FAMILIA: Je, Unahitaji kuwa na Ndoa Imara, yenye Furaha na Amani? Soma hapa...

Lasthope kitu cha kwanza. 1) Jifunze kuongea maneno ya kushukuru. Shukurani ni jambo ambalo humfanya mtu ajisikie vizuri na kufanya vizuri zaidi kwa ulichomsi fia na unapoacha kushukuru unavunja moyo.

2) Fanya vitendo vya uungwana na ukarimu,endeleza kufanya vitendo vya ukarimu ulivyovifanya kabla ya ndoa.

Mfano: Nendeni matembezini pamoja, mweleze mwenzi wako jinsi unavyomthamini na kumpenda, tumia muda kukaa na kuongea na mwenzi wako,ombeni pamoja na kuwa makini kuongea naye wakati umekasirika.

3) Mkubali mwezio wa ndoa,mkubali mwenzi wako hata kama ana kasoro japokuwa kuna mambo ambayo huwezi kuvumilia na kuacha yatendeke chukua hatua kuzuia mwenendo huo.
 
Kuna memba ameniomba niseme yale ninayoona yanafaa kuhusiana na hii kitu na akasema itakuwa vyema kama nitaanzisha mada kuyahusu nami bila hiyana nimeona niseme machache na naamini wachangiaji wataongezea mengine

Haya nitakayoyasema hapa ni mtazamo wangu na kama unahitaji kuoa/olewa basi nakushauri uyasome na uyazingatie kwani ni mtazamo wangu kuwa kama unahitaji ndoa basi fanya haya

Kama hauna mpango wa kuingia kwenye ndoa pita kimya kimya tu

Karibu ...

Ni muda sasa makelee yamezidi kuwa hakuna wa kuoa au hakuna wa kuolewa,hizi kelele zimezidi na hii ni dalili kuwa kuna tatizo mahali na sidhani kama kuna jitihada za kutosha zinafanyika kutatua hili tatizo

Kimsingi karibu watu wengi tu wanahitaji ndoa na tatizo linakuja lilelile nani wa kuoa/olewa?Tutake tusitake kama kweli tunahitaji ndoa ni lazuma tubadilike hasa kimtazamo

Maendeleo yameongezeka sana na muingiliano wa tamaduni umeleta balaa na mema mengi sana,kama kuna mtu anahitaji kuwa na ndoa iliyoimara hana budi kwanza kubadilika na kukubaliana na utamaduni anaoishi ili kuweza kuingia kwenye ndoa kama hutaki ndoa basi baki hivyo hivyo

Hapa nitaeleza yale ninayodhani kuwa kama tukiyazingatia basi yanaweza kutusaidia sana kubadilika na nitayaweka kwenye makundi mawili kwa kutofautisha jinsia

WANAUME

Kwenye suala hili Wanaume tumekuwa na matatizo kadhaa na haya hapa ni baadhi

Elimu

Elimu imekuwa tatizo sana linapokuja suala la ndoa,kijana akimaliza elimu hasa kuanzia O level au chuo anaanza kuwa na mawazo kuwa wale ambao hawajasoma sio wife material na hawafai kabisa kuolewa
Hili liunaweza kuwa na ukweli lakini ni mdogo sana kwani ili mtu awe bora kwenye ndoa sio lazima awe ameenda sana shule,ushahidi wa hili ni ubora wa mama zetu ambao wengi kama walikuwa wamesoma sana basi ni darasa la saba na sisi ambao ni wa siku nyingi kidogo basi mama zetu wengi walikuwa hata shule hawajaenda lakini hilo halikumfanya asiwe mama bora

Na hata hawa viongozi wetu tunaowasifia na kuwaita kielelezo cha Waafrika au waasisi wa mataifa yetu wengi wao walilelewa na wazazi ambao hawakupata kabisa elimu au walipata kidogo sana kutokana na mambo mengi sana.Sitayazungumzia hayo yaliyosababisha wasipate elimu kwani hiyo ni mada nyinmgine lakini kitendo cha kukosa elimu hakikuwafanya wakawa mama wasiofaa na matokeo yake malezi yao ndio hayo yamewafanya hao kuwa viongozi bora

Ukisasa

Hili ni tatizo jingine kubwa sana la vijana,vijana siku hizi wamekuwa na mambo ya ukisasa sana hadi ile hadhi ya kiume imepotea kabisa na kumekuwa hakuna tofauti na wanawake labda unaweza kuiona tofauti hiyo kwenye mavazi tu

Vijana siku hizi wanapaka poda,wanatinda nyusi yaani unakuta vijana wanakabana makoo na warembo kwenye yale maduka ya urembo.Siku hizi huwezi kujua hii dresing table kama ni ya mwanamke au mwanaume yaani imejaa vipodozi hadi karaha

Sisemi kuwa wanaume au vijana wasijipende lakini kuna limitation ya haya mambo,siku hizi vijana wanatembea na vioo kwenye walllet zao utadhani wakina dada,ukimkuta ofisini kaweka poda,hii ni laana kabisa na kamwe usidhani kuwa kuna mwanamke yeyote yule anaejitambua atakubali kuolewa na mwanaume au kijana wa aina hii

WANAWAKE

Wanawake nao wana yao

Elimu

Tukubali au tusikatae hili ni tatizo.Wanawake wana matatizo yanayofanana na ya vijana kwenye hili lakini kwa wanawake linaonekana kama ni kubwa sana,Siku hizi mwanamke akishafika O level au zaidi basi huyo anawaona watu wengiine kama sio watu sanasana wanaume hili ni tatizo lakini ukiliangalia kwa undani linaonekana tatizo hili linaanzia kwenye asili

Kiasili mwanamke ameumbwa kuwa chini ya mwanaume hili ni kweli mtake msitake na mwanamke yoyote yule akiwa na uwezo kifedha kumzidi mwanaume au akiwa na elimu kumzidi au kwa kifupi akiwa na chochote kile cha kumzidi mwanaume basi mwanamke huyo humuona mwanaume huyo kama sio mwanaume vile,hili ni suala la kimaumbile zaidi,lakini ni tatizo

Kama mwanamke kaumbwa hivi basi ni wazi kuwa hakustahilio kukipata kile kinachompa tatizo kwenye maisha yake ya leo,najua mnaweza kutokukubaliana na hili lakini ki ukweli mwanamke ndivyo alivyoumbwa.Sisemi mwanamke asisome lakini kuna haja ya kuliangalia hili kwa makini kama kweli tunahitaji kuwe na ndoa au familia zile ambazo tunazitamani

Kama mwanamke atakuwa na degree basi huyo ambae atamuona na kuishi nae kwa angalau amani basi ni mwenye elimu kubwa zaidi yake,sasa jiulize ni wangapi wanaelimu ambao watatosha kuwaoa hawa wanawake wanaomaliza chuo kila uchao?Kila siku ukiangalia ndoa ambazo zina amani ni zile ambazo either mwanamke hajasoma kwa kiwango cha kufikia form 6 au kama mwanamke mesoma basi ameamua kuishi kimazoea tu

Sisemi kuwa wanawake ambao hawajasoma hawana matatizo na pia sisemi kuwa kila mwanamke ambae amesoma ana matatizo lakini ninachotaka kusema hapa ni kuwa wengi wa wanawake ambao wamesoma wana matatizo

Fedha
Hili jambo limegawanyika kwenye makundi mawili

1:Kuna wanawake ambao wamefanikiwa kupata mafanikio ya kifedha
2:Kuna wanawake ambao kwao hela ni kila kitu


Wenye mafanikio kifedha

Hawa kuolewa imekuwa tatizo sana kwako kwasababau kwanza wako busy sana na shughuli zao na kama ujuavyo sisi Waafirka tunahitaji mwanamke ambae ukirudi nyumbani unamkuta na ukute amekupikia chakula,sasa huyu ni mara chache sana utaweza kumkuta nyumbani na kukupikia chakula

Chakula cha kupikiwa na mke kinanoga jamani sasa haya mabo ya kupikiwa na beki tatu tutayaweza wapi?

Hili ni tatizo kubwa sana kwa aina hii ya wanawake lakini kuna tatizo lingine ambalo limekuwa likiwatatiza sana hawa wanawake ambao wanamafanikio ya kifedha,tatizo hili ni kama hilo la wenye elimu,wanakwaida ya kuwaona wanaume ambao wamewaziki kipato kama vile sio wanaume na tatizo hili nalo ni la kimaumbile zaidi lakini kikubwa sana wanawake hawa wanashindwa kuolewa mara nyinmgine hata kama atakuwa hana matatizo hayo kwa sababu ya wanaume kuwaogopa wanawake hawa

Sasabau za kuwaogopa zinatofautiana kutoka kwa mwanaume mmoja hadi mwingine lakini kitendo cha mwanamke kuwa na mafanikio kifedha ni tatizo kwao na ni sababu mojawapo ya kutokupata mume

Wanawake ambao wanaona fedha ni kila kitu

Hawa nao hili limekuwa ni tatizo kwasababu wamejikuta wakikaa muda mrefu sana biula kuolewa kwasababu wanawatafuta sana hawa wanaume wenye hela na bahati mbaya sana hawa ni wachache na wengi wao wanakuwa wameoa na hivyo wanawake hawa kuishia kuwekwa nyumba ndogo tu

Kingine ni kuwa wanawake hawa hawataki kuwajibika na kukubali kuolewa na kuyatengeneza maisha yao wanataka wakute maisha yameshatengenezwa tayari,kwanini usinyanyaswe na mwanaume wakati umemkuta tayari ana kila kitu na hata hujui aliteseka vipi kuzipata hizo hela?
Kama unataka heshima nenda kaolewe na mwanaume ambae haja setle kisha muanzie chini au hamjui kuwa maisha yanatengenezwa?

Pia wasichokijua wanawake ni kuiwa hawa wanaume wenye hela wengi utakuta hawakufika hapo peke yao,yaani unakuta kuna mwanamke nyuma yao na baada ya kupata tu fedha waliamua kuwaacha hawa wanawake waliowasaidia kufika walipofika na kutafuta wale wanaodhani ni sawa kuwa nao kwenye mafanikio,sasa mwanamke ambae atakutana na mwanaume wa aina hii atajikuta akitumiwa na kuachwa kwasababu hawa watu tabia yao siuo nzuri kiujumla na mara nyingi wanawake hawa huishia kuzalishwa na hawa wanaume na mwishowe kuachwa na kuja kupata shida sana kupata mume kwani wanaume nao siku hiziz ni wachache walioko tayari kuoa mwanamke mwenye watoto

Jamani sisemi mwanaume akiwa hana hela ni mwema,wapo mabazazi wengi tu lakini linapokuja suala la mafanikio ya kifedha ni bora mwanamke ukawa makini sana unapokutana na mwanaume wa aina hii

Ukisasa
Wanawake wamejikuta wakikaa muda mwingi sana bila kupata waume wa kuwaoa na kuishiwa kuchezewa tu kwasababu ya tatizo hili la ukisasa

Wanawake mnatakiwa mjue kuwa mwanaume yoyote yule ambae ni husband material ni lazima kuna mambo yanamfanya hivyo

Husband material anakuwa na sifa zifuatazo
Anamjali mkewe
Anajali watoto
Ni msikivu
Mpole kiasi
Mbahili kiasi
N.k


Wanawake au mabinti wanatakiwa watambue kuwa mwanaume yoyote yule mwenye sifa hizo mara nyingi huonekana kama wa kizamani hivi na mabinti mwanaume wa hivyo humuita mshamba na hawamuitaji,Hawamutaji kwasababu mabinti wengi sana wanahitaji kwenda salun za gharama,kwenda kujirusha kila w/end,kutumia vipodozi na mavazi ya gharama,hawataki kupika n.k

Halafu cha kushangaza wanawake hao hao wanadai eti wanahitaji ndoa,ni ndoa gani hiyo?

Wengi wa aina hii ya wanawake huishia kuangukia kwenye mikono ya wanaume mabazazi na kuishia kufanikiwa kutumia hela za hawa mabazazi lakini ndoa haipo

Hakuna mwanaume yoyote yule mwenye uchungu wa familia anaehitaji maendeleo atakaekubali kuishi na mwanamke wa aina hiyo kama unahitaji ndoa iliyo imara kubali kubadilika

Yapo mengi sana ya musema lakini kwa sasa hayo yanawafaa

Ninachotaka kuwaambieni ni kuwa kama kweli tunahitaji kuzipata ndoa zile ambazo tunaishia kuzisikia kwenye hadithi basi hatuna budi kubadilika,najua hiki ni kitu kigumu sana lakini ndio dawa yenyewe

Wenu Baba Paroko wa Parokia ya MMU
Wasalaam

Jumatatu njema ......
 
Hebu rudi kwenye maandiko matakatifu hususani Biblia inasemaje juu ya hii topic yako?
 
Husband material anakuwa na sifa zifuatazo
Anamjali mkewe
Anajali watoto
Ni msikivu
Mpole kiasi
Mbahili kiasi
N.k

.[/B][/U]

sasa kama hamna watoto utajuaje kama ni husband material? kwa hizo sifa ina maana mpaka ujue husband material ni mpaka akishakuoa.
 
Mapenzi hayana fomula ila yana changamoto za kufanana.
Kukabiliana nazo, kila mtu awe mbayu wayu.
 
Back
Top Bottom