Familia yenye Nguvu Tanzania

Mzee wa Torano

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
518
1,000
napenda kujua kama Tanzania pia kuna Familia Zenye Nguvu kama Hizo hapo chini na Nyinginezo
..Nguvu katika Uchumi/biashara
..Nguvu katika Utawala/siasa
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,698
2,000
Tanzania kuna watu wenye nguvu individual na si familia kama usikiavyo influence ya Kennedy family na Rockefeller family kwa marekani.

kikwete ni rais ila ndani ya familia yake kuna malofa na mafukara wa kutosha.
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,158
2,000
Rupia,Sykes,Karume,Kawawa, Dewji,Manji,Mengi,Kingunge
Kuna baadhi ya familia zimekuwa na uwezo tangia ukoloni, zikaweza kusimama kipindi cha Mwalimu na zinaendelea kusimama hata katika regime zingine zilizofuatia za kifisadi na ujanja ujanja.
Katika kuangalia hili suala inabidi kuwa makini usije kuunganisha familia ambazo zimeibuka miaka ya 90s kwa madili kama ya EPA nk, ambazo hazina hata rekodi za kulipa kodi, uhakika wa biashara wanazozifanya (mfano kuuza madawa na ndovu) na uhalifu mwingine kisa tu kwa vile wana pesa na madaraka!

 

chumvichumvi

JF-Expert Member
May 6, 2010
1,200
1,500
mtoa hoja uneongeza maelekezo kidogo ili uchangiaji uwe wa moja kwa moja maana hapa najiuliza nguvu katika uchumi kwa maana ya kushikilia uchumi wa nchi au kwa kuwa na pesa nyingi au kwa matumizi ya kifahari na hizo fedha ziwe halali au haramu .....
 

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,521
1,225
Kwa Tanzania hakuna familia yenye nguvu kama swali linavyotaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom