Fani kimbilio kwa vilaza kwa sasa ni fani ya Utabibu na Udaktari

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,904
Uzalendo kwanza.

Kichwa cha habari kinahusika, miaka ya nyuma mtu ulikuwa ukifeli au kupata ufaulu hafifu unaambiwa hata ualimu umeshindwa? Lakini kwa miaka ya hivi karibuni naona trend imehamia kwenye fani ya Afya na Tiba.

Just imagine fani nyeti kama afya ila pass mark za udahili ni kuwa na D D D kwenye masomo yanayoitwa ya sayansi. Kuna watu watesema eti hiyo ni minimum pass mark lakini wanasahau kwamba wanafunzi wengi wanaangukia kwenye ufaulu huo na kudahiliwa ngazi ya Diploma alafu baadae wanakuwa Medical Doctor baada ya kujiendeleza.

Binafsi naamini mtu mwenye uelewa mdogo au ufaulu finyu hata ajiendeleze ataishia kuwa mtaalam wa average tuu. Bahati mbaya watu wa hivi ndio wamejaa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, na hii kazi saizi imevamiwa na kila mtu sio kazi ya wito na kujitoa bali kazi ya kusaka pesa.

Watu wenye uelewa finyu ndio tunategemea wagundue chanjo ya corona na kufanya operation complex, huu ni utani na kuchezea afya zetu. Hawa ndio mara nyingi unakuta wanagombana na kutoleana maneneo machafu na wagonjwa. Pia kwa watu wa hivi pesa mbele huduma inafuata. Binafsi nikienda hospital au dukani nikakuta vile vitoto vyenye D 3, huwa siko tayari vinihudumie kwenye ishu za msingi labda kupima pressure na maabara ila prescriptions hapana, huwa niko tayari kughairi huduma na kutafuta kwingine au nimpigie simu daktari naemfahamu hakupitia huu utaratibu wa D 3.

Kana kwamba haitoshi saizi kumezuka vyuo uchwara kila kona vinavyotoa haya mafunzo ya fani za afya almaarufu Health and Allied Sciences, sayansi zipi na pass mark za D? Hii fani inaonekana ni simple sana kuliko fani zingine tofauti na tulivyokuwa tunatishwa zamani kwamba fani za afya ni ngumu na zinahitaji watu wenye akili. Kwa sasa fani hii ni kama shamba la bibi na fani ya vilaza na zoa zoa.

Please regulatory authorities tunaomba mliangalie hili maana afya zetu ni muhimu sana.
 
Vilaza? Hizo D3 wanaozipata wame hustle kwa kiasi chao.

Pili uwezo wa mtu si kila wakati utapimwa kwa ufaulu wa darasani, wapo wenye hizo D's lakini wana uelewa mzuri kuzidi C au B ya kukariri na ndo sababu wanamudu masomo ya juu hadi MD.

Kwa kifupi, wataalam wa afya wanastahi kupewa heshima yao.

Utendaji mbaya sehemu ya kazi ni hulka tu ya mtu kutokana na malezi na pia mapungufu ya usimamizi sehemu ya kazi, sisi ngozi nyeusi kwa asilimia kubwa mpaka kusukumwa au kutishiwa ndo tunafanya kazi kwa weledi.
 
Vilaza? hizo D3 wanaozipata wame hustle kwa kiasi chao.
Umeongea point sana, hujakurupuka kama mtoa mada.

Mtoa mada bado amelala usingizi mzito akidhani ya kwamba waliofaulu darasani na kupata A ndio wana akili nyingi au ndio wameelewa sana fani yao kumbe kufaulu kwa kukariri makaratasi ni tofauti na uweledi.

Ukitaka kujua kwamba hili angalia kwenye wizara na taasisi mbalimbali katika nchi yetu,utakuta kuna watumishi humo walipasua sana ktk mitihani yao na wana CV nzito tena wengine wana Phd lakini ukija kwenye utendaji ni sifuri.

Yaani vitu vidogo vidogo tu vya kutumia logic hawavioni hadi Rais ndio aje kuwafundisha ndipo wanashtuka, tena unakuta Rais fani yake ni ya Kemia lakini anawafundisha watu wa fani tofauti ikiwemo na wanasheria.

Sasa hapo mtoa mada atasemaje
 
Vilaza? hizo D3 wanaozipata wame hustle kwa kiasi chao.
Duuh! Naona Madaktari na Manesi mnatambiana ufaulu kwa kulinganisha nyakati.

Nadhani hakuna taaluma ambayo siyo ya muhimu katika maendeleo ya Dunia. Wanaoenda kwenye sayari za juu siyo manesi na madaktari, wala wanasimamia uchumi wa dunia siyo madaktari. Hivyo, na sisi WACHUMI tuna heshima yetu na umuhimu wetu, wahandisi wana umuhimu wao na walimu wana umuhimu wao.
 
Back
Top Bottom