junior2008
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 528
- 42
habari zilizoripotiwa na gazeti la habari leo ni kuwa mmoja wa wanafamilia ya Nyerere ametoa tamko la kuikana chadema na kusema kwamba chama hicho kisitumie jina na kaburi la hayati Nyerere kujipatia umaharufu wa kisiasa! pia amesisitiza kwamba wao kama familia hawaungi mkono maandamano ya chadema na hawana uhusino wowote na chadema.
TAHARIFA RASMI NI HII;
WAKATI Watanzania wakizidi kujitokeza kulaani maandamano ya kichochezi ya Chadema, familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imeelezea kushangazwa na uongo wa viongozi wa chama hicho, kwamba familia hiyo inakiunga mkono.
Mbali na kuelezea kilichotokea wakati viongozi wa chama hicho walipotembelea familia hiyo hivi karibuni, pia imekemea mbinu za kutumia kaburi la Baba wa Taifa kujipatia umaarufu.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia hiyo, tofauti na ilivyotangazwa na vyombo vya habari vinavyoshabikia maandamano hayo, familia hiyo haikuunga mkono maandamano hayo na badala yake ilisisitiza umuhimu wa kuzingatia utaratibu wa Serikali na kudumisha utulivu.
Akitoa taarifa hiyo jana, mmoja wa wanafamilia hiyo, Makongoro Nyerere, aliweka bayana kwamba familia hiyo haijaunga mkono Chadema kwa mambo inayoendelea nayo sasa, ikiwamo maandamano yaliyoendeshwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba chama hicho kimepata baraka na kuombewa dua yenye lengo la kuungwa mkono na mjane wa Mwalimu Nyerere, Mama Maria na familia yake kwa lengo la kukitabiria ushindi.
Makongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM ya Mkoa kilichoshirikisha wajumbe na wabunge wa CCM wa mkoa huo, alisema kilichofanyika Butiama ni utaratibu wa kawaida wa kupokea wageni wanaotembelea kaburi la Mwalimu.
Source: Habari leo. Hilo ni gazeti la mafisadi kazi yao ni kuandika pumba tu. Tulishaona kwenye TV (ITV) na vyombo mbalimbali vya habari siku CHADEMA walipoenda kutembelea kaburi la hayati baba wa taifa, JK Nyerere, mpaka mmoja wa watoto wa Nyerere akatabiri kuwa 2015 CHADEMA watashinda uchaguzi, sasa hizo habari za habari leo ni udaku mtupu na hazina mashiko! Kutembela kaburi la baba wa Taifa ni heshima tu CHADEMA hawakufanya hivyo kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa kwasababu wao sio wa kwanza kufanya hivyo!!