Familia ya mzee kingunge yaumbuliwa na halmashauri ya jiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Familia ya mzee kingunge yaumbuliwa na halmashauri ya jiji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 25, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  Ni ukusanyaji mapato kituo kikuu Ubungo
  Latangaza kukusanya milioni 4/- kwa siku
  Familia ya Kingunge ilidai kupata mil. 1.5/-


  Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru.
  Makusanyo ya mapato katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT), yameongezeka maradufu, ikiwa ni wiki chache tangu mkataba wa kampuni binafsi inayomilikiwa na familia ya Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru, kumalizika na kazi hiyo kukabidhiwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilianza rasmi kukusanya mapato kituoni hapo Novemba Mosi, mwaka huu baada ya kampuni hiyo ya familia ya Kingunge ya Smart Holdings, iliyokuwa imepewa zabuni hiyo kwa zaidi ya miaka mitano kumaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi uliopita.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi, alisema jana kuwa tangu Halmashauri ianze kazi hiyo, imekuwa ikikusanya mapato ya wastani wa Shilingi milioni nne kwa siku.

  Kingobi aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa taarifa katika kikao cha Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam.

  Kwa hesabu hiyo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa mwezi itakuwa ikikusanya Sh. milioni 120.

  Awali, kampuni ya Smart Holdings ililalamikiwa kuwa ilikuwa ikikusanya mapato makubwa katika kituo hicho, lakini ikiishia kuilipa serikali fedha kidogo Sh. milioni 1.5 tu kwa siku.

  Katika makusanyo hayo, kampuni hiyo ilikuwa ikiilipa serikali sh. milioni 46.5 kwa mwezi.

  Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimuagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kufanya ukaguzi wa hesabu za mapato katika kituo hicho na katika Shirika la Masoko ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam na kisha kuwasilisha ripoti ofisini kwake.

  Pinda alitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao cha majumuisho, baada ya ziara yake ya siku tatu, jijini Dar es Salaam, Machi 15, mwaka huu.

  Katika agizo lake, Pinda alisema bila kujali mmiliki halali wa kampuni hiyo, ukaguzi wa hesabu hizo unapaswa kufanyika kwa maslahi ya umma, kabla ya kuchukua hatua kwa mujibu wa mapendekezo yatakayotolewa na CAG.

  Katika ziara hiyo, Pinda alishangazwa na kushtushwa na utendaji mbovu wa uongozi wa UBT, mkataba uliofikiwa kati ya kituo hicho na kampuni hiyo na namna ilivyopatikana.

  Pinda alifikia hali hiyo, baada ya kupewa taarifa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Kingobi, kuhusu hali ya utendaji wa uongozi wa UBT, ukusanyaji wa mapato, mkataba wa mkandarasi na maendeleo ya kituo hicho.

  Katika taarifa yake, Meneja wa Kituo hicho, Fadhili Izumbe, alisema kwa mujibu wa mkataba, mkandarasi huyo huipa Halmashauri ya Jiji, Sh. milioni 1.5 kwa siku, taarifa iliyomshangaza Pinda na kumfanya ahoji: “Hata kama anakusanya Shilingi bilioni moja anatoa Sh. milioni 1.5? Na kwa nini mkataba utamke shilingi badala ya asilimia?”.

  Kwa siku mabasi zaidi 400 husafirisha abiria, teksi 100 na watu zaidi ya 2,000 huingia UBT.

  Pia, kuna maduka ya vinywaji (baa na grosari), maduka ya kawaida, hoteli, ‘vioski’, gereji, ambavyo vyote hulipa ada za viwango mbalimbali.

  Siku moja baada ya ziara hiyo ya Pinda, mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Smart Holdings, Hassan Khan, alisema viongozi wa Halmashauri ya Jiji waliokuwapo kwenye ziara hiyo, hawajui lo lote na ndio maana walishindwa kumueleza Waziri Mkuu ukweli kuhusu mkataba huo.

  Khan alisema katika mkataba huo, walikubaliana na Halmashauri ya Jiji kuwa wangekuwa wakiilipa asilimia 75 na kushangazwa kusema asilimia hiyo ni sawa na Sh. milioni 1.5.

  Alisema katika mkataba huo, pia walikubaliana wawe wanalipa kiasi hicho cha fedha kwa kila siku bila kujali hali ya mapato itakayokuwa na bila kujali pia kuwa siku za mwishoni mwa juma (wikiendi) na wakati madaraja yanapokatika, kampuni yao hupata hasara.

  Utouh alikabidhi ripoti ya UBT mjini Dodoma, Julai mwaka huu, wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge.

  Akijibu maswali ya papo kwa papo mwishoni mwa mwezi uliopita bungeni, Pinda alisema ripoti hiyo inapitiwa na Katibu Mkuu wa Tamisemi na yule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na kuahidi kuwa itatolewa hadharani baada ya maofisa hao wa serikali kumaliza kazi ya kuipitia.

  Hata hivyo, kabla Pinda hajatoa kauli hiyo, wiki kadhaa zilizopita, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alidokeza kuwa serikali ingechukua kituo cha Ubungo kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwisho wa mwezi uliopita.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kazi kweli kweli
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  Kasheshe!!!!
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  ipo kazi yetu macho
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we switibebi achana na mambo ya huku bana ,mi nimeachika ni PM tuanze mchakato
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmhhhh naogopa "kigogo""
  afadhali magomeni,posta,manzese ningeku pm....badilisha jina tuanze kazi...
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  ?????????? kazi unayo... micharuko tu.
   
 8. A

  Ashavin Member

  #8
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ina maana hili walikuwa hwalijui?
   
 9. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi yule mzee Kingunge akingaka wanapoguswa mafisadi hamkujua? Wazungu wanasema: Tell me your friend I will tell who are. Nionyeshe rafiki yako nami nitajua wewe ni mtu wa namna gani. Hakuna fisadi asiyekuwa muongo. Hivyo rafiki wa fisadi lazima naye awe muongo.
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  alafu tukiwaita wezi wanasema tuna wakash'fu au tuna toa maneno ya uchochezi.
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona wameipa kampuni ya kingunge kazi ya kukusanya tena ushuru ktk jengo la machinga complex? Au wanasubiri tena mpaka pinda ahoji?
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nakwambia hawa CCM sijui wana nini, kingunge huyu huyu kapewa tena kazi ya kukusanya ushuru ktk machinga complex.....hivi hawajui madudu yake??
   
 13. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tanzania kichwa cha mwendawazimu...Alhaj Ali Hassan Mwinyi
   
 14. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  walikua wanaiba pesa haiwezekani wao wapate m 1.5 kwa siku wakati wenzao wanapat 4m, wizi mtupu akina kingunge
   
 15. Mwamanda

  Mwamanda Senior Member

  #15
  Nov 25, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  nasikia kizunguzungu
   
 16. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Wadau... ni habari nzuri lakini tusiende "personal" maana ni kampuni ndiyo iliyopewa dhamana..sasa kama ni ya Mzee KNM na familia yake au vinginevyo

  Ninaamini ni kampuni ndiyo iliyopata Tenda ya kukusanya mapato.... Na kama Jiji wangekuwa makini kama wanavoonyesha wameanza basi pengine mkata wenyewe ungeandaliwa kwa makini zaidi baada ya wao JIJI kufanya utafiti/ufuatiliaji wa mapato tarajiwa..... Naona Ule ujanja wa kununua daladala halafu mwenyewe ukaizungusha kwa wiki kujua mapato na njia kisha kumpa malengo dereva JIJI hawakuutumia..kwa hio wasitambe sasa...! sana sana wafiche nyuso zao. Ni katika ukumbi huu ndipo palipotolewa hoja ya ufisadi UBT.
   
 17. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi nafikiri huu ni mwanzo mzuri, Ningependekeza Muheshimiwa PM au CAG wakague mapato yanayokusanywa na Familia ya Kingunge kutokana na PARKING ZA DAR ES SALAAM CITY CENTRE (maeneo yote ya Karioakoo na Posta) kupitia kampuni ya NPS inayomilikiwa na mke wa kikongwe huyo.
  Kwa utafiti wangu mdogo,niliofanya mwaka 2008, just mtaa mdogo pale maeneo ya HINDIRA GANDHI wenye parking slot 10 au 15 tu (opposit to Dr K.K Khan Hospital), kwa siku wanakusanya si chini ya Tsh 120,000.
  Swali je katika system yao yote kuna parking slot ngapi zinazolipiwa jijini DSM, je wanakusanya sh ngapi kwa siku, na wanalipa Tsh ngapi serikalini kwa siku au kwa mwezi?
  Je kuna lazima yoyote ya kubinafsisha hii huduma kwa MAFISADI kama hawa?
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Wakulaumiwa ni viongozi wa CCM kwani ndani ya CCM kuna Mafisadi wengi na wengi wao ni Vigogo hatuwezi kuwataja hapa JF wanajijuwa hao wenyewe kinachotakiwa wakati wa uchaguzi ujao CCM iondoke kije chama kipya kitakacho weka usawa wa haki kwa watu wote inshallah Mungu ibariki Tanzania na uwabariki wananchi wa Tanzania Ameen
   
 19. Deny

  Deny Member

  #19
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 56
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  mmmmmhhhh!!!!

  Hivi jamani kwa nini tusione aibu kushindwa kuendelea hata miaka karibu 50 ya kujitawala bado tunazidi kurudi nyuma!!!!!
  Ingawa sikuwepo wakati ule lakini hii hali si inazidi enzi ya ukoloni kwa madhambi, wizi na dhuluma? Si afadhali wakati ule nchi ilikuwa ikienda mbele kimaendeleo?
  Uhuru gani sasa huu ambao hatujui haki zetu?? Tunaibiana wenyewe rasilimali na kodi zetu za maendeleo na kuwaona wanotuibia ni mashujaa!!!
  Tusipoondoa ujinga na kudanganyana tutaendelea kudharaulika duniani. Tutaendelea kunyanyaswa kwa ujinga wetu, tutaendelea kudanganywa kwa kuletewa kila kitu kutoka nje.
  Hao watoa misaada wenyewe wanapowaona hao wachache wanavyoishi kifahari kuliko hata wai waliotoa misaada hiyo wanatucheka na kutudharau!!!!
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  hakuna alieenda personal mkuu sasa embu tuambie ya nani???ndugu yangu
   
Loading...