Familia ya Mwinyi yazua Tafrani

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
FAMILIA ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi juzikati ilizua tafrani mtaani kufuatia mzozo mkubwa wa nyumba kati ya mjukuu wa Mzee Mwinyi, Abdi Hassan Mwinyi na anayedai ni mmiliki wa kurithi, Edward Francis Bogwe.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwananyamala-Komakoma, Dar ambapo mtoto wa rais mstaafu huyo aitwaye Abas Mwinyi aliongoza sekeseke mtaani.

Ishu ilikuwa hivi; miezi kadhaa iliyopita, Edward alimfikisha Mahakama ya Ardhi chini ya Jaji Kombolwa, Abdi akimtaka ahame kwenye nyumba hiyo ambayo ni mali ya familia, aliachiwa na marehemu baba yake, Francis Bogwe.

Baada ya kusikiliza utetezi wa pande zote mbili, mahakama ikaamuru Abdi ahame kwenye nyumba hiyo kwa vile ni mali ya Francis.
Francis akiongozana na madalali alikwenda kumtoa Abdi na vitu vyake, ikiwemo familia na kupiga kufuli milango muhimu ya kuingilia ndani na kuondoka nyumba ikiwa tupu.

Lakini siku mbili mbele, Abas akiwa na ndugu zake wengine pamoja na askari kibao, sambamba na huyo Abdi alifika akiwa na karatasi mkononi yenye maagizo kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ikidai kuwa, Abdi aendelee kuishi ndani ya nyumba hiyo hadi keshi ya msingi iliyofunguliwa na Abas ya kupinga kuhamishwa kwa Abdi itakaposikilizwa.
Kesi hiyo ilisikilizwa Desemba 2, mwaka huu kwenye mahakama hiyo jijini Dar.

Baada ya kufika kwenye geti la nyumba hiyo na kukuta watoto wa familia ya Bogwe, akiwemo dada wa Francis aitwaye Josephine Bogwe, Abas alisema: "Shida yetu fungueni mlango tuingie ndani hii ni nyumba yetu mambo mengine tutajuana mahakamani." (huku akionesha hati kutoka Mahakama ya Ardhi).

Baada ya kauli hiyo ndipo tafrani ilipoibuka ambapo Josephine alitoa makaratasi yanayoonesha kuwa, nyumba hiyo ni haki yao kama familia.

Josephine alimtaka Abas na ndugu zake waoneshe vielelezo vyao vinavyoonesha kuwa nyumba hiyo ni yao.
"Hapa hadi kieleweke mnataka kutudhulumu haki yetu, haiwezekani mahakama itupatie haki nyinyi mnakuja na maaskari kuamuru nyumba ifunguliwe ili muingie ndani," alisema Josephine.

Hata hivyo, katika kesi iliyofunguliwa na Abas kwenye Mahakama Ardhi, Jaji Mziray alisema Abdi si mmiliki halali wa nyumba hiyo kwa kuwa hana nyaraka zinazoonesha aliuziwa nyumba hiyo na marehemu Francis.

Kwa upande wa Edward, Jaji Mziray alisema kwamba hakutakiwa kumuhamisha Abdi mara ya kwanza bila kupata hati ya hukumu akatakiwa kushughulikia hati hiyo kwanza.

Source: GPL
 
si wahamie ktk vitalu maporini arusha na lodge zao?Au akaishi ktk lodge za Unique lodge?
 
Ukwasi wote ule bado wanataka kudhulum nyumba mwananyamala!?
 
Mambo mengine ni ya kujidhalilisha tu, hivi familia ya Mwinyi ina dhiki kiasi gani mpaka wang'ang'anie kuishi kwenye nyumba ambayo si yao? waache ujinga wao huo.
 
Kakke Tamaa na kupenda dhuluma tu

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Last edited by a moderator:
hiyo nyumba ya namna gani au ndio tamaa zao tu kudhulumu raia kupitia majina ya babu zao...
 
si wahamie ktk vitalu maporini arusha na lodge zao?Au akaishi ktk lodge za Unique lodge?
Hata mimi namfahamu shemeji yao mmoja tulilikua naye kijiweni alivyooa tu mtoto wa mzee ruksa enzi zile akapewa kitalu... Waende kwenye vitalu vyao sio kudhulumu watu.
 
Mambo mengine ni ya kujidhalilisha tu, hivi familia ya Mwinyi ina dhiki kiasi gani mpaka wang'ang'anie kuishi kwenye nyumba ambayo si yao? waache ujinga wao huo.

watoto wa kiswahili ktk circle zao wameshageuza sehmu ya kuonyesha heshima ya familia....ni tabia zao.
 
Na Buffalo Camp/Lodge pale Loliondo

karibu kabisa na waarabu waliowapa nchi........halafu hawa dogo na ndugu zao ktk imani wanaofany akazi kwa muarabu wapo very busy kuwateta waarabu sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom