Familia ya watu wanne yauawa kwa moto wa petroli wakiwa wamelala ndani

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Familia nzima ya watu wanne wamepoteza maisha baada ya mtu au kikundi cha watu wasiofahamika kuwafanyia unyama na ukatili kwa kumwagia Petroli nyumba yao wakiwa wamelala majira ya usiku katika eneo la Kiwalani jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu hao.

Huu ni ukatili uliopitiliza. Hivi mtu anapata faida gani kuondoa roho ya mtu, tena aliyelala? Yaani ina maana.dhamira inakuwa imekufa kiasi hicho?.ni jambo gani kubwa hivyo la kumfanya mtu ateketeze familia nzima? Bado ninashangaa.
 
Dah mi mwenyewe nashangaa, frustrations za ugumu wa maisha ujinga nafikiri zinachangia sana kwenye haya natukio
 
Binadamu tumepoteza kabisa 'ubinadamu" tumekuwa na roho ambayo hakuna kiumbe Mungu alimuumbia roho ya aina hiyo, mpaka shetani anatuogopa maana tunaweza kwenda kwake na kuteka himaya yake nae akawa mtuhumiwa. Poleni wafiwa.
 
Hilo tukio linahuzunisha sana,nilikuwa nasikiliza mazungumzo ndani ya daladala la kutoka kijiwe samli siku ya mazishi ya waliotangulia kuzikwa wiki iliyopita watu walikuwa wanadai kijana aliyeachwa na binti(mmoja kati ya marehemu) ndio kafanya unyama huo.
 
Mimi ninaona Ni ukosefu wa malezi, Na Nchi hii kila viongozi wetu wa Serikali wanapotamka kuwa Serikali haina DINI kwa uchunguzi wangu majanga Na laana zinaongezeka.
 
aisee tunaelekea wapi sasa yaani binadamu wamekuwa kama wanyama unauwa mtu kisa nini hata ukiua itakusaidia inini
jamani kilichobaki tumwombe Mungu aikomboe taifa letu hamna kingine shetani amemua kuweka roho hii ya mauaji ndani ya taifa letu
 
Hilo tukio linahuzunisha sana,nilikuwa nasikiliza mazungumzo ndani ya daladala la kutoka kijiwe samli siku ya mazishi ya waliotangulia kuzikwa wiki iliyopita watu walikuwa wanadai kijana aliyeachwa na binti(mmoja kati ya marehemu) ndio kafanya unyama huo.
basi haya ni maamuzi magumu kuwahi kutokea, kaachwa kaamua akate mzizi wa fitna nyumba nzima.
 
Back
Top Bottom