Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Sijui wangapi mna ‘personal experiences’ za kushikiliwa na Polisi kwa kosa lolote lile.
Ni kweli Watanzania wengi ni wanyonge sana hasa wanapokuwa mbele ya dola. Hata wenye hela huwa ghafla wanageuka wanyonge hata haki zao zinapogandamizwa.
Kwa mazingira na mazoea ya Kitanzania, bado wengi wetu, si wenye nchi, si Polisi na hata si Mahakama wanaoelewa na kuheshimu dhana ya ‘innocent until proven guilty’.
Mfano, wengi hawaheshimu haki ya mtuhumiwa ya kwamba hata ukishakuwa katika mikono yao, una haki ya kutozungumza chochote mpaka wakili wako awepo.
Familia inachotaka ni kuona uko huru. Wakifika kituo cha polisi, wataanza kuwapa polisi hela za chai, watazungumza kinyongenyonge, wakati huo huo maafande wanazidi kukaza kwa kauli zao. Na hapo ukute kesi yako inahusisha wasiojulikana, kesi yako kimsingi haiko polisi.
Masaa 24 yanapita, 48, 72, unakuja kugundua wiki 2, mtu wenu hajafikishwa mahakamani wala hajaachiwa. Wakili wenu yupo yupo tu na ndiyo kwanza familia inamwambia atulie, yatakwisha tu haya, hawataki kushindana na dola.
Mara nyingi familia zetu ndiyo zinalea tabia hii ya kushikilia watu hovyo hovyo bila kufuata sheria.
Myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, ni rahisi kusema lakini siyo kutenda.