Familia ya mzee Zahir Zorro 'ilivyomuokoa' Nzela

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Kuna mambo mengi sana siku hizi yanakosekana kwenye tasnia ya burudani Tanzania. Naamini mambo yamekuwa feki sana kiasi kwamba kuna utamu na uchungu wa kisanaa tunaukosa. Au nimezeeka?

Miongoni mwa mambo tuliyofaidi miaka 10 kurudi nyuma kwenye tasnia hii pendwa ya vijana ni wasanii kutugusa moja kwa moja kwa sababu kuna wakati walilazimika kutumia mikasa ya maisha yao binafsi (lived experience) ili ku-vent na jamii ikaponea humo humo. Sijui kama naeleweka.

Hili lilitokea kwa NZELA. Ukiendelea kusoma utanielewa.

Sote tunaukumbuka wimbo wa Nzela wa B-Band siyo? Afro sound fulani hivi classic ambayo mpaka leo ikipigwa inakupa feeling nzuri kabisa.

Sasa kubwa zaidi kwenye hicho kibao ni ujumbe ambao watu wengi waliuchukulia kawaida enzi zile, pengine hadi sasa, lakini kwa kuunganisha mtiririko wa matukio ni rahisi kuunganisha nukta na kugundua haukuwa wimbo tu kama wimbo mwingine wa kawaida bali kilio cha familia kwa binti yao mpendwa.

Nzela, kwa mujibu wa mashairi yaliyomo, alikuwa ni binti pekee wa familia ambaye alitoroka nyumbani baada ya kubeba ujauzito akiwa mwanafunzi na hakuna mwanafamilia aliyejua katorokea wapi. Ni kama familia ilishaamua kumsamehe na kumtaka arudi nyumbani kuungana nao. Mama, Baba, Kaka, Mjomba na jirani wote walimtumia ujumbe kupitia wimbo huo.

Pamoja na sanaa kubwa iliyotumika kwenye uandishi na kutwist baadhi ya mashairi, lakini kwa asilimia kubwa yaliyoimbwa yanamsadifu aliyekuwa binti wa familia ya Mzee Zahiri Ally Zorro, tuliyemfahamu kwa jina la Maunda Zorro.

Ni kama wimbo wa Nzela ulifanikiwa kwani binti alijirudi na kupewa sapoti kubwa na familia hadi kubadili mwenendo wake, akaishi maisha mapya yenye heshima na adabu, akapata umaarufu na kupokelewa vizuri na Watanzania hivyo kutengeneza maisha kupitia kipaji chake na kipaji cha familia ambacho ni muziki. Yaliyobaki ni historia.

Kwa bahati nzuri au mbaya sana tumempoteza Nzela kwa ajali ya gari hivi karibuni, lakini kinachotia faraja ni kwamba alibadili tabia na akauamaliza mwendo akiwa ni mmoja wa wasanii wanaoheshimika na kupendwa sana nchini na nje ya mipaka ya nchi.

Naamini wimbo huu utabaki katika kumbukumbu za kudumu za familia ya Mzee Zorro wakati huu ambao wanaendelea kumuomboleza na kumuenzi binti yao mpendwa na kipenzi cha Watanzania, NZELA.

IMG-20220511-WA0037.jpg
 
Dah...ni Sanaa Kubwa, akili Kubwa..! Kizazi hicho Katika Kutengeneza Wimbo msanii anaanza na Kuyajenga Maudhui halafu anaweka beat.

Vijana Wa sasa anaanza Kuomba Beat kutoka Kwa Producer halafu ndo apachike Maudhui.
Hiyo imepelekea nyimbo Za Hovyo sana kutolewa na Kizazi hiki..!

Mtu anaimba 'Nataka Kulewa' hlf anarudia rudia Hayo maneno Wimbo tayari..!
 
Dah...ni Sanaa Kubwa, akili Kubwa..! Kizazi hicho Katika Kutengeneza Wimbo msanii anaanza na Kuyajenga Maudhui halafu anaweka beat.

Vijana Wa sasa anaanza Kuomba Beat kutoka Kwa Producer halafu ndo apachike Maudhui.
Hiyo imepelekea nyimbo Za Hovyo sana kutolewa na Kizazi hiki..!

Mtu anaimba 'Nataka Kulewa' hlf anarudia rudia Hayo maneno Wimbo tayari..!
Huyo Domo na harmonaizi ndo zao pia hata alikiba kaishiwa
 
So ndo alimpa Gonjwa zito la ukimwi ? Km nyimbo inavyosema

"Dunia ni tambala lililotoboka kumbuka Kuna Gonjwa zito la ukimwi"

Mkuu umesoma hadi darasa la ngapi!? Kile kipengele cha ufaham swali la kwanza kwenye mitihani kuanzia darasa la 5 unalifaham!? Form one ukifika wanaita comprehension. Hua swali la kwanza la mtihani wa kiingereza.
 
Back
Top Bottom