Familia ya Nyerere yatabiri CHADEMA kushinda 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Familia ya Nyerere yatabiri CHADEMA kushinda 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Feb 27, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  • Mama Maria aongoza sala

  na Sitta Tumma na Janeth Josiah, Musoma

  FAMILIA ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, imekitabiria Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa kishindo wa kuongoza nchi mwaka 2015.

  Familia hiyo ya mwasisi wa taifa imesema ukomo wa serikali ya CCM umefika ambapo inaamini Uchaguzi Mkuu wa urais ujao, CHADEMA itaibuka kidedea.

  Kauli hiyo ya familia ya Mwalimu Nyerere, ilitolewa jana na mtoto wa tatu wa Baba wa Taifa, Magige Nyerere, akiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati viongozi wa CHADEMA Taifa walipozuru nyumbani kwa mwasisi huyo Butiama, Musoma, mkoani Mara, ambapo waliweka mashada katika kaburi hilo na Mama Maria kuongoza sala.

  Alisema anaamini wapigakura mwaka 2015 watakuwa milioni 12 na kati ya hao, CHADEMA itapata kura milioni sita na CCM itaambulia kura milioni nne.

  Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo wa Baba wa Taifa kwa sasa nchi iko katika joto kubwa la kisiasa.

  "Lazima tuseme ule ukweli uchaguzi mkuu uliopita CHADEMA haikuweza kuongoza dola, lakini mwaka 2015 wapigakura watakuwa milioni 12 na milioni sita zitaenda CHADEMA na milioni nne CCM.

  "Hali ilivyo sasa, joto la kisiasa hapa nchini liko juu na wananchi wameonekana kufanya mageuzi ya kiuongozi," alisema Magige Nyerere mbele ya mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere.

  Huku akimfananisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mdogo wake, Makongoro Nyerere, ambaye naye alikuwapo alisema, "Nakiri kuwa mimi ni CCM, lakini nafurahia kazi na siasa yenu…naomba uendelee hivyo na hata ukiwa bungeni kama kiongozi wa upinzani."

  Viongozi hao wa CHADEMA na msafara wao walizuru nyumbani kwa Nyerere majira ya saa 5:55 asubuhi kwa lengo la kumsalimia mjane wa Baba wa Taifa.

  Kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alimuomba Mama Maria kukiunga mkono chama hicho na kukiombea mema.

  "Mama tumekuja kukusalimia na familia yako…CHADEMA tunaomba mtuombee na mtuunge mkono," alisema Mbowe kisha Mama Maria kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelezo hayo.

  Akitoa nasaha zake mbele ya kaburi la Nyerere, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema mchakato wa Nyerere kuwa Mtakatifu mwenye kheri bado haujakamilika, hivyo raia wawe na uvumilivu.

  Alisema nchi ya Uganda imepiga hatua juu ya mchakato huo, hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.

  Kuhusu maandamano ya CHADEMA nchi nzima, Magige Nyerere alisema," Awali nilipatwa na wasiwasi mkubwa, lakini nimebaini kumbe ni maandamano mazuri; yaendelee."

  Hata hivyo, mtoto huyo wa Baba wa Taifa alisema maandamano hayo ni vema yakaendelea kwa amani, ili kufikisha ujumbe husika katika mamlaka husika.

  Wakiwa wilayani Tarime jana Mbowe alimtaka Rais Kikwete kuacha mara moja kuwajaza hofu Watanzania juu ya kuwepo mipasuko ya kidini. Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa kabla ya mkutano, alihoji sababu ya Rais Kikwete kushindwa kuwakamata na kuwasweka ndani wanaoleta chokochoko za kidini.

  Viongozi hao wa CHADEMA kesho wataendelea na ziara yao katika mkoa wa Shinyanga kwa kufanya maandamano makubwa ya kuwashukuru wananchi kwa kuwapa kura na kuwataka wananchi wapinge hatua ya serikali ya kutaka kuilipa kampuni ya Dowans.

  Source: Tanzania Daima litakalotoka kesho tarehe 28/02/2011
   
 2. P

  Percival JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,568
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ndiyo demokrasia hiyo - hakuna cha ajabu. hata mie nadhani itakua hivyo.
   
 3. MIAMIA.

  MIAMIA. JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa asilimia MIAMIA mimi ni mwanachama na masalia wa CCM,kiroho safi na thabiti kabisa lakini siasa ya CHADEMA naipenda na mwenendo wa CDM ni vema na wakiweredi saaaana,aksante kwa changamoto ya CDM!! nipo nanyi kwa nafsi,akili na mwili.
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  teh! Dsm its enoghf kaka, watasema chama cha wasukuma tena!
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Huo ni ukweli mtupu kabisa hata Mh.Regia(MB) ameshatujuza mida:
  Leo tulitembelea Kaburi la Hayati Baba wa taifa na kufanikiwa kukutana na Mama Maria pamoja na watoto wake wawili,Magige na Makongoro. Walitupokea vizuri sana.Pamoja na mambo yote yaliyofanyika kuna jambo moja tu nililolipenda zaidi.Maneno mazuri ya Magige kwa chama cha CHADEMA kuhusu maandamano. Amesema hivi ukiwa huna taarifa utapinga sana wanachokifanya CHADEMA kama ambavyo yeye alikuwa akipinga mwanzoni hasa Wabunge wa CHADEMA walivyotoka nje ya Bunge kutomsikiliza Rais Kikwete lakini baadaye amejifunza kwamba CHADEMA wanafanya kitu chema na akatoa mfano wa maandamano yanayoendelea sasa kuwa yanaumuhimu mkubwa sana hivyo akatoa rai kuwa kila mwenye kuipenda nchi hii basi lazima aunge mkono harakati hizi za CHADEMA.Amekiri kuwa yeye ni CCM damu lakini anaunga mkono harakati hizi za CHADEMA.

  Vile Vile ameitakia CHADEMA ushindi wa Urais mwaka 2015 kwa kutaka wajitokeza wapiga kura Milioni Kumi na Mbili halafu CHADEMA ipate Kura Milioni Sita na CCM Milioni Nne.

  Nawasilisha
  Kutoka Kitangiri Mwanza

  Reagia E Mtema
  Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
   
 6. T

  Teh Teh Teh Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anguko la ccm inakuja.
   
 7. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwa taarifa zangu za kiintelgensia kama viongozi wakuu wa CHADEMA hawatabadili mienendo na fikra zao mapema CHADEMA hawataweza kuchukua nchi kwa namna yoyote na ikishindikana watu wengine wanasema ni bora tufanye kama tunisia , misri nk lakini hapa itakua vita ya wenyewe kwa wenyewe. Ninachosali ni baadhi ya viongozi wakuu wa chama kubadili mienendo na njama zao za siri na kuweka lengo moja tu mbele maslahi ya umma wa Tanzania.
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Inatia moyo sana kazi yenu si bure kupata watu wanaowaunga mkono baada ya kufanya utafiti ijakuwa mwanzo walikuwa na mtazamo hasi this is great man keep up moving dont löok back.

  Jana nilikuwa mahali na muheshiwa mmoja wa ccm aliongea mamaneno mazito zaidi ya kukiunga mkono CDM Anasema kunawatu wengi ndani ya CCM wanaunga mkono arakati za CDM Kwa siri sana wakiangalia upepo wa mageuzi unavyokwenda na ikiwa Uongazi wa juu hatafanya reform huenda wakaamua kujitoa na kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CDM.

  Na hili limedhìrika juzi wakati mwenyeki wa UWT kuelezea hisia zake kuwa anavutiwa na Harakati za CDM.

  My take: Nawashauri CDM Wasilewe na sifa wanazozipata au kuona watu wengi wanawaunga mkono kwani historia inaonyesha kwamba watu hawatabiriki anaweza kukuunga mkono leo kesho akakubadilikia utadhani siyo yule wa jana aliyekuwa anakupiga makofi so CDM ni vema mkapanga mikakati ya kupata wanachama wengi zaidi na kuwa na takwimu hususa na pili kuweka nguvu maeneo yaliyo huenda impact yake isiwe kubwa lakine the next few years watapata huemda wakabadilika
   
 9. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  .....vivaaaaaaaaa!
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  katiba inaruhusu uhuru wa kujieleza. Mtoto wa Nyerere ni mmoja wa mwenye haki hiyo.
   
 11. D

  Do santos JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Shk yahya au kajura?
   
 12. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inshaahla kwa kauli za familia ya hayati mwl nyerere! Mungu ibariki CDM,Mungu ibariki Tanzania!
   
 13. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo mnataka kumwambia EL aache preliminary campaigns au nini?
   
 14. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kusema kweli,hakuna kitu cha ajabu.lakini kauli hiyo inaiongezea credit CHADEMA na kufanya chama kiaminike zaidi kwa wananchi.
   
 15. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Asante kwa comment yako,kikweli CHADEMA ndio chama mbadala,saidia kuwaambia ukweli wanachama wenzio wa kijani,hii nchi ni yetu sote,vyama vinapita lakini nchi itasimama daima
   
 16. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  tuko pamoja mkuu,achana na chama cha kijani.jiunge na chama cha mabadiliko CHADEMA
   
 17. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  very soon
   
Loading...