Familia ya Nelson Mandela yapongezwa kwa kusema hadharani binti yao alikufa kwa COVID-19

Pinkman

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
707
1,538
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amepongeza familia ya Rais wa kwanza wa nchi hiyo Nelson Mandela kwa kusema wazi kwamba binti yao, Zindzi, alikufa kwasababu ya ugonjwa wa virusi vya corona, Jumatatu.

Hilo litafanya jamii kutonyanyapaa wanafamilia waliopata maambukizi, Bwana Ramaphosa amesema.

Zindzi alizikwa Ijumaa asubuhi kando ya kaburi la mama yake ambaye pia alikuwa mwanaharakati aliyepinga ubaguzi wa rangi Winnie Madikizela-Mandela

Afrika Kusini ni moja ya nchi za Afrika iliyopata maambukizi ya juu ya ugonjwa wa virusi vya corona ikiwa na zaidi ya maambukizi 320,000

Kumekuwa na zaidi ya vifo 4,600 na serikali imekadiria kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi 50,000 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Licha ya kwamba raia wamefahamishwa kuhusu vile virusi vya corona vinavyosambaa, dalili na athari zake bado kumekuwa na taarifa za unyanyapaa dhidi ya waliopata maambukizi.

Rais Ramaphosa amesema nini?

"Ningependa kushukuru familia ya Mandela kwa mfano mzuri wa kushirikisha taarifa hizi na taifa. Hivi ni virusi ambavyo vinaathiri kila mmoja, na hakustahili kuwa na unyanyapaa wowote miongoni mwa waliopata maambukizi," alituma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter kabla ya mazishi ya Zindzi Mandela.

Aliongeza kwamba kusema wazi sababu ya kifo chake, ni ishara ya mshikkamano wa juu zaidi kwa mwanamke aliyejitolea maisha yake kwa raia wenzake wa Afrika Kusini."
 
Kwa hio kwa Tz wahaya pia ni mawakala wa mabeberu sio?Maama ukimwi ulianzia kwao hapa bongo.
sio hivyo kiongozi kuna baadhi ya mambo yanavyokwenda mtu unakuwa unajiuliza maswali
mf sa walitangaza vifo nadhani kama elfu 50 cha ajabu ramaphosa akasema kweli idadi imekua kama WHO ilivyotabiri
janga limetokea ni kama wao hawana maamuzi nalo jinsi ya kudhibiti wanafuata maagizo kutoka kwa wazungu
 
SA kwa africa nahisi ni mawakala wa mabeberu kwa mambo fulani fulani
yaani kila kitu kinachoanzia kwa mabeberu wao lazima wakipokee kwa utimilifu mf ukimwi wanaongoza wao covid nayo wao WTF
Ukimwi si unaongoza kwa mswati kwa sasa
 
Back
Top Bottom