Familia nzima ya Dr. Kigwangwala imeshindwa uchaguzi Nzega leo

Kitu kinacho nishangaza mimi kuhusu hawa jamaa wa Magamba ni UROHO WA MADARAKA!

Wewe ni Mbunge wa jimbo kwa kuchaguliwa au kwa kuteuliwa bado unaenda kugombea Ujumbe wa Mkutano wa Taifa ili iweje???Kwanini watu wanakuwa na tamaa mbaya ya madaraka kwa kujirundikia vyeo au madaraka mbalimbali ilhali kuna watu hawana hata cheo kimoja???Unakuta Mbunge huyo huyo ni Waziri,huyohuyo ni Mjumbe wa CC,huyohuyo ni mjumbe wa NEC, huyohuyo ni mjumbe wa Board,huyohuyo ni mlezi wa UVCCM,huyohuyo ni Mwenyekiti ya Club fulani n.k.,n.k.

CCM badilikeni muwaachie na wengine madaraka. Msifikiri nyie kuwa mna akili sana kuliko watu wote,after all hatuoni huo uwezo wenu katika kuongoza zaidi ya kuendekeza ufisadi na umalaya! Badilikeni!
Problem solved
 
Aisee
Kama ambavyo niliwajuza leo ni kuwa Mh. Kigwangala leo alikamatwa na rushwa wakati wakiwa katika harakati za kuomba kushinda....matokeo yametoka kama ifuatavyo...Mh Kigwangwala aligombea nafasi ya ujumbe wa Mkutano mkuu wa taifa kupitia wazazi na bahati mbaya amedondoka...mkewe aligombea mkutano mkuu wa taifa kupitia UWT nae kwa bahati mbaya ameanguka na mdogo wake aligombea mkutano mkuu wa taifa kupitia Vijana nae kwa bahati mbaya ameanguka.....poleni sana kwa kushindwa na kimbilieni Chadema
 
Back
Top Bottom