Familia Nzima Wajinyonga Kukimbia Hali Ngumu ya Maisha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
Familia Nzima Wajinyonga Kukimbia Hali Ngumu ya Maisha
3771170.jpg

Saturday, December 19, 2009 6:51 PM
Familia moja ya Kihindi inayoishi Dubai wamejiua kwa wakati mmoja kwa kujinyonga wakiacha ujumbe kuwa maisha magumu ndio yaliyopelekea wachukue uamuzi huo wa kuzitoa roho zao. Watu watatu wa familia toka India yenye makazi yake katika mji wa Dubai wamefariki dunia baada ya kujinyonga huku mtu wa nne ambaye ndiye aliyetoa wazo hilo la kujinyonga amenusurika maisha yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, baba mmoja wa Kihindi aliwashauri wanae wawili na mkewe wajinyonge kwa wakati mmoja ili kukimbia hali ngumu ya maisha iliyokuwa ikiwakabili.

Siku ya jumatano mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40, mkewe mwenye umri wa miaka 38, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 22 na mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 20 walijifunga kitanzi na kujitundika kwenye feni la kwenye dari la nyumba yao iliyopo kwenye maeneo ya Karama mjini humo ili wafariki wote kwa wakati mmoja.

"Baba wa familia hiyo alikiri kuwa yeye ndiye aliyetoa wazo la kujiua", alisema Mkurugenzi wa kitengo cha makosa ya jinai cha Dubai, Khalil Ebrahim alipokuwa akiongea na gazeti hilo.

Baba huyo aliwaambia polisi kuwa kitanzi chake kilichoropoka toka kwenye feni na hivyo kunusurika maisha yake wakati mkewe na watoto wake hawakuwa na bahati kama yake na wote walifariki dunia.

Familia hiyo iliacha barua ikisema kuwa hali ngumu ya kiuchumi ndiyo iliyowafanya wachukue uamuzi huo.

Mwanaume huyo alikuwa akimiliki duka la nguo lililopo kwenye ghorofa alilokuwa akiishi na familia yake. Biashara yake ilikuwa haimuendei vizuri kama kawaida.

Dubai inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na madeni makubwa kufuatia mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani.

http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3771170&&Cat=2
 
Huyo mzee akili hana, badala ajitahidi kufight zaidi, anatoa ushauri wa kijinga... sasa hatima yake ni jela
 
Too bad!...Matatizo yakiingia ndani ya nyumba yanachapa sana...kweli hawa ndugu walikosa ushauri nasaha...Pole zao.

Lakini ndo madhara ya baba ndani ya nyumba kutokusimama katika zamu yake!
 
Too bad!...Matatizo yakiingia ndani ya nyumba yanachapa sana...kweli hawa ndugu walikosa ushauri nasaha...Pole zao.

Lakini ndo madhara ya baba ndani ya nyumba kutokusimama katika zamu yake!

Mbaya zaidi sasa wanateseka huko jehanamu maana wamejiua na sehemu yao ni huko. May GOD forbid.
 
Ni tatizo la kutunza matatizo rohoni kama mzigo wa Almasi.Athari zake ni kuhisi upo peke yako mwenye matatizo hapa duniani>(P.T.O)
 
Too sad........ & very shameful act!
hommie,
mbona haya mambo kwa wanyalu tunaona kawaida tu?...sisi kuzila,kujinyonga na WOW!wow!wow! Sana tu.nipo chawote nimeagiza kitu yako ile.pembeni totooz naiaga aga si unajua zimebaki 23days?..:-D
 
kuna maamuzi mengine huwa ni magumu sana hapa dunia
mkasa huu kweli wa ajabu
 
Back
Top Bottom