Fananisha Upanuzi wa uwanja wa ndege Dar vs Nairobi

selemala

JF-Expert Member
Feb 14, 2007
370
253
image.jpg

Nairobi

image.jpg

Tanzania.jpg

Dar.

Nimeona picha ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (Nairobi) nikaona kuna tofauti kubwa sana na upanuzi unaoendelea wa kiwanja cha Julius Nyerere (Dar).

Utofauti huu ni wa kimipango au wakimahitaji?

sources:
Kenya's $50 billion megaprojects - CNN.com
Terminal 3, Julius Nyerere Airport, phase 1 and 2 - Dar es Salaam, Tanzania | BAM International

..nadhani mtoa hoja angetafuta taarifa za ziada kuhusu mradi wa upanuzi JNIA.

..Hebu tuwasikilize wahusika wa mamlaka ya viwanja vya ndege kwa upande wa Tz wanasema nini kuhusu mradi wa terminal 3.

..nimewawekea video hapa chini kwa hiyo tuiangalie kwanza halafu tuone kama mradi unakidhi mahitaji na matarajio ya wa-Tz.

..angalia video hapa:

cc selemala, Ritz, The Boss, Ngongo, Geza Ulole, msemakweli, falcon mombasa, Kozo Okamoto , Eli79
 
Embu jiulize haya...
1.kwanini watanzania wengi wakitaka kwenda nje wanatumia uwanja wa jomo kenyatta??
2. Kwanini pembe za ndovu, twiga wanapitishwa uwanjani na hawaonekani wanaenda kukamatiwa uswis???
3. Kwanini wauza madawa wengi wanapita tz wanaenda kukamatiwa sauzi africa???
 
Hata ukiangalia kwa picha utaona upanuzi wa Dar uko juu,ila hoja ya msingi labda utuambie huo upanuzi ya Nairobi ili iwe na terminal ngapi ...........maana kwetu tunapanua ili kuwe na terminal 3 ?????? ( kumbuka uwanja wa ndege majengo ni nyongeza ila kikubwa na muhimu ni ukubwa wa uwanja na ubora wa huduma za anga na wasafiri )
 
Dar ni mkubwa katika Ramani yao naufananisha na Adis Ababa sio Mbaya.. Kwa majengo tuu sio landing lane huko sijui tuna eneo kiasi gani ana wao kiasi gani...
 
Hata ukiangalia kwa picha utaona upanuzi wa Dar uko juu,ila hoja ya msingi labda utuambie huo upanuzi ya Nairobi ili iwe na terminal ngapi ...........maana kwetu tunapanua ili kuwe na terminal 3 ?????? ( kumbuka uwanja wa ndege majengo ni nyongeza ila kikubwa na muhimu ni ukubwa wa uwanja na ubora wa huduma za anga na wasafiri )
Wewe kweli hamnazo!! Uwanja bila majengo ni sawa na choo bila maji!!!
 
Selemala ni kweli kuna tofauti kubwa ya shughuli Za upanuzi Kati ya uwanja wa Dar na Nairobi. Sababu kubwa ni kutokana na mahitaji ya viwanja hivi ya muda mfupi na mrefu ujao kutokana na makisio ya ukuaji au ongezeko la watumiaji (demand forecasting) au uamuzi wa kimkakati (strategy). Ndio maana utakuwa na master plan kuonyesha nini unategemea hapo baadae kama makisio yako yatauwiana kwa karibu na hali halisi ya kipindi ulichokisia muda unapofika au kukaribia. Dunia ya sasa hujengi kwa sifa maana ni gharama ambayo baadae inatakiwa ujue itajilipa vipi baada ya mradi kumalizika na kuanza kufanya kazi la sivyo itakuwa ni mzigo au jipu lisilotumbuka kwako. Soko la usafiri wa anga la Kenya ni karibu 70% ya soko lote la Afrika Mashariki. Ingawa hali hii siyo ya kudumu ( status quo) kwani soko hubadilika kutokana na mikakati ya washindani na kubadilika kwa vichocheo vya ukuaji wa soko (kumbuka Dubai). Kwa kifupi, kutokana na mahitaji yetu ya kipindi tulichojipangia, upanuzi wa uwanja unakidhi mahitaji yetu na hakuna haja ya show off ambayo itatugharimu bila sababu ya msingi. Hata hivyo maono yangu ni kuwa hali ya soko la usafiri wa anga la Tanzania na Afrika Mashariki inaweza kubadilika ghafla kutokana na uchumi utakavyobadirika (mafuta, gesi, na madini mengine). Sitaona ajabu Dar wakahama hapo na kujenga sehemu ingine uwanja mkubwa zaidi katika miaka 10 ijao kutokana na ukuaji mkubwa na wa ghafla wa soko la usafiri wa anga (tunza hii post you may need it in future to prove me wrong).
View attachment 317740
Nairobi

View attachment 317739
Dar.

Nimeona picha ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (Nairobi) nikaona kuna tofauti kubwa sana na upanuzi unaoendelea wa kiwanja cha Julius Nyerere (Dar).

Utofauti huu ni wa kimipango au wakimahitaji?

sources:
Kenya's $50 billion megaprojects - CNN.com
Terminal 3, Julius Nyerere Airport, phase 1 and 2 - Dar es Salaam, Tanzania | BAM International
Sel
 
Different structural designs. Kwa macho yangu Kenyatta airport is more modern in terms of structure, tunnels zimetengenezwa na hivyo ukitoka waiting hall, straight unaingia kwenye gate na tunnel moja kwa moja kwenye ndege...(Haya ni macho yangu coz sijaona structural design kwa undani). Pia nadhani it accommodates more planes kwa pamoja zaidi ya JKN International.
Lakini pia JKN itakuwa bomba, kinda Emirates international airport...teh teh!

Swali: nini kinaangaliwa zaidi wakati wa kujenga uwanja wa ndege? Je, ni landing size? Size ya majengo? Idadi ya ndege kwa mkupuo mmoja? Au ni structural design??
 
Ileje muweleweshe Sunsan kwa unavyoelewa wewe ndio maana ya hili jukwaa si kutukana wala kejeli..unalojua wewe sana mimi sijui na nachojua mimi inawezekana wewe haujui..tuishi ivyo Mkuu maisha yaende na tusiojua kitu tuendelee kujifunza..
 
Different structural designs. Kwa macho yangu Kenyatta airport is more modern in terms of structure, tunnels zimetengenezwa na hivyo ukitoka waiting hall, straight unaingia kwenye gate na tunnel moja kwa moja kwenye ndege...(Haya ni macho yangu coz sijaona structural design kwa undani). Pia nadhani it accommodates more planes kwa pamoja zaidi ya JKN International.
Lakini pia JKN itakuwa bomba, kinda Emirates international airport...teh teh!

Swali: nini kinaangaliwa zaidi wakati wa kujenga uwanja wa ndege? Je, ni landing size? Size ya majengo? Idadi ya ndege kwa mkupuo mmoja? Au ni structural design??

Eli landing size ni uwezo wa kutua ndege unazohudumia (runway capacity) ambayo inahusiana na ukubwa wa ndege hizo na frequency za utuaji na urukaji (landing and take off). Size ya jengo (terminal building) ni uwezo wa kuhudumia abiria wanaofika na kuondoka (arrival and departure). Hivyo huenda ukawa na ndege nyingi sana lakini abiria ni wachache (Arusha airport) na usihitaji jengo kubwa au ukawa na abiria wengi sana kutokana na ukubwa wa ndege unazohudumia (international airports). Structure design ukiwa na maana ya muonekano wa jengo (literary) ni ubunifu na hauhusiani na ukubwa wa jengo!!!
 
Wewe kweli hamnazo!! Uwanja bila majengo ni sawa na choo bila maji!!!
Bila shaka huu ndio uwezo wako wa uelewa,nimesema majengo ni "nyongeza" kwa maana si ktk vitu vinavyofanya uwanja uitwe mkubwa. ( majengo yanaweza kuwa kati no 4 au 5 ktk vitu vinavyoufanya uwanja uitwe wa kimataifa na ni bora.)
 
Structure ya JNIA inapendeza kwa macho kuliko JKIA. Tatizo la JNIA kwa nje imezungukwa na uswazi, mfano Lumo Kigilagila na Kitunda. Taswira ya jiji kwa juu unaweza ukadhani mnatua kijijini
 
View attachment 317740
Nairobi

View attachment 317739
Dar.

Nimeona picha ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (Nairobi) nikaona kuna tofauti kubwa sana na upanuzi unaoendelea wa kiwanja cha Julius Nyerere (Dar).

Utofauti huu ni wa kimipango au wakimahitaji?

sources:
Kenya's $50 billion megaprojects - CNN.com
Terminal 3, Julius Nyerere Airport, phase 1 and 2 - Dar es Salaam, Tanzania | BAM International

Tunatengeneza banda la kuku badala ya airport. naamini tuna wasomi wengi sana na viongozi wengi sana ambao wametembea nchi za wenzetu na kuona airports zao,hivi kweli hii best design ya kiwanja tunachohitaji kwa karne hii?labda kama ni kwa akili ya kusogeza siku na kwa akili ya mipango ya sasa tu hapo nitaelewa lakini kwa mipango ya naadae kalaghabao!kuliko kuwa na mabanda mawili yenye majina terminal 1&2 ni bora zingeunganishwa tukapata terminal moja ya maana.tungeweza Ku manipulate hali za kisiasa za majirani zetu tukawa hub kwa usafiri wa anga africa mashariki.tungetengeneza uwanja wa maana wenye huduma za kila aina kama ilivyo dubai,doha etc sisi ndo tungekuwa gateway.ndege zote za majuu zingetua kwanza hapa kwetu kwanza na abiria wakasambazwa kwa ndege za ndani kama ikivyo sasa nairobi.wabongo tunafikiria kula tu,tunawaza leo tu kesho itajijua.tulishadhihakiwa na mtu low life kama kagame kuhusu bandari but tupo tunachekacheka tu,ambavyo tungechukua dhihaka ya kagame kama changamoto tungekuwa hub kwa huduma za bandari africa mashariki na kati.dunia inakuws,biashara zinakuwa eti tunatengeneza uwanja wa kubeba watu milioni 6 kwa mwaka tunashangilia,hii ikiwa na maana after 5 to 7 yrs tutahitaki banda lingine in the name of terminal 4.kwanini tusijenge uwanja wa kuchukua hata watu mil 20 au hata 30 kwa mwaka ili tujue hatuta hitajo kujenga uwanja kwa miaka 30-50 ijayo?kwamba tunamaliza hili na kuhamia kwenye jingine.sisi kila siku tunakalia kufanya yale yale na kudai ni maendeleo
Kalaghabao
 
Samsun uwanja ni majengo na njia ya kurukia/kutua ndege (terminal side na air side) huwezi kuvitenganisha. Lazima vyote viuwiane!!!

Bila shaka huu ndio uwezo wako wa uelewa,nimesema majengo ni "nyongeza" kwa maana si ktk vitu vinavyofanya uwanja uitwe mkubwa. ( majengo yanaweza kuwa kati no 4 au 5 ktk vitu vinavyoufanya uwanja uitwe wa kimataifa na ni bora.)
 
Eli landing size ni uwezo wa kutua ndege unazohudumia (runway capacity) ambayo inahusiana na ukubwa wa ndege hizo na frequency za utuaji na urukaji (landing and take off). Size ya jengo (terminal building) ni uwezo wa kuhudumia abiria wanaofika na kuondoka (arrival and departure). Hivyo huenda ukawa na ndege nyingi sana lakini abiria ni wachache (Arusha airport) na usihitaji jengo kubwa au ukawa na abiria wengi sana kutokana na ukubwa wa ndege unazohudumia (international airports). Structure design ukiwa na maana ya muonekano wa jengo (literary) ni ubunifu na hauhusiani na ukubwa wa jengo!!!

Thanx kiongozi, lakini unapoongeza landing capacity(runway capacity), maana yake si kuwa unategemea more flights zitue hapo na hivyo kuongeza frequency za utuaji wa ndege kubwa, (japo hilo pia huchangiwa na uchumi wa nchi na jinsi inavyovutia foreigners kwa shughuli za kiuchumi na biashara). Naamini yote lazima yaende sanjari, ukiongeza landing capacity unategemea international flights zitue kwako, pia frequency iongezeke hence majengo lazima yatoshe ili kuweza ku accommodate abiria.
Structural design hiyo ni taste tu, lakini pia kwa complex airports lazima structure iwe more friendly ili kuhakikisha abiria hawasumbuki wakiwa transit au check in.
 
Back
Top Bottom