FAMILIA: Je, Unahitaji kuwa na Ndoa Imara, yenye Furaha na Amani? Soma hapa...

Jamani naombeni kujua wanawake wanapenda kufanyiwa nini na waume zao. Na wanaume pia wanapenda kufanyiwa nini na wake zao. Nataka kujua experience ya watu tofauti ili nijue. Wenye ndoa zenye furaha na amani zisizokuwa na constant arguments pia nini siri yake? Roles gani kila mtu anaplay kuhakikisha marriage inakuwa bed of roses. I mean kona zote, family responsibilities, sex life, entartainment e.g outings, gifts, communication, Care etc. Kila kitu kinatakiwa kifanyweje ili kuwepo na happines ndani ya ndoa.
 

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Heshima kwenu wakuu!

Kumekuwa na mijadala anuai inayogusia suala la FURAHA, AMANI na UIMARA wa ndoa za wadau. Huu ni mjadala muhimu sana kwani ndoa ikiwa imekidhi vigezo hivi basi inazaa matunda mazuri yakiwemo malezi bora kwa watoto, ufanisi katika maisha na uimara wa familia na Taifa kwa ujumla wake.

Thread hii ina mikusanyiko ya maoni toka kwa wadau mbalimbali na tutajitahidi kuiweka kwenye bandiko hili ile ambayo inaweza kumsaidia mwenye uhitaji wa kujua zaidi.

Karibu

=====
SOME NOTABLE CONTRIBUTIONS:

1)
Binafsi nafikiri sababu za kufunga ndoa na tabia za watu wakiwa ndani ya ndoa ndio chanzo cha mafanikio au kuvunjika kwa ndoa.

Ndoa nyingi za vijana huwa ni kutokana na sababu zifuatazo:
1. Mimba isiyopangwa
2. Umri wa kuoa umefikwa
3. Nina kazi, pesa, uwezo sasa iliyobaki ni kuwa na mke/mume
4. Nitambulike katika jamii
5. Fulani ni mzuri wa sura, anavutia n.k.

Wengi hawafikirii kuwa katika ndoa kuna masuala ya msingi ya kupatana kabla ya kufunga hizi ndoa.

1. Matumizi ya fedha
2. Mtaishi wapi
3. Ndugu na marafiki
4. Maisha ya watoto- elimu, afya, mahitaji
5. Wasaidizi/wafanyakazi wa nyumbani

Wanaume mara nyingi hufikiria haya na ndio inayowaletea matatizo sana badaye;

1. Mke ni mali yangu
2. Mke lazima afuate kila nitakachosema/amua
3. Mimi ni mwenye maamuzi ya mwisho
4. Heshima ni lazima kwangu hata nikiwa nimekosea mimi
5. Ndugu yangu ni zaidi ya mke wangu

Wanawake mara nyingi na wao hukosea yafuatayo;

1. Ndugu yangu ana haki kuliko ndugu wa mume wangu
2. Ndugu wa mume wangu ni wabaya wangu hata iweje
3. Fedha ya mume ni yangu ila ya kwangu ni yangu
4. Lazima nisikilizwe mimi

Mara zote matatizo yanatokana na utofauti wa ideals kati yetu. Wanaume wengi wanaoa kwa kutumia rules za utamaduni ambao mara nyingi hutumika kukandimiza wanawake na kumuona hasitahili. Wanawake na wao wameamka nakujua haki zao.

Cha muhimu ni kuhakikisha tunaelimishana mapema kabla ya kuingia katika hizi ndoa maana majukumu yanaongezeka kadri ya siku. Kutazama mlipotoka ni muhimu sana ili mjue kubadilika kwa nyakati.

Hakuna ndoa inayo pay-off kama ndoa ambayo mwananume atampenda mkewe na mwanamke atamheshimu mumewe. Ila kumbuka ili kupata vyote hivyo lazima mchangie yawezekane msitegemee yatatokea tu.

Marriage is a full time job.

2)
FUNGUO ZA KUJENGA NDOA IMARA NA MAHUSIANO YA KUDUMU

USIKAE NA DONGE MOYONI

Kitu kizito kuliko vyote kukibena duniani ni DONGE MOYONI (grudges)

Pia unaweza kuathirika zaidi na kile umeweka moyoni kwani mwenzako anaweza kuwa hajui.

Kuweka vitu moyoni bila kuvitoa au kuzungumza na mwenzi wako huweza kuathiri afya na amani.

Kawaida kama una hasira hakikisha unazimaliza mapema na kuelewana na mwenzi wako kabla jua halijazama na kama ni usiku hakikisha unaenda kulala huku umeshalitoa donge lako.

FAHAMU KWAMBA HONEYMOON SIYO MAISHA NDOA

Kuna tofauti kubwa kati uchumba, Honeymoon na maisha ya ndoa, uchumba na Honeymoon hupewa moto kemikali ambazo zimo ndani yetu. Hatua ya pili ambayo ni ndoa yenyewe hapa tairi linakutana na barabara ili kuweka wazi uimara na udhaifu. Katika ndoa ni majukumu na kuwajibika na familia iliyoanzishwa, wakati uchumba na Honeymoon ni kuburudishana.

MUNGU KWANZA

Kumweka Mungu kwanza katika ndoa, huleta furaha ya kweli (joy) faraja na ulinzi. Kumweka Mungu kwanza maana yake mume na mke wanaishi kwa utii na amri za Mungu mwanzilishi wa ndoa wanaomba pamoja na kuwa na mahusiano yanayoongozwa na Mungu.

Kwa vipimo vya kibinadamu huwezi kuwa na furaha siku zote kwa safari ndefu kama ya ndoa furaha ya kweli hupatikana kwa kumuweka Mungu namba moja.

MFAHAMU MWENZI WAKO NA KUJIFAHAMU WEWE MWENYEWE

Baada ya mapenzi ya Honeymoon kwisha wanandoa huwa na mgodi wa kuanza kuchunguzana na kufahamiana. Wakiwa Honeymoon wanandoa huona kila kitu shwari, wakianza maisha ya ndoa kila mmoja huanza kuona makosa kwa mwenzake hata Kirusiyo hiyo ni nafasi ya wanandoa kufahamiana ni nafasi nzuri ya wanandoa kusifiana, kutumia muda pamoja, kupeana zawadi, kusaidiana kazi ndogo ndogo za nyumbani, kubusiana na kukumbatiana (touch)

KUWA MSIKILIZAJI MZURI

Binadamu ana asili ya kupenda kuongea zaidi kuliko kusikiliza, kusikiliza kuna maana zaidi kuliko kuongea, wanaume Huongea ili kitu kifanyike na mwanamke Huongea kuchangia wazo na hisia zake. Kuna wakati kila mwanandoa anahitaji kusikilizwa wanaume ni vizuri kuwasikiliza wake zao wanapotoa mawazo yao na hisia zao.

Mwanamke huongea maneno 45 elfu kwa siku, na mwanaume 15 elfu, ni nani anahitaji kusikilizwa zaidi?

KICHEKO

Wanandoa wanahitaji kuwa na kicheko siyo kuwa serious kila wakati kutaniana kusikopitilizwa huongeza furaha katika ndoa pia ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Wanandoa ni muhimu kuwa na wakati ambapo wanaweza kukaa pamoja na kuwa na kicheko iwe ni kuangalia TV na kusimuliana hadithi ambazo zinawafanya mcheke ni vizuri wanandoa kucheka wakiwa wao wenyewe au wakiwa pamoja na watu wengine.

Kicheko huleta raha katika ndoa.

JIFUNZE KUKUBALI KWAMBA UMEKOSA NA KUOMBA MSAMAHA

Binadamu wote tunafanya makosa na wakati mwingine hayo makosa huumiza tunaowapenda. Lazima tukumbuke wakati tumekosa tunahitaji tuombe msamaha.

Usizunguke (indirect way) bali be straight sema “Nisamehe au I am sorry”. Pia usibadili topic au kuanza kusifia ili usiombe msamaha.

Pia tunahitaji kufahamu kwamba wenzi wetu si mara zote wapo perfect kama ulivyo wewe (imperfect).

Pia ni vizuri kufahamu kwamba ndoa ni kazi inayoendelea na siyo mwisho wa safari.

MHESHIMU, USIMDHARAU

Kumdharau mwenzi wako wakati mwingine huwa kitu rahisi sana. Mwanzo wa mapenzi hata kama kuna hitilafu mara nyingi huitilii maanani, una minimize, lakini baada ya honeymoon kwisha utaona na kukumbuka/ Tambua mambo mengi ambayo huyapendi na unaweza kuanza kupambana nayo na kumdharau mwenzi wako.

Kumdharau mwenzi wako ni kama mmomonyoko ambao ni sumu kwenye mahusiano.

Mwanandoa mwenye busara hawezi kumuaibisha mwenzi wake bali ataongea kwa hekima na kumaliza tofauti zozote kwa upendo.

Kawaida angalia uwezo wake na si udhaifu wake.

USICHUJE (filtering)

Usimchekeche na kumbandika jina la kudumu kwamba mara zote yupo vile:

Sentensi zinazoanza na haya maneno uwe makini sana.

Kila siku unafanya KirusiiKirusii…………………..

Mara zote nakwambia lakini………………:

You never……………………, You always……………………

Mara nyingi Ukitokea msuguano wengi huanza kulalama kwa kutumia hayo maneno huwa na maana kwamba unafanya the same mistake over and over na anakupa hicho kibandiko kama jina la mkosaji wa kila siku.

Si kweli kwamba unaweza kufanya makosa yaleyale kila siku, muda wote miaka yote.

WEKA MKAZO KWENYE UWEZO NA SI UDHAIFU

Mwanamke na mwanaume wapo tofauti siku zote na ni mpango wa Mungu kuwa tofauti ili kwa tofauti tuweze kusherehekea uumbaji wa Mungu na ili mke na mume waweze kila mmoja kumridhisha mwenzake.

Huwezi kuwa na mwenzi ambaye ana udhaifu mwingi kuliko uwezo na ukiona ana udhaifu mwingi kuliko uwezo basi tatizo ni wewe si yeye.

3)
Ni muda sasa makelee yamezidi kuwa hakuna wa kuoa au hakuna wa kuolewa,hizi kelele zimezidi na hii ni dalili kuwa kuna tatizo mahali na sidhani kama kuna jitihada za kutosha zinafanyika kutatua hili tatizo

Kimsingi karibu watu wengi tu wanahitaji ndoa na tatizo linakuja lilelile nani wa kuoa/olewa?Tutake tusitake kama kweli tunahitaji ndoa ni lazuma tubadilike hasa kimtazamo

Maendeleo yameongezeka sana na muingiliano wa tamaduni umeleta balaa na mema mengi sana,kama kuna mtu anahitaji kuwa na ndoa iliyoimara hana budi kwanza kubadilika na kukubaliana na utamaduni anaoishi ili kuweza kuingia kwenye ndoa kama hutaki ndoa basi baki hivyo hivyo

Hapa nitaeleza yale ninayodhani kuwa kama tukiyazingatia basi yanaweza kutusaidia sana kubadilika na nitayaweka kwenye makundi mawili kwa kutofautisha jinsia

