Familia kubwa kuliko zote nchini Uingereza inayoishi nyumba moja (watoto 22)

The Radford Family

Noel (50) na Sue (46) Radford walikuwa mayatima na walikutana wakiwa wadogo.
View attachment 1847101

Sue alipata mimba akiwa na umri wa miaka 14 huku Noel akiwa na 18. Walikaa bila kongeza mtoto hadi walipooana binti akiwa na miaka 17.
View attachment 1847102

Tangia wakati huo karibu kila mwaka Sue huwa na ujauzito hadi leo hii 2021 ana mtoto wa 22 aliyezaliwa 2020, wavulana 11 na wasichana 11.
View attachment 1847111
View attachment 1847112
View attachment 1847113
Mimba yake ya 17 iliharibika ikiwa imeishakuwa kubwa, walimzika mtoto na kila mwaka humpelekea zawadi kwenye kaburi lake na huwa wanasafiri na picha yake kila wakisafiri. Bado wanamuhesabu kama mwanafamilia (asingehesabiwa wangesema wana watoto 21 tu).
View attachment 1847114
Kwa sasa Wana wajukuu 6.

Watoto wanne wakubwa (mkubwa 32years) wanaishi kwao na familia zao ambapo sio mbali na nyumbani. Wengine 18 bado wapo wanachangamsha jumba lao lenye vyumba 10.
View attachment 1847118

Unaambiwa kelele za watoto wakiwa wanacheza nje ya nyumba ni kama shule wakati wa break.
View attachment 1847123
View attachment 1847124
Baba alikuwa akifanya kazi kama Baker kwenye bakeries mbalimbali na sasa anamiliki Bakery yake akisaidiwa kazi na wanawe wawili anaowalipa.
View attachment 1847126

Bakery ndo inayoendesha maisha yao, watoto wanasoma private schools, wamenunua jumba lao, watoto wana afya na furaha. Wanaweza kwenda "vacation" familia nzima.
View attachment 1847131
View attachment 1847132
Kuna kiasi fulani cha pesa huwa wanapewa na serikali kama familia zingine zote huko Uingereza wanazopewa kulingana na idadi ya watoto (child benefits).

Wanakwambia watu wanafikiri wao wanazaa tu kwakuwa ni wavivu na wanategemea misaada lakini wao wana familia kubwa kwasababu wanapenda kuwa na familia kubwa na wanafanya kazi kwa bidii na wala hawategemei misaada ya watu wasiojiweza.

Reality shows, interviews wanazopata na YouTube channel yao zitakuwa zimewasaidia ku boost maisha. Kwakweli ukiwaangalia huwezi kusema ni "masikini".
View attachment 1847188

Wanatumia kama 350 pounds sawa na Tsh. 1,123,000/= kila wiki kwa ajili ya chakula pekee. Inabidi mama aende shopping Kila siku kununua vyakula. Wanasema kipindi watoto wamefunga shule ndo balaa, watoto wanakula kama nzige (locusts).
View attachment 1847137
View attachment 1847140
View attachment 1847191
Baba ndio mpishi mkuu wa familia. Mama mara nyingi ana deal na watoto na usafi.
View attachment 1847143
View attachment 1847146
View attachment 1847148
Wanakwambia karibu kila wiki kuna birthday ya mtu, na kama desturi lazima wakate keki. Mama mwenyewe kasema ana "birthday fatigue". Baba anasema hata hakumbuki tarehe za wanawe za kuzaliwa.
View attachment 1847161

Bila kusahau sherehe kubwa ya Krismas ambapo watoto wote hununuliwa zawadi.
View attachment 1847167
View attachment 1847171
Wanasema wao sio matajri, hawanywi pombe, hawavuti sigara, hawatoki kula out, hawanunui magari ya kifahari. Hela yote wanayopata inarudi kwa watoto wao.
View attachment 1847199

Wameshazoea kila wakienda vacation lazima watu wawanyoshee vidole na kuwahesabu.
View attachment 1847185

Mtoto mmoja alisema kwenye interview Moja kuwa kuna tendency ya kuchelewa kuondoka nyumbani kwa watoto hao kwani wanapapenda nyumbani kwao hawatamani kuondoka.
View attachment 1847203

View attachment 1847109
Waambie Hawana akili..
Hahaha wewe mwenye akili unaishi stoo kule buza
 
Child benefit inaongezeka kadri ya mzigo wa watoto, hapo watoto wao wakubwa unakuta wapo kwenye jobseekers allowance, hawana kazi lakini kila wiki wanapokea hela tokea serikalini! Matibabu bure NHS, Wasituzuge!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Na Magufuli akikushauri unampinga
Zuzu akikushauri, ukafuata ushauri wake, wewe unakuwa ni Zuzumagic.
Jitu linakwambia uzae wakati huohuo kafanya MAISHA yawe magumu Sana, haajiri, hapandishi watu vyeo Wala madaraja, hamna pisho, mtaani kaua biashara, kaua kilimo yaani kaua uchumi kwa ujumla wake, hai watoto utawalisha Nini?
 
Back
Top Bottom