Familia ya Ed Warren na Makumbusho ya kutisha

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,563
2,045
Habarini za asubuhi wanaJF poleni kwa wagonjwa wote na wale wazma niendelee kuwa na afya njema. Baada ya kukaa kimya kirefu bila kuleta uzi wa kuongezeana maarifa basi leo Naomba nilete uzi huu ukiwa ni muendelezo wa uzi wangu uliopita.Uzi uliokuwa ukiwaelezea Bwana Na Bibi Warren.

Unaweza kuupata hapa Ijue familia ya Bwana & Bibi Warrens; Waanzilishi wa chama cha kufuatilia na kutatua mambo yanayohusu upande wa pili wa kiroho.

IMG_0946.jpg
Leo ninakwenda kuelezea namna familia hii ilivyotunza vikaragosi, wanasesere, pamoja na vitu vilivyokuwa vinahusika moja moja kwenye masuala mazima ya kiroho. Haswa zile roho chafu pamoja na mashetani ambayo yaliingia kwenye vitu hivi au kutumia vitu hivi kuleta athari kwa wanadamu na familia zao.

Mfano mzuri ni Mwanasesere wa Annabelle na taa ya Crooked Man.
Karibuni sana.

Wakati ambao Ed pamoja na Lorraine ambaye ni mke wake walipoanza kuzunguka katika familia mbalimbali ili kuleta suruhu ya matatizo yao; waliona ni vyema wakachukua vitu ambavyo vilionekana vina tabia tofauti na ilivyo Kawaida. Waliamua kufungua Makumbusho yao Mwaka 1952 na kuanza kuweka vitu hivi.

IMG_0944.jpg

Kwa mujibu wa Mwanahabari mmoja aliyekwenda kumuhoji Bwana Ed Warren kuhusu Makumbusho hiyo; mwanahabari Huyu alipewa masharti mengi kabla ya kuanza matembezi ndani ya Makumbusho hiyo. Moja kati ya masharti hayo ni kuwa; hakutakiwa kushika kitu chochote hata kabati Kwani kila kitu kilichomo ndani mle ni hatari. Sharti lingine ni kuwa hakushauriwa kukipa mkazo wa macho kitu chochote kwa muda mrefu; yaani Alitakiwa kuangalia kisha kuendelea na matembezi.

Makumbusho hii Ina jumla ya hifadhi ya vitu zaidi ya Mia moja. Mfano kifaa cha Muziki cha Perron pamoja kikaragosi cha Nyani.
Leo nakupa bidhaa tano tu bora na hatari zinazopatikana humo ndani.

IMG_0940.jpg

Makumbusho hii inapatikana mtaa wa 30 Knollwood Drive Monroe, Jimbo la Connecticut, Marekani Ingawa kwa sasa imefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na sababu mbalimbali. Ikiwemo ubalozi wa watu wengi wanaokwenda kuangalia Makumbusho hiyo.

IMG_0943.jpg

5. Vifaa na mawe katika Makaburi ya Watoto.

Mbali na kukusanya vifaa vilivyobeba roho chafu ndani ya Makumbusho yao; pia familia ya Warren walikusanya vifaa vilivyotumika kwenye matambiko ya Kishetani ambayo yalifanyika na baadaye familia hii ikafanya uchunguzi na mengine kuyazuia. Ikumbuke kuwa matambiko sio tu Afrika hata Ulaya wapo wanaofanya matambiko kwenye mapori.

Moja kati ya vifaa hivi ni mawe ya utambulisho katika makaburi ya Watoto wadogo kati ya miaka (1-10). Vifaa na mawe haya yalitumika kwenye matambiko machafu ya kishetani.

Ndani ya Makumbusho hii kuna hifadhi ya mawe na vifaa vilivyokutwa makaburini zaidi ya hamsini.

IMG_0936.jpg

4. Sio kila kitu kilichopo ndani ya Makumbusho hii basi kimepewa laana au kubeba mapepo au roho chafu. Baadhi ya vitu ndani ya Makumbusho hii vile vilivyopatikana kipindi au wakati wa uchunguzi na utafiti.

Ndani ya Makumbusho hii kuna mafuvu ya watu ambayo kuna mengine yalitumika kwenye matambiko ya kishetani. Aidha katika kufufua mtu, kuwasiliana na wafu, mapepo pamoja na kutengeneza laana.

Hii ni Moja kati ya vitu ambavyo familia ya Warren wanakataza watu kuvigusa Kabsa.

IMG_0937.jpg

3. Lulu za Kifo ni Moja kati ya bidhaa ambazo zimebeba laana na inasadikika kuwa endapo mtu atavaa mkufu huu basi mkufu utamnyonga mtu huyo shingoni mwake. Mmiliki wa mwisho wa Mkufu huu wa Lulu alianza kulalamika kuwa mkufu Ulikuwa unamkaba mara baada ya kuvaa tu Lulu hizi.

Mkufu huu wa Lulu zinazovutia sana zimehifadhiwa katika Makumbusho hii; huku zikiwa zimepigwa marufuku Kabsa kwa mtu kuzishika Kwani zinaweza kumpa tamaa ya kuvaa.

IMG_0938.jpg
Inadaiwa kuwa yule mwanahabari alivutiwa nazo sana kiasi kwamba ilikuwa ni kidogo tu afungue kabati ili achukue mkufu huu. Lakini Mwenyeji wake Bwana Ed Warren alimzuia.

2. Mwanasesere Kivuli ni kikaragosi anayetisha sana; achana na muonekano wa Annabelle au Chucky, Huyu ni zaidi ya hao Kwani Huyu hufanya majanga na maajabu wakati ya usingizi wa usiku.

Wakati ambao Annabelle husadikika kuwa huvamia watu na kuwakaba mpaka kifo; Huyu mwanasesere humuingia mtu katika ndoto na mtu huyo huanza kupata ndoto kama anakufa kumbe ndo anakufa kweli.

IMG_0941.jpg

1. Annabelle Halisi
Kama umepata kuangalia filamu mbili za Annabelle yaani Annabelle pamoja na Annabelle Coming Home; basi utakuwa unaelewa ninazungumzia mwanasesere Huyu.

Annabelle ni Moja kati ya Wanasesere hatari zaidi duniani; na kudhihirisha hilo familia ya Warren iliamua kumuweka kwenye Makumbusho lakini hii haikutosha wakamuweka ndani ya kikabati kitakatifu kikiwa na karata moja ya Taroti kama ulinzi.

Achana na yule Annabelle wa kwenye filamu Kwani huyo ameongezewa tabia nyingi. Lakini kitu cha kujiuliza ni kwanini mwanasesere huyu apewe ulinzi mkubwa namna hii?

Kiukweli na uhalisia Annabelle hakufanya mambo yale yote ndani ya filamu. Lakini familia ya Warren kuona ni vyema kuufungia mdoli huu ndani ya kabati na kuzuia mtu kuushika inaonesha ni kiasi gani wanaogopa kilichomo ndani.

IMG_0942.jpg

Mwisho:
Watu kadhaa walikuwa na Imani kuwa hii familia inaleta usanii tu na hakuna kitu cha ajabu kuhusu vitu hivyo. Wengine walijaribu kukugusa vitu hivyo na kukutana na mambo ya ajabu. Mfano kijana mmoja anayeitwa Scott aligusa na kukiangalia kikaragosi cha Nyani huku akiongea maneno ya dhihaka. Mwisho we alipata na mshtuko wa moyo ghafla. Lakini mpaka alipofariki Mwanamama Lorraine Mwaka 2019 hakuwahi kuruhusu mtu kufanya matembezi bila ya yeye kuwepo.

Naomba nimalize leo hapa Mungu akijalia nitaleta muendelezo wa kinachoendelea katika Makumbusho hii.

Shukrani sana

Cc. @Mshana_Jr
 
Attachments

  • IMG_0943.jpg
    IMG_0943.jpg
    112.7 KB · Views: 3
Kumbe Bongo uchawi bado sana mana kitambaa chekundu kilichobaki kutoka kwa mshona nguo na mifupa ya mbuzi inatosha kupiga pesa kutoka kwa wazembe
 
kuna movie inaitwa anabelle.... Ndo story yake hii! kumbe ni kweli
 
Ndio Mkuu yaani walichukua mkasa mzima na wakaufanyia Movie. Lakini walijaribu kuomba Annabelle Halisi lakini walipewa somo kuwa hiyo issue sio maigizo...... Annabelle hatakiwi kufunguliwa kwenye hicho kikabati na kila baada ya miezi mitatu huwa anakwenda Pastor kuombea.......
Karibu sana Mkuu
 
Kwangu inatisha tu kila nikiona vitu hvyo

Mkuu Chukulia picha umesahau kuzima camera yako usiku nayo ikawa inaendelea kuchukua matukio Chumbani kwako.... Ile unaamka asubuhi unakuta midoli inapiga misele tena kama mtu tu... utafanyaje mkuu!!???
 
Mkuu acha imagine hzo 😵😵😵😵
 
Back
Top Bottom