WANAUME

Kwenye suala hili Wanaume tumekuwa na matatizo kadhaa na haya hapa ni baadhi

Elimu

Elimu imekuwa tatizo sana linapokuja suala la ndoa,kijana akimaliza elimu hasa kuanzia O level au chuo anaanza kuwa na mawazo kuwa wale ambao hawajasoma sio wife material na hawafai kabisa kuolewa
Hili liunaweza kuwa na ukweli lakini ni mdogo sana kwani ili mtu awe bora kwenye ndoa sio lazima awe ameenda sana shule,ushahidi wa hili ni ubora wa mama zetu ambao wengi kama walikuwa wamesoma sana basi ni darasa la saba na sisi ambao ni wa siku nyingi kidogo basi mama zetu wengi walikuwa hata shule hawajaenda lakini hilo halikumfanya asiwe mama bora

Na hata hawa viongozi wetu tunaowasifia na kuwaita kielelezo cha Waafrika au waasisi wa mataifa yetu wengi wao walilelewa na wazazi ambao hawakupata kabisa elimu au walipata kidogo sana kutokana na mambo mengi sana.Sitayazungumzia hayo yaliyosababisha wasipate elimu kwani hiyo ni mada nyinmgine lakini kitendo cha kukosa elimu hakikuwafanya wakawa mama wasiofaa na matokeo yake malezi yao ndio hayo yamewafanya hao kuwa viongozi bora

Ukisasa

Hili ni tatizo jingine kubwa sana la vijana,vijana siku hizi wamekuwa na mambo ya ukisasa sana hadi ile hadhi ya kiume imepotea kabisa na kumekuwa hakuna tofauti na wanawake labda unaweza kuiona tofauti hiyo kwenye mavazi tu

Vijana siku hizi wanapaka poda,wanatinda nyusi yaani unakuta vijana wanakabana makoo na warembo kwenye yale maduka ya urembo.Siku hizi huwezi kujua hii dresing table kama ni ya mwanamke au mwanaume yaani imejaa vipodozi hadi karaha

Sisemi kuwa wanaume au vijana wasijipende lakini kuna limitation ya haya mambo,siku hizi vijana wanatembea na vioo kwenye walllet zao utadhani wakina dada,ukimkuta ofisini kaweka poda,hii ni laana kabisa na kamwe usidhani kuwa kuna mwanamke yeyote yule anaejitambua atakubali kuolewa na mwanaume au kijana wa aina hii

WANAWAKE

Wanawake nao wana yao

Elimu

Tukubali au tusikatae hili ni tatizo.Wanawake wana matatizo yanayofanana na ya vijana kwenye hili lakini kwa wanawake linaonekana kama ni kubwa sana,Siku hizi mwanamke akishafika O level au zaidi basi huyo anawaona watu wengiine kama sio watu sanasana wanaume hili ni tatizo lakini ukiliangalia kwa undani linaonekana tatizo hili linaanzia kwenye asili

Kiasili mwanamke ameumbwa kuwa chini ya mwanaume hili ni kweli mtake msitake na mwanamke yoyote yule akiwa na uwezo kifedha kumzidi mwanaume au akiwa na elimu kumzidi au kwa kifupi akiwa na chochote kile cha kumzidi mwanaume basi mwanamke huyo humuona mwanaume huyo kama sio mwanaume vile,hili ni suala la kimaumbile zaidi,lakini ni tatizo

Kama mwanamke kaumbwa hivi basi ni wazi kuwa hakustahilio kukipata kile kinachompa tatizo kwenye maisha yake ya leo,najua mnaweza kutokukubaliana na hili lakini ki ukweli mwanamke ndivyo alivyoumbwa.Sisemi mwanamke asisome lakini kuna haja ya kuliangalia hili kwa makini kama kweli tunahitaji kuwe na ndoa au familia zile ambazo tunazitamani

Kama mwanamke atakuwa na degree basi huyo ambae atamuona na kuishi nae kwa angalau amani basi ni mwenye elimu kubwa zaidi yake,sasa jiulize ni wangapi wanaelimu ambao watatosha kuwaoa hawa wanawake wanaomaliza chuo kila uchao?Kila siku ukiangalia ndoa ambazo zina amani ni zile ambazo either mwanamke hajasoma kwa kiwango cha kufikia form 6 au kama mwanamke mesoma basi ameamua kuishi kimazoea tu

Sisemi kuwa wanawake ambao hawajasoma hawana matatizo na pia sisemi kuwa kila mwanamke ambae amesoma ana matatizo lakini ninachotaka kusema hapa ni kuwa wengi wa wanawake ambao wamesoma wana matatizo

Fedha
Hili jambo limegawanyika kwenye makundi mawili

1: Kuna wanawake ambao wamefanikiwa kupata mafanikio ya kifedha
2:Kuna wanawake ambao kwao hela ni kila kitu

Wenye mafanikio kifedha

Hawa kuolewa imekuwa tatizo sana kwako kwasababau kwanza wako busy sana na shughuli zao na kama ujuavyo sisi Waafirka tunahitaji mwanamke ambae ukirudi nyumbani unamkuta na ukute amekupikia chakula,sasa huyu ni mara chache sana utaweza kumkuta nyumbani na kukupikia chakula

Chakula cha kupikiwa na mke kinanoga jamani sasa haya mabo ya kupikiwa na beki tatu tutayaweza wapi?

Hili ni tatizo kubwa sana kwa aina hii ya wanawake lakini kuna tatizo lingine ambalo limekuwa likiwatatiza sana hawa wanawake ambao wanamafanikio ya kifedha,tatizo hili ni kama hilo la wenye elimu,wanakwaida ya kuwaona wanaume ambao wamewaziki kipato kama vile sio wanaume na tatizo hili nalo ni la kimaumbile zaidi lakini kikubwa sana wanawake hawa wanashindwa kuolewa mara nyinmgine hata kama atakuwa hana matatizo hayo kwa sababu ya wanaume kuwaogopa wanawake hawa

Sasabau za kuwaogopa zinatofautiana kutoka kwa mwanaume mmoja hadi mwingine lakini kitendo cha mwanamke kuwa na mafanikio kifedha ni tatizo kwao na ni sababu mojawapo ya kutokupata mume

Wanawake ambao wanaona fedha ni kila kitu

Hawa nao hili limekuwa ni tatizo kwasababu wamejikuta wakikaa muda mrefu sana biula kuolewa kwasababu wanawatafuta sana hawa wanaume wenye hela na bahati mbaya sana hawa ni wachache na wengi wao wanakuwa wameoa na hivyo wanawake hawa kuishia kuwekwa nyumba ndogo tu

Kingine ni kuwa wanawake hawa hawataki kuwajibika na kukubali kuolewa na kuyatengeneza maisha yao wanataka wakute maisha yameshatengenezwa tayari,kwanini usinyanyaswe na mwanaume wakati umemkuta tayari ana kila kitu na hata hujui aliteseka vipi kuzipata hizo hela?
Kama unataka heshima nenda kaolewe na mwanaume ambae haja setle kisha muanzie chini au hamjui kuwa maisha yanatengenezwa?

Pia wasichokijua wanawake ni kuiwa hawa wanaume wenye hela wengi utakuta hawakufika hapo peke yao,yaani unakuta kuna mwanamke nyuma yao na baada ya kupata tu fedha waliamua kuwaacha hawa wanawake waliowasaidia kufika walipofika na kutafuta wale wanaodhani ni sawa kuwa nao kwenye mafanikio,sasa mwanamke ambae atakutana na mwanaume wa aina hii atajikuta akitumiwa na kuachwa kwasababu hawa watu tabia yao siuo nzuri kiujumla na mara nyingi wanawake hawa huishia kuzalishwa na hawa wanaume na mwishowe kuachwa na kuja kupata shida sana kupata mume kwani wanaume nao siku hiziz ni wachache walioko tayari kuoa mwanamke mwenye watoto

Jamani sisemi mwanaume akiwa hana hela ni mwema,wapo mabazazi wengi tu lakini linapokuja suala la mafanikio ya kifedha ni bora mwanamke ukawa makini sana unapokutana na mwanaume wa aina hii

Ukisasa
Wanawake wamejikuta wakikaa muda mwingi sana bila kupata waume wa kuwaoa na kuishiwa kuchezewa tu kwasababu ya tatizo hili la ukisasa

Wanawake mnatakiwa mjue kuwa mwanaume yoyote yule ambae ni husband material ni lazima kuna mambo yanamfanya hivyo

Husband material anakuwa na sifa zifuatazo
Anamjali mkewe
Anajali watoto
Ni msikivu
Mpole kiasi
Mbahili kiasi
N.k


Wanawake au mabinti wanatakiwa watambue kuwa mwanaume yoyote yule mwenye sifa hizo mara nyingi huonekana kama wa kizamani hivi na mabinti mwanaume wa hivyo humuita mshamba na hawamuitaji,Hawamutaji kwasababu mabinti wengi sana wanahitaji kwenda salun za gharama,kwenda kujirusha kila w/end,kutumia vipodozi na mavazi ya gharama,hawataki kupika n.k

Halafu cha kushangaza wanawake hao hao wanadai eti wanahitaji ndoa,ni ndoa gani hiyo?

Wengi wa aina hii ya wanawake huishia kuangukia kwenye mikono ya wanaume mabazazi na kuishia kufanikiwa kutumia hela za hawa mabazazi lakini ndoa haipo

Hakuna mwanaume yoyote yule mwenye uchungu wa familia anaehitaji maendeleo atakaekubali kuishi na mwanamke wa aina hiyo kama unahitaji ndoa iliyo imara kubali kubadilika

Yapo mengi sana ya musema lakini kwa sasa hayo yanawafaa

Ninachotaka kuwaambieni ni kuwa kama kweli tunahitaji kuzipata ndoa zile ambazo tunaishia kuzisikia kwenye hadithi basi hatuna budi kubadilika,najua hiki ni kitu kigumu sana lakini ndio dawa yenyewe
 
Ukiingia kwenye ndoa ili kutafuta furaha umeliwa. Na watu wengi wamefanya kosa hili. Wengi wanadhani ndoa ni sehemu ya kutafuta furaha na utifilimu (completion) - it's wrong.
Ndoa nimuunganiko wa watu wawili wenye furaha na walio kamili wanaunganika na kuwa mwili mmoja. Kwenye ndoa unaingia kuchangia sio kupata.

Kujibu swali lako ni kwamba ili kuwe na furaha kwenye ndo yako ni wewe kuwa na furaha kwenye maisha yako kabla ya ndoa na kumtafuta mwenye furaha na anayejitegemea kikamilifu.
 
Marriage quotes
Marriage is not a word. It is a sentence--a life sentence.

Marriage is love. Love is blind. Therefore, marriage is an institution for the blind.

Marriage is an institution in which a man loses his Bachelor's Degree and the woman gets her Masters.

Marriage certificate is just another word for a work permit.

Marriage is not just a having a wife, but also worries inherited forever.

Marriage requires a man to prepare 4 types of "rings":
* The Engagement Ring
* The Wedding Ring
* The Suffe-Ring
* The Endu-Ring
Married life is full of excitement and frustration:
* In the first year of marriage, the man speaks and the woman listens.
* In the second year, the woman speaks and the man listens.
* In the third year, they both speak and the neighbors listen.

It is true that love is blind but marriage is definitely an eye-opener.

Getting married is very much like going to the restaurant with friends. You order what you want, and when you see what the other fellow has, you wish you had ordered that.

It's true that all men are born free and equal, but some of them get married!

There was this man who muttered a few words in the church and found himself married. A year later he muttered something in his sleep and found himself divorced.

A happy marriage is a matter of giving and taking; the husband gives and the wife takes.

Son: How much does it cost