PORIYA TIBERIA, HUKO ISRAEL.
HABARI ZINASEMA MAREHEMU ALIKUWA AMELAZWA KWA WIKI TATU HOSPITALI HAPO AKISUMBULIWA NA KISUKARI PAMOJA NA NIMONIA. ALIKUWA HUKO KATIKA MSAFARA WA MAHUBIRI NA MCHUNGAJI MWAKASEGE.
MIPANGO YA KUULETA MWILI WAKE NYUMBANI KWA MAZISHI UNAFANYWA NA TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA HABARI ZINAPOTUJIA. KWA SASA KINACHOFAHAMIKA NI KWAMBA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE ARUSHA NA ATAKAPOZIKIWA BADO HAIJAJULIKANA KWANI YEYE KWAO NI KIGOMA.

MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMINA

Source:
Michuzi:
 
Alikuwa ni mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili kuna kanda yake alitoa yenye jina KATIKA IBADA,katika kanda hizo aliimba nyimbo ambazo zinavutia sana.
 
RIP Fanuel! Mungu awatunze watoto wake na mjane! Nawapa pole sana wote walioguswa moja kwa moja na msiba huu
 
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana libarikiwe. Tunaiombea familia yake, marafiki, wapenzi wa muziki wake wa injili na wote walioguswa kwa karibu sana na kifo chake. Mungu awape wafiwa faraja, nguvu, uvumilivu na kufuta majonzi mioyoni mwao.
 
Mmoja kati ya waimbaji mahili wa nyimbo za injili. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. RIP ndugu Sedekia.
 
Mungu wetu wa upendo na huruma,uilaze mahali pema peponi roho ya marehemu sedekia.apumzike kwa amani.
 
pumzika kwa amani, nasi twasubili zamu yetu ni vyema tukae tumejiandaa kwani hatujui siku wala saa.
 
Mhn...!
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi na atupe busara za kuweza kuyatengeneza maisha yetu sisi tuliobaki ili tuweze kuenenda kwa kadri ya mapenzi yake na hatimaye tu urithi ufalme wa mbinguni pale tutakapoitwa kwake.

Amen

....nimenyeshewa mvua ya baraka.......

.....will always remember what you preached thru gospel songs....
 
Namkumbuka sana,aliimba wimbo mmoja uitwao PASIPO MAONO niliupenda sana.
RIP Zedekia
 
Miaka hii miwili au mitatu iliyopita Wanamuziki mahiri watatu wa Muziki wa Injili wamefariki dunia.

2007- Emma Chichi
2008-Angella Chibalonza
2009- Fanuel Sedekia

BWANA alitoa na BWANA ametwaa jina lake lihimidiwe. Fanuel Sedekia ameacha Mjane na watoto wawili wadogo. Tumwinue mjane wa marehemu kwenye sala pamoja na watoto wake wadogo ili Mungu awatie nguvu na kuwafariji.

miongoni wa album zake Maarufu ni
1. Anaweza!
2. Unaweza tena!
3. Manukato (mpya ya mwisho)
 
Kwa kweli sisi wanadamu kila siku yatupasa tutafakari sana safari yetu hapa duniani! Muumba kutunyima kujua siku ya kutoweka kwetu ni mtihani mkuu kwetu.Huyu bwana nimefanya nae kazi kwa pamoja kwa mda mrefu yeye na bendi yake ya ETM mkoani Arusha! Kwa alivyokuwa kijana usingedhani kwamba anaweza kututoka.Tunatembea ni Marehemu.Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake libarikiwe.
 
ninaupenda sana Wimbo wake wa Nitaimba Halleluya wakati wote na ule wa Moyoni nimempata Yesu.....Mungu amlaze Pema Amen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom