Familia ya Ben na Azory unganeni muombe msaada wa Interpol kujua hatma ya ndugu zenu

superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
6,317
2,000
Hivi hizi familia zina hali gani mpaka sasa, je matumbo yaliyowazaa watu hawa na maziwa yaliyowanyonyesha yanajisikia vibaya kwa kiwango gani?

Najaribu kuvaa viatu vya mama yake Ben na mke wa Azory.

Nishauri utawala huu ukiondoka madarakani ndugu wote waliopotelewa na ndugu zao wajiorodheshe majina waombe uchunguzi huru juu ya WHEREABOUTS ya ndugu zao.

Kupotelewa na mme au mtoto sio Jambo dogo hata kidogo. Ndugu zangu watanzania tunapoelekea uchaguzi tutafakari pia machungu waliyonayo wanafamilia na wanaukoo waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira ya kutatanisha halafu polisi wanachukulia POA.

Adimin naomba msiu merge Wala kuufuta Uzi huu.

Akhsante.

S...!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
2,227
2,000
Hapo utashangaa kuona serikali yetu inagoma kuruhusu uchunguzi toka nje wakidai hata wao wanaweza, halafu wakiachwa wafanye huo uchunguzi, wanarudi kulala usingizi, hawa watu sijui wakoje?!
 
mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,171
2,000
Hapo wa kuonewa huruma ni Ben Saanane, ila Azory Gwanda kuna dalili zote alikuwa anashirikiana na wale washenzi wa Kibiti ndio maana serikali ikaamua kumpoteza, huwezi kushirikia na magaidi wanaoua makumi ya watz na kuleta taharuki halafu serikali ikuchekee tu kwa kuwa ni wewe ni mwandishi wa habari.
 
superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
6,317
2,000
Wachaga wangekuwa na akili kama wahaya wangetakiwa wapige kelele kwenye kampeni za CCM wakitaja jina la Ben Saanane halkadhalika na huko atokako Azory jamani sio Jambo dogo hata kidogo mtu apotee halafu dunia ikae kimya.
 
superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
6,317
2,000
Hapo wa kuonewa huruma ni Ben Saanane, ila Azory Gwanda kuna dalili zote alikuwa anashirikiana na wale washenzi wa Kibiti ndio maana serikali ikaamua kumpoteza, huwezi kushirikia na magaidi wanaoua makumi ya watz na kuleta taharuki halafu serikali ikuchekee tu kwa kuwa ni wewe ni mwandishi wa habari.
Nadhani alitumwa na mwajiri wake mwananch media kuchunguza yanayoendelea kosa lake ni lipi?
 
mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
3,171
2,000
Nadhani alitumwa na mwajiri wake mwananch media kuchunguza yanayoendelea kosa lake ni lipi?

Kwa nini iwe yeye na sio mwandishi mwingine, tuache kutetea ujinga, serikali ilikuwa inalinda usalama wa taifa zima, kama Azory alikuwa mshiriki wa ugaidi au kikwazo hawawezi muonea huruma, maslahi na usalama wa taifa lazima uwe mbele.
 
Themagufulianz

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
3,985
2,000
Ujamaa ndio shida. Kusubiri serikali ikulishe.

Tuliojituma kulima tumeishi maisha matamu sana.

Viva Magu
Kweli kabisa, yule mnyampala wa barabara ambaye nu Mr. Kufoka ajiandae kurudi kwao kuvua samaki. Ametusababisha tuishi maisha mabaya.
 
share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
4,927
2,000
Awamu ya tano ndiyo umetia fora kwa uhuni huu wa kuuwa raia wake. Madhalimu wanapotawala nchi huugua. Yote haya mwisho ni tarehe 28 Oktoba 2020. Wakiiba kura watakiona cha moto kilichomfanya Mobutu na Iddi Amina Dada kufia ugenini.
 
mtingi1

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
743
1,000
Hapo wa kuonewa huruma ni Ben Saanane, ila Azory Gwanda kuna dalili zote alikuwa anashirikiana na wale washenzi wa Kibiti ndio maana serikali ikaamua kumpoteza, huwezi kushirikia na magaidi wanaoua makumi ya watz na kuleta taharuki halafu serikali ikuchekee tu kwa kuwa ni wewe ni mwandishi wa habari.
Unaweza kusaidia uchunguzi ukikamatwa wewe.

Sent from my OPPO R11s using JamiiForums mobile app
 
maji ya gundu

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
2,096
2,000
Hivi hizi familia zina hali gani mpaka sasa, je matumbo yaliyowazaa watu hawa na maziwa yaliyowanyonyesha yanajisikia vibaya kwa kiwango gani?

Najaribu kuvaa viatu vya mama yake Ben na mke wa Azory.

Nishauri utawala huu ukiondoka madarakani ndugu wote waliopotelewa na ndugu zao wajiorodheshe majina waombe uchunguzi huru juu ya WHEREABOUTS ya ndugu zao.

Kupotelewa na mme au mtoto sio Jambo dogo hata kidogo. Ndugu zangu watanzania tunapoelekea uchaguzi tutafakari pia machungu waliyonayo wanafamilia na wanaukoo waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira ya kutatanisha halafu polisi wanachukulia POA.

Adimin naomba msiu merge Wala kuufuta Uzi huu.

Akhsante.

S...!
Sio suala dogo hilo
 
superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
6,317
2,000
Awamu ya tano ndiyo umetia fora kwa uhuni huu wa kuuwa raia wake. Madhalimu wanapotawala nchi huugua. Yote haya mwisho ni tarehe 28 Oktoba 2020. Wakiiba kura watakiona cha moto kilichomfanya Mobutu na Iddi Amina Dada kufia ugenini.
Halafu anarukaruka zuchu wakati Kuna watu wamepotea bila yeye kutoa neno kwahiyo miruko ya zuchu ni Bora kuliko ndugu wa Ben na Azory ?
 
superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
6,317
2,000
Mbowe kampeni hizi omba mwili au nguo za Ben kwa mamlaka za nchi VINGINEVYO jivike nguo za msiba.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
18,075
2,000
kinachouma unakuta ukoo mzima hakuna anayejua hata nini maana ya Interpol.

jamani kuweni makini na mienendo yenu,msisababishe matatizo familia na wapendwa wenu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom