Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Kabla sijaendelea maana ya familia hapa ni baba, mama na watoto. Ndugu ili awe katika hii biashara inabidi mumfikirie sana yupo nanyi kwa shida na raha
Kwa hapa bongo tunaonaga kwa macho yetu jinsi ambavyo familia zinazofanya biashara kifamilia zinavyofanikiwa. Mfano mzuri ni kwa waarabu na wahindi wenye uraia wa Tanzania kama kina mo dewji, bakhresa, manji, rostam, n.k ambao baada ya mzee Mengi kufariki kwa haraka haraka wameshikilia listi ya top 10 namba moja hadi kumi kwa utajiri.
wahenga hawakukosea msemo wao "umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu", Watanzania wengi sana wanapenda kufanya biashara kivyao vyao pasipo kushirikisha familia kwa kiwango kinachoridhisha.
yani ndio maana kama baba ndie alikua ana biashara zake zilizolisha familia siku akifariki ndio watoto wanaanza kujua kwamba baba alikua na biashara fulani na fulani na huishia kuuza biashara za marehemu kwa sababu hawajui namna ya kuziendesha kutokana na baba yao kutowashirikisha au kuwashirikisha kwa kiwango kidogo.
Nachowashauri ndugu zangu watanzania tuwe tunashirikisha familia kwenye biashara, kama una mradi na umeona mdogo wako au kaka yako hana kazi kwanini usimuombe akusaidie?, kama wewe ni baba au mama wa familia unapungukiwa nini kuwashirikisha watoto wako au Mme/mke wako wajue A - Z ya jinsi biashara yako inavyofanya kazi na wakusaidie.
oneni wenzetu waarabu jamani, mtu akimaliza degree yake ni moja kwa moja kuutumia ujuzi wake ili aisaidie familia yake, lakini mtanzania akitoka chuoni yeye anataka aajiriwe au aanzishe biashara Yale hata kama kaka yake ana biashara kubwa.
Watanzania wengi hawatakagi habari ya familia wala ndugu kwenye biashara, na ikitokea wamewaweka maslahi yanakuaga madogo sana yanayokatisha tamaa wanafamilia kukusaidia, unakuta kaka mwenye biashara anaingiza milioni 20 kwenye biashara ila anamlipa mdogo wake laki 3 tu.
Damu ni nzito kuliko maji, muunganiko wa familia katika biashara una nguvu sana, Naombeni ambao mna biashara shirikisheni familia,
TUACHE UMIMI NA UBINAFSI, HATA SIMBA AKIWA KAJITENGA HAWEZI KUSHINDANA NA TIMU CHA FISI.