Familia ya Mkenya aliyekwama Guantanamo yataka Rais Ruto aingilie kati

Mr Death

Senior Member
May 4, 2016
174
149
mohammed-abdul-malik-457x300.jpg



JAMAA za Mkenya mmoja anayezuiliwa katika gereza la Amerika la Guantanamo Bay nchini Cuba, imeomba serikali iwasaidie kumrejesha nyumbani mpendwa wao baada ya wakili Bw Miguna Miguna kurudi nchini.

Amerika haikumpata Bw Malik Mohammed Abdul na hatia na ikamwachilia huru mnamo Januari, lakini hajarejea nchini tangu wakati huo.

“Ni jana tu tumemuona Bw Miguna amerejea nchini baada ya kutimuliwa hapo awali, kudhalilishwa na kuteswa. Ombi langu ni Rais William Ruto kumrejesha ndugu yangu Bw Malik ambaye amekaa miaka mingi kule Guantanamo nchini Cuba,” alisema dadake Bw Abdul, Bi Mwajuma Rajab.

Bi Rajab alielezea masikitiko ambayo familia yao inapitia baada ya aliyekuwa wakili wa ndugu yao kujiuzulu.

“Kufikia sasa hatujaarifiwa wakili wake mpya ni nani. Ndugu yangu alipatikana hana hatia na ikasemekana anarudi nchini. Ni matumaini yetu kama familia ya Bw Abdul kuwa Serikali itamzingatia pia yeye na kumrudisha aungane na familia na jamaa zake,” alisema Bi Rajab.

Malik alishutumiwa na Amerika kwa kuendeleza uhusiano wa karibu na wanachama wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda katika Afrika Mashariki na kuwa na uhusiano na wanachama wakuu.

chanzo : Familia Ya Mkenya Aliyekwama Guantanamo Yataka Ruto Aingilie Kati - Zotekali Blog
 
Huyo ni gaidi tu, Marekani inapowaachia hao sio kwamba si magaidi, tayari wameshamalizana nao ni majoka ya kabisa tu hawana madhara Tena na wameshadunga sindano watakufa lini.
 
Back
Top Bottom