Family Photo

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,702
hadithi-ya-daudi-na-raza-pic-by-f-macha-e1307496913839.jpg
Inanikumbusha Mbaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Safi Sana Mr Daudi
 
Hahahaha AD hii picha we acha tu.

Sasa saa ya kwenda kwetu kwaheri Mwalimu kwaheri tutaonana keshoooo....

Ukitoka kwa Mr. and Mrs. Daudi Unaenda kwa Juma na Roza..
Viatu vya Roza hadi hii Leo Sijavisahau
 
Duuuuuu, enzi zile za 'nchi yetu inategemea vijana na vijana wenyewe ndiyo sisi, shikamoo mwalimu'. Nimekumbuka sana enzi zile hakuna ukimwi wala vitu feki au uchakachuaji.
 
Kitabu cha Juma na Roza mii nnacho pamoja na kile Bulicheka alivyokutana na mfalme Huihui wa Wagagagigikoko. Umenihuzunisha kwasababu nimekumbuka jambo baya ambalo ni hili. ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI, SHIKAMOO MWAAAALIMU.
 
umenikumbusha mbali sana , kuna yeyote anayekumbuka ile hadithi ya Ndoto za Kimweli?

Ndoto inaendelea, wageni wenye matumbo meupe walivyokuja, waliingia wakachukua mazao, watu, nyara na madini lakini mwenye nyumba aliwafukuza, baada ya Baba mwenye mji kufa, watoto waka wafuata wale wenye matumbo meupe waje wachukue walicho taka na wao watawalinda ... ndoto inaendelea....!
 
Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, Shkamooo mwalimu.
Break time walioishiwa na madaftari wanapanga foleni. Unaonyesha daftari lililokwisha,linasainiwa unapewa jipya. Mbio unawahi bulga
 
Umenikumbusha enzi tulikuwa tunaaga hivi parade "vijana mpo....., ndiyo tupo, tupo kabisa shauri chama chini ya uongozi wa umoja wa vijana, ccm juu, ccm juu, ccm juu kwa heri mwalimu.
 
Umenikumbusha enzi tulikuwa tunaaga hivi parade "vijana mpo....., ndiyo tupo, tupo kabisa shauri chama chini ya uongozi wa umoja wa vijana, ccm juu, ccm juu, ccm juu kwa heri mwalimu.
Duuh! nizamani sana, enzi hizo chipukizi yani tulikuwa tunaadaptishwa umagamba live
 
Hizi habari za kukumbushana kitambo hivyo ni nzuri...duh kitambo kweli
 
Dah umenikumbusha mbali miaka ile ya 80 yaani hapo ndio elimu ilikuwepo kama una ile ya Mandawa na Manenge mkuu iweke pia
 
Imenikumbusha enzi zile tunaimba ule wimbo "Are you sleeping x2, brother Musa x2, morning bell is ringing x2 ding dong ding x2"
 
Dah umenikumbusha mbali miaka ile ya 80 yaani hapo ndio elimu ilikuwepo kama una ile ya Mandawa na Manenge mkuu iweke pia[/QUOT

Yaani mkuu umefufua hisia za kitambo sana. Zama zile, hata kama hatukuwa na madarasa tulipata elimu. Siku hizi watu wanajivunia madarasa ambayo hayana elimu; Kwa upamde mwengine wa maisha: Mrs daudi bado anaonekana yuko fit hata baada ya kutotoa mara tatu. Siku hizi mhh!
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom