Family business ni bora kuliko kujiajiri mwenyewe; utengano ni udhaifu, umoja ni nguvu

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Kabla sijaendelea maana ya familia hapa ni baba, mama na watoto. Ndugu ili awe katika hii biashara inabidi mumfikirie sana yupo nanyi kwa shida na raha

Kwa hapa bongo tunaonaga kwa macho yetu jinsi ambavyo familia zinazofanya biashara kifamilia zinavyofanikiwa. Mfano mzuri ni kwa waarabu na wahindi wenye uraia wa Tanzania kama kina mo dewji, bakhresa, manji, rostam, n.k ambao baada ya mzee Mengi kufariki kwa haraka haraka wameshikilia listi ya top 10 namba moja hadi kumi kwa utajiri.

wahenga hawakukosea msemo wao "umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu", Watanzania wengi sana wanapenda kufanya biashara kivyao vyao pasipo kushirikisha familia kwa kiwango kinachoridhisha.

yani ndio maana kama baba ndie alikua ana biashara zake zilizolisha familia siku akifariki ndio watoto wanaanza kujua kwamba baba alikua na biashara fulani na fulani na huishia kuuza biashara za marehemu kwa sababu hawajui namna ya kuziendesha kutokana na baba yao kutowashirikisha au kuwashirikisha kwa kiwango kidogo.

Nachowashauri ndugu zangu watanzania tuwe tunashirikisha familia kwenye biashara, kama una mradi na umeona mdogo wako au kaka yako hana kazi kwanini usimuombe akusaidie?, kama wewe ni baba au mama wa familia unapungukiwa nini kuwashirikisha watoto wako au Mme/mke wako wajue A - Z ya jinsi biashara yako inavyofanya kazi na wakusaidie.

oneni wenzetu waarabu jamani, mtu akimaliza degree yake ni moja kwa moja kuutumia ujuzi wake ili aisaidie familia yake, lakini mtanzania akitoka chuoni yeye anataka aajiriwe au aanzishe biashara Yale hata kama kaka yake ana biashara kubwa.

Watanzania wengi hawatakagi habari ya familia wala ndugu kwenye biashara, na ikitokea wamewaweka maslahi yanakuaga madogo sana yanayokatisha tamaa wanafamilia kukusaidia, unakuta kaka mwenye biashara anaingiza milioni 20 kwenye biashara ila anamlipa mdogo wake laki 3 tu.

Damu ni nzito kuliko maji, muunganiko wa familia katika biashara una nguvu sana, Naombeni ambao mna biashara shirikisheni familia,

TUACHE UMIMI NA UBINAFSI, HATA SIMBA AKIWA KAJITENGA HAWEZI KUSHINDANA NA TIMU CHA FISI.
 
WaTZ wenzetu muwe Kama sisi.. maana tumezaliana na kuishi pamoja kwa miongo mingi..vipi? Na iwejee mushindwe kuiga wajomba zenu almaarufu "Waarabu" ?? Tunawrza wapa somo na michongo namna ya kuShare!!
 
Tatitizo familia zetu zinakatabia kakutawanyika yani kila mtu akajenge Nyumba yake, ukijumlisha tuna kasumba ya kuchukiana na kuchukia mafanikio ya wenzetu....

Wenzet hukaa zaid pamoja, Nyumba za Familia unakuta familia ata, Mzee Akifariki anakabiziwa Mmoja ndo kiongozi wa Familia na mali yote
 
FYI... Juu ya yote:- tulitaifishiwa, tulifilisiwa, tulibambikiziwa, tulilaaniwa, tulisingiziwa na tulipakiziwa.... Lakini Mungu si Athumani hutazama na kuhukumu atakavyo... Together twaweza unganisha milima!!
 
Tatitizo familia zetu zinakatabia kakutawanyika yani kila mtu akajenge Nyumba yake, ukijumlisha tuna kasumba ya kuchukiana na kuchukia mafanikio ya wenzetu....

Wenzet hukaa zaid pamoja, Nyumba za Familia unakuta familia ata, Mzee Akifariki anakabiziwa Mmoja ndo kiongozi wa Familia na mali yote
Mkuu mbona wazungu wanafanikiwa na huwa hawaishi pamoja?
 
Mkuu mbona wazungu wanafanikiwa na huwa hawaishi pamoja?
Ata sisi tunafanikiwa pia ila ela azivuki kizaz chapili cha 3 mkuu....

Kuna familia ya Rockerfellah au Rotch Kids tangu 1800's mpaka leo bado wanaukwasi na upo kifamilia unazani wangegawana kila mtu ale kona wangekuanao mpaka leo mkuu.....?

Ao wenzetu mpaka wanaona wao kwa wao ili mali zisitapakae
 
Tiririka mkuu, ongeza nyama
Partnership Ina historia kubwa...na si Lazima muwe ukoo mmoja au familia moja!!
Muhimu ni maadili na makubaliano yenye misingi ya kujituma vilvyo!! Kujenga umoja NI Jambo na kushirikiana NI Jambo lingine!!
KM;- wahindi wanaAmini biashara ikianza Leo basi unapaswa usile mtaji huo Wala kutumia mtaji huo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo!! (Usitamani mmea unapochipua ukala majani yake)!!
Kea Waarabu nao huaanza biashara kwa kianzio kwa Swadaqa ya LiLLah na hutughushi au kudhulumu upande wowote..ili isije chafua Rasilimali iliyowekezwa!! ( kutojionyesha au kujisifia Kati wa miliki)!! Happ pagumu Sana !!
 
Well said..umeona huku Majuu foundation za marehemu zinadumu zaidi ya miaka Mia nne na ushe!!(Matunda yake yanaifaa Hadi Africa;Asia;Nk nk..)
 
Partnership Ina historia kubwa...na si Lazima muwe ukoo mmoja au familia moja!!
Muhimu ni maadili na makubaliano yenye misingi ya kujituma vilvyo!! Kujenga umoja NI Jambo na kushirikiana NI Jambo lingine!!
KM;- wahindi wanaAmini biashara ikianza Leo basi unapaswa usile mtaji huo Wala kutumia mtaji huo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo!! (Usitamani mmea unapochipua ukala majani yake)!!
Kea Waarabu nao huaanza biashara kwa kianzio kwa Swadaqa ya LiLLah na hutughushi au kudhulumu upande wowote..ili isije chafua Rasilimali iliyowekezwa!! ( kutojionyesha au kujisifia Kati wa miliki)!! Happ pagumu Sana !!
Asante sana mkuu, katika siri nzito nilizowahi kuzisoma jf zenye impact katika maisha yangu hii ni mojawapo. Umeandika maneno machache yenye thamani ya vitabu 1000. Nimesoma vitabu vingi lakini sijawahi kukutana na hizi siri.

Nimejikuta navutiwa kuelewa zaidi hiyo ya wahindi na warabu.. hapa kwa mwarabu na connect na kuelewa maana ya ule msemo wa ..kuanza na mguu mbaya
 
Ndg mpendwa!! Karibu Sana... Tubadilishane rai,mawazo na tafkira!! Haya mataifa yanauzoefu wa kijamii kati ya mashariki na magharibi ya ulimwengu !! (Umma wa wastani) na no Rich culture na utamaduni mpana went wasaa wa kuvumilia...
 
Kiukweli family business ni kitu ambacho ni kigumu sana Kwa sisi waafrika kukifanya...kama sahiv tu, ndugu tunakaa mbali na hatushirikiani Kwa lolote lkn tunachukiana...tukiingia kwenye family business si tutauana na kushikana uchawi..
Kweli mkuu yaani hii rangi nyeusi sijui Ina laana gani.
Eti utashangaa watu wanashikiana mapanga kwa mali walizotafuta watu wengine(wazazi).
Au utakuta vijana hawafanyi kazi wala kutafuta pesa eti kwa vile wazaz Wana assets kwa hyo miaka yote wanazingojea tu hadi wazazi wadondoke.
 
Mkuu mbona wazungu wanafanikiwa na huwa hawaishi pamoja?
Wazungu wanaandalia mazingira watoto wao, mtaji utapewa, nyumba utapewa ukaishi huko...(wana uprivacy tu lakini sio wabinafsi)..... NB:Kwa mtazamo wangu wakimuvi muvi sijawahi ishi nao
 
Back
Top Bottom