Family day ya Huzuni,na mfadhaiko kwa wafanyakazi wa Halmashauri ya Moshi(V)

papaa masikini

Senior Member
Mar 5, 2011
176
69
Ndugu wana Jf,naomba niwasilishe kilio cha wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini,wakiwemo walimu na manesi,na doctors,cha wao mpaka sasa hawajapata malipo yao ya mishahara ya mwisho wa mwezi huu,toka serikalini.
Na baada yakuanza zoezi lakufuatilia madai yao hayo,serikali husika imeshindwa kutoa maelezo yakutosheleza,huku kukiwa na uvumi kuwa fedha zao za mshahara zilipelekwa Igunga kwenye kampeni za CCM,na wengine wakidai kuwa zimeshikiliwa na kigogo mmoja wa serikali mkoani hapo,akizifanyia shughuli zake.
Hapo kesho ni sikukuu ya familia(Family Day)siku ambayo wafanyakazi wengi hukaa na familia zao wakifurahia,lakini kwa wafanyakazi wa Halmashauri ya Moshi (v) ni kilio.
Nawasilisha!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom