FAMILIA: Je, Unahitaji kuwa na Ndoa Imara, yenye Furaha na Amani? Soma hapa...

This is easier said than done. Kwa mfano unajisikiaje ukiwa wewe ndo unamnunulia mwenzio zawadi kila mara, yeye wala hata hajisumbui na si kwamba hana pesa ila tu anona si muhimu or whatever, unakuwa wa kwanza kukomunicate everytime yeye wala, baada ya ndoa habari ya outing haoni umuhimu , anona kama ni anasa, je bado utakuwa na moyo wa kufurahia one way bila kurudishiwa?Je utakuwa na moyo huo?

Mkuu,
Kutoa ni kwa wote.... ukipenda kupokea uwe tayari kutoa pia.... its a two way traffic..
Muhimu mke na mume kufanyiana yale yote yaliyo mema...na pia kuwa tayari kujua mwenzio anapenda nini umfanyie au asichopenda ili usikifanye.
 
Uwazi na uaminifu,mapenzi ya kweli...ndani ya ndoa ndio msingi wa ndoa na maisha yenye furaha.....kushirikishana kwenye maamuzi piaa....hekima na busara.....zitawale....taaam za mwili na mawazo ziepukwe....ni summary tu
 
FUNGUO ZA KUJENGA NDOA IMARA NA MAHUSIANO YA KUDUMU

USIKAE NA DONGE MOYONI

Kitu kizito kuliko vyote kukibena duniani ni DONGE MOYONI (grudges)

Pia unaweza kuathirika zaidi na kile umeweka moyoni kwani mwenzako anaweza kuwa hajui.

Kuweka vitu moyoni bila kuvitoa au kuzungumza na mwenzi wako huweza kuathiri afya na amani.

Kawaida kama una hasira hakikisha unazimaliza mapema na kuelewana na mwenzi wako kabla jua halijazama na kama ni usiku hakikisha unaenda kulala huku umeshalitoa donge lako.

FAHAMU KWAMBA HONEYMOON SIYO MAISHA NDOA

Kuna tofauti kubwa kati uchumba, Honeymoon na maisha ya ndoa, uchumba na Honeymoon hupewa moto kemikali ambazo zimo ndani yetu. Hatua ya pili ambayo ni ndoa yenyewe hapa tairi linakutana na barabara ili kuweka wazi uimara na udhaifu. Katika ndoa ni majukumu na kuwajibika na familia iliyoanzishwa, wakati uchumba na Honeymoon ni kuburudishana.

MUNGU KWANZA

Kumweka Mungu kwanza katika ndoa, huleta furaha ya kweli (joy) faraja na ulinzi. Kumweka Mungu kwanza maana yake mume na mke wanaishi kwa utii na amri za Mungu mwanzilishi wa ndoa wanaomba pamoja na kuwa na mahusiano yanayoongozwa na Mungu.

Kwa vipimo vya kibinadamu huwezi kuwa na furaha siku zote kwa safari ndefu kama ya ndoa furaha ya kweli hupatikana kwa kumuweka Mungu namba moja.

MFAHAMU MWENZI WAKO NA KUJIFAHAMU WEWE MWENYEWE

Baada ya mapenzi ya Honeymoon kwisha wanandoa huwa na mgodi wa kuanza kuchunguzana na kufahamiana. Wakiwa Honeymoon wanandoa huona kila kitu shwari, wakianza maisha ya ndoa kila mmoja huanza kuona makosa kwa mwenzake hata Kirusiyo hiyo ni nafasi ya wanandoa kufahamiana ni nafasi nzuri ya wanandoa kusifiana, kutumia muda pamoja, kupeana zawadi, kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani, kubusiana na kukumbatiana (touch)

KUWA MSIKILIZAJI MZURI

Binadamu ana asili ya kupenda kuongea zaidi kuliko kusikiliza, kusikiliza kuna maana zaidi kuliko kuongea, wanaume Huongea ili kitu kifanyike na mwanamke Huongea kuchangia wazo na hisia zake. Kuna wakati kila mwanandoa anahitaji kusikilizwa wanaume ni vizuri kuwasikiliza wake zao wanapotoa mawazo yao na hisia zao.

Mwanamke huongea maneno 45 elfu kwa siku, na mwanaume 15 elfu, ni nani anahitaji kusikilizwa zaidi?

KICHEKO

Wanandoa wanahitaji kuwa na kicheko siyo kuwa serious kila wakati kutaniana kusikopitilizwa huongeza furaha katika ndoa pia ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Wanandoa ni muhimu kuwa na wakati ambapo wanaweza kukaa pamoja na kuwa na kicheko iwe ni kuangalia TV na kusimuliana hadithi ambazo zinawafanya mcheke ni vizuri wanandoa kucheka wakiwa wao wenyewe au wakiwa pamoja na watu wengine.

Kicheko huleta raha katika ndoa.

JIFUNZE KUKUBALI KWAMBA UMEKOSA NA KUOMBA MSAMAHA

Binadamu wote tunafanya makosa na wakati mwingine hayo makosa huumiza tunaowapenda. Lazima tukumbuke wakati tumekosa tunahitaji tuombe msamaha.

Usizunguke (indirect way) bali be straight sema “Nisamehe au I am sorry”. Pia usibadili topic au kuanza kusifia ili usiombe msamaha.

Pia tunahitaji kufahamu kwamba wenzi wetu si mara zote wapo perfect kama ulivyo wewe (imperfect).

Pia ni vizuri kufahamu kwamba ndoa ni kazi inayoendelea na siyo mwisho wa safari.

MHESHIMU, USIMDHARAU

Kumdharau mwenzi wako wakati mwingine huwa kitu rahisi sana. Mwanzo wa mapenzi hata kama kuna hitilafu mara nyingi huitilii maanani, una minimize, lakini baada ya honeymoon kwisha utaona na kukumbuka/ Tambua mambo mengi ambayo huyapendi na unaweza kuanza kupambana nayo na kumdharau mwenzi wako.

Kumdharau mwenzi wako ni kama mmomonyoko ambao ni sumu kwenye mahusiano.

Mwanandoa mwenye busara hawezi kumuaibisha mwenzi wake bali ataongea kwa hekima na kumaliza tofauti zozote kwa upendo.

Kawaida angalia uwezo wake na si udhaifu wake.

USICHUJE (filtering)

Usimchekeche na kumbandika jina la kudumu kwamba mara zote yupo vile:

Sentensi zinazoanza na haya maneno uwe makini sana.

Kila siku unafanya KirusiiKirusii…………………..

Mara zote nakwambia lakini………………:

You never……………………, You always……………………

Mara nyingi Ukitokea msuguano wengi huanza kulalama kwa kutumia hayo maneno huwa na maana kwamba unafanya the same mistake over and over na anakupa hicho kibandiko kama jina la mkosaji wa kila siku.

Si kweli kwamba unaweza kufanya makosa yaleyale kila siku, muda wote miaka yote.

WEKA MKAZO KWENYE UWEZO NA SI UDHAIFU

Mwanamke na mwanaume wapo tofauti siku zote na ni mpango wa Mungu kuwa tofauti ili kwa tofauti tuweze kusherehekea uumbaji wa Mungu na ili mke na mume waweze kila mmoja kumridhisha mwenzake.

Huwezi kuwa na mwenzi ambaye ana udhaifu mwingi kuliko uwezo na ukiona ana udhaifu mwingi kuliko uwezo basi tatizo ni wewe si yeye.
 
Kuolewa kwa wakati huu ni bahati sana kutokana na wengi kukata tamaa ziambatanazo na wanaume wengi kuficha makucha kulikoni wanawake. Mashauri mengi yanaripotiwa kuwa wanawake wengi kwa sasa hawapendi kuolewa kutokana na matukio yakutisha ndani ya ndoa likiwamo la mihogo mingi kufubaa na kushindwa kurutubisha ipasavyo.

Hivyo basi hakikisha wote mnafanya mazoezi mepesi kila mara, zingatieni chakuala bora,matunda yakutosha, punguzeni malumbano(ni vigumu malumbano kuisha), acha pombe au kunywa bia 4 na maji lita 2 kwa wakati huo huo.Maji ya vuguvugu kuogea pia ni mazuri.

Wanawake msiwatete waume kwa shida ya mihogo yao na hakkisha unamjali. Wadada jamani hakikisheni nyie ndio wakulaumiwa kwa ndoa kuvunjika kwani asilima kwabwa mwapenda maisha ya mkato hivyo kuambatana na tamaa nzito za kupata wepesi wa maisha.

Mbali na kubakwa wanaume hawanauwezo wowote wa kushawishi ndoa kuvunjika iwapo wadada wote watakataa ushawishi toka kwa akina Adamu.Hii ni kwa sababu akina HAWA ndio wanamiliki rasilimali adimu na wakiamua ndoa hazivunjiki na wala hata magonjwa mengine yazinaa ukiwamo UKIMWI yatapugua kwa kiasi kikubwa. Jamani jilaumu mwenyewe kwa kuwa kwenye shida ya ndoa na usijite kuwa ndani ya ndoa

Nawakilisha.
 
Kwa hio mhogo tu ndio garantee ya wanawake kutaka kuolewa na ndoa kudumu?
 
Kuolewa kwa wakati huu ni bahati sana kutokana na wengi kukata tamaa ziambatanazo na wanaume wengi kuficha makucha kulikoni wanawake. Mashauri mengi yanaripotiwa kuwa wanawake wengi kwa sasa hawapendi kuolewa kutokana na matukio yakutisha ndani ya ndoa likiwamo la mihogo mingi kufubaa na kushindwa kurutubisha ipasavyo.

Hivyo basi hakikisha wote mnafanya mazoezi mepesi kila mara, zingatieni chakuala bora,matunda yakutosha, punguzeni malumbano(ni vigumu malumbano kuisha), acha pombe au kunywa bia 4 na maji lita 2 kwa wakati huo huo.Maji ya vuguvugu kuogea pia ni mazuri.

Wanawake msiwatete waume kwa shida ya mihogo yao na hakkisha unamjali. Wadada jamani hakikisheni nyie ndio wakulaumiwa kwa ndoa kuvunjika kwani asilima kwabwa mwapenda maisha ya mkato hivyo kuambatana na tamaa nzito za kupata wepesi wa maisha.

Mbali na kubakwa wanaume hawanauwezo wowote wa kushawishi ndoa kuvunjika iwapo wadada wote watakataa ushawishi toka kwa akina Adamu.Hii ni kwa sababu akina HAWA ndio wanamiliki rasilimali adimu na wakiamua ndoa hazivunjiki na wala hata magonjwa mengine yazinaa ukiwamo UKIMWI yatapugua kwa kiasi kikubwa. Jamani jilaumu mwenyewe kwa kuwa kwenye shida ya ndoa na usijite kuwa ndani ya ndoa

Nawakilisha.

mantiki ya mada hii ni nini??nimetoka kapa maana nimekuta uzi unavipengele kama 3vyote tofauti na uzi wenyewe!!labda utarudi kunielewesha kama hautajali!Sasa sijajua ulikuwa na maana walio tayari kwenye ndoa??sasa na ..............anyway ngoja nisubiri wa dau!
 
Nyakatihizi kuna hatari kwenye ndoa za watu kutokuaminiana, usaliti umekuwa mkubwa mnokuliko wakati mwingine wowote.Waume hawashikiki kwa vischana vinavyoonyeshakifua kimejaa embe mbili , wake nao hawakamati kwa wanaume wenye mshiko na wasiona mshiko ili hali ni kuvutwa na kila tamaa ya mwili na dunia na shetani wa uzinifu .vilio kwenye ndoa ni vingi mno kuliko hata tunavyolia na majanga mengine ya kitaifa. Ukatali kwenye ndoa unazidi kukua kwa sababu ndoa nyingi hazijajengwa kwa misingi imara ya kujua neno la Mungu.Hii ni hatari sana kwa wanandoa wanaoishi bila kuifanya ndoa yao imjue Mungu na matakwa yake kwa wanandoa.Ifanye ndoa yako kuwa mpya na yenye furaha kila siku utaona matokeo yake na mtastawi kwa kila kitu......................... mikwaruzano haitakuwepo..........mtasharikiana kwa kila jambo............hakutakuwa na kufanya mambo kisirisiri................hautaweza kusaidia ndugu zako au rafiki zako kisirisir............hautawaza wanaume au wanawake wa barabarani....................

Ndoa nimpango wa Mungu tangu alipomuumba Eva kwa ajili ya Adamu.Ndiyo maana mwanamumehumwacha baba yake na mama yake akambatana na mkewe nao wawili huwa mwilimmoja.Ndoanyingi za kikristo zimekuwa na matatizo mengi kwa sababu hazikujengwa kwenyemsingi mzuri wa neno la Mungu.Na mara nyingi tatizo linalonekana ni masuala yapesa na mambo mengine ya kinyumba.Kwa mfano yawezekana uko kwenye ndoa, nikweli wewe ni mwanamume mwenye uwezo wa fedha, wengine wanawanunulia magari aukuwafanyia mambo mazuri wake zao lakini wewe humfanyii hivyo mke wako. Hata kwa wanawake pia, wapo ambao wamekuwa wakiwafanyia yaliyomazuri waume zao hasa kwa kuwapa fedha na kadhalika, lakini wanashindwakufahamu kuwa suala la kula vizuri au fedha siyo vitu muhimu kwa wanandoa.

Lamuhimu katika ndoa ni kuishi kwa upendo na amani na pia kuangalia pandezote, kwa mfano kama ni kweli uko sawa kwenye sualala fedha, unapaswa kuangalia pia katika suala la mahusiano na mahaba kwaujumla, je, kama mwanamume, una uwezo wa kushughulika kama ambavyo mwanamumeanapaswa vilevile na mwanamke ana uwezo wa kushughulika kama ambavyomwanamke anapaswa.

Jambola msingi kwa wanandoa kupenda kuwa na mazungumzo ya wazi huku mkiwa na shinaimara katika Neno la Mungu. Eeh hata nyumbani,utakuta Pia mke usipende kumuachia housegirl kila kazi za kumtunza mme wako na watoto wako.Ni wajibu wako mwanamkekuhakikisha mumewe wako anajisikia raha kuwa na wewe na hakukosea kukuoa na hana sababu ya kutembea nje ya ndoa kwa sababu roho yake itakuwa imetulizwana mahaba yako.Lakinini vizuri wakati fulani kumuuliza unaonaje leo nikakupikia chapati, viazi,tambi na kadhalika.Pia wanaume utakuta wanaendamatembezi bila kumjulisha mke wake na akirudi akiulizwa ulikuwa wapi eeheanakuwa mkali kama nyati aliyekosa malisho kwenye mbunga ya Masai Mara.

naweza k
Maranyingi wana ndoa wamejikuta kila mtu anafanya mambo yake bila kumshirikishamwenzake kwa kukosa uaminifu kati yao.Unaweza kufanya kitu ukafikiriunatengeneza, kumbe unaharibu. Mpendwa tuzifanye ndoa zetu kuwa zenye upendo na salama nyingi.Kitu muhimu kwenye ndoa ni kuwa na upendo maana upendo uvumilia yote shida na raha,hauhesabu mabaya.Mara nyingi watu wana pokuwa kwenye hatua ya uchumba huwa wanaupendo usiokuwa na kifani lakini wengi wanashindwa kuendelea kuutuza upendo huopindi wanapoanza maisha ya ndoa.Mtume Paulo aliandika juu ya upendo katikabarua yake ya kwanza kwa wakorintho akisema ''Mwenyeupendo huvumilia,hufadhili, mwenye upendo hana wivu, hajidai, walahajivuni.Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hanawepesi wa hasira, haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hurahiaukweli.Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote na hustahimili yote.Upendo hauna kikomo kamwe(1Korintho13:4-8)'

'Kuna baraka katika maisha ya ndoa kama wanandoa wakiishi pamoja kwa upendo na kama ndugu na mwili mmoja. Kwa mwanamke anayemtii mume
wake anaweza kubadili mwenendo wa mumewe kama mwanamume huyo hajaamini neno la Mungu kwa kuona mwenendo wa mkewe ukiwasafi. Na kwa wanaume wanaowatendea wake zao kwa heshima watapokea zawadi ya uhai anaowapeni Mungu napia sala zao hazitatiliwa kizuizi na Mungu.
Kwa wanaotafuta wa chumba nilazima utafute mwenzi ambaye hamtofautiani interest na itapendeza kama kumpata mwenzi mcha Mungu na wote muwe wenye imani inayofanana na kama haifanani mmoja wenu akubali kufuata imani ya mwenzake kwa kuishika na kutenda kama inavyoelekeza.Pia acha tabia ya kutest kwanza kabla ya ndoa hiyo hupunguza upendo wakati mtakapoanza kuishi pamoja utaona kama tena hufurahishwi na penzi la mwenzi wako.

Jenga ndoa yako katika Msingi wa upendo na kumcha Mungu

 
dah niko hapa kwa mwezi mmoja sijaona post kama hii, imenivutia sana maana mii natarajia kuingia kwenye ndoa mda sii mrefu, nafikiri umeniongezea kitu ambacho sikukitilia maanani sana be4.»»» mungu akulide ili siku nyingine uelewa wako juu ya unachokiamini uwafikishie na wengine. nakutakia siku njema.
 
dah niko hapa kwa mwezi mmoja sijaona post kama hii, imenivutia sana maana mii natarajia kuingia kwenye ndoa mda sii mrefu, nafikiri umeniongezea kitu ambacho sikukitilia maanani sana be4.»»» mungu akulide ili siku nyingine uelewa wako juu ya unachokiamini uwafikishie na wengine. nakutakia siku njema.

asante na Mungu akutangulie katika kila hatua uliyonayo ili mwenzi wako utakayeishi naye awe ni tulizo halisi la moyo wako naye akufurahie siku zote za maisha yenu.Kitu muhimu ni kujua kuna majaribu mengi mno kwa wanandoa na majaribu haya yakupasa kuyashinda kwa kumcha Mungu na kwa kujitahid kuifanya kila jambo kwa ushirikiano na kusikiliza mawazo ya kila mmoja wenu.Maneno kama dear nataka tufanye hiki au kile ni mazuri sana kwa wanandoa.Pia usiache kutumia maneno kama haya kila siku sweet, honey, missing you, i love you,pole mpenzi, wewe ni mrembo,wewe ni handsome, ninabahati ya kuwa na mme/mke kama wewe na mengine yenye kuonyesha hisia za mapenzi na kuthaminiana na mwenzi wako
Ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom