Fantuzzi icd yazidiwa

vita

Member
May 4, 2011
80
95
Wadau,

nawaletea hoja nyingine amabapo FANTUZI ICD ,yard inayopokea makontena ya mizigo toka nje au kwa maana nyepesi ni mojawapo ya Bandari Kavu zilizoteuliwa na Kamishna wa Forodha kutunza mizigo inayotoka nje vkable ya kulipiwa kodi na ikishalipiwa wenyewe wanachukua.

Yard hii kwa sasa imezidiwa kwa kuwa na makontena mengi sana kupita uwezo .Pamoja na makontena ya mizigo,vile vile inatunza makontena matupu yanayokuwa yameshatolewa mzigo.Makontena hayo ya CMA na DELMAS shippinh lines inabidi yarudishwe hapo ili yatunzwe mpaka takaposafirishwa nje au kuwekewa mizigo mengine ya nje.

Kwa kuwa yard imejaa, magari yanayo beba makontena hayo yamekuwa yakikaa nje ya yard kusubiri kushusha kwa wastani wa siku nne hadi tano nje ya yard na maeneo yanayozunguka hapo.Kwa sababu magari ni mengi sana matokeo yake foleni ni kubwa barabara yote ya Mbozi Chang'ombe mpaka Port Access au Mandela road na yenyewe imejaa magari nhayo makibwa mpaka foleni inafika uwanja wa Taifa.

Imekuwa cni Shiidah !

Tabu hii imesababisha magari yakubeba mizigo mjini yapungue na kazi za watu zilale.

Na si hivo tu bali wenye magari hawataki kupakia mizigo ya meli za CMA na DELMAS !

Hii inaharibu juhudi za kujikwamua kiuchumi

Waziri wa Uchukuzi uko wapi ? Mzee Mwakyembe ? Watu wa Forodha mko wapi ? mnakula kipupwe tu ? SUMATRA mko wapi ? mnakaa kukimizana na vidaladala tu ? mambo ya msingi kama haya mnaachia yaende shaghala bhaghala ?

Polisi na Trafiki mko wapi ili muwahoji hao wenye Yard kwa niniwanasabisha foleni kubwa ! Ifungieni Yard hiyo ili yard zenye uwezo ndo zifanye kazi ati !
 

vita

Member
May 4, 2011
80
95
Issa michuzi uko wapi Mzee wa blog kapige picha utupie ! au we mpaka picha za wanasiasa tu ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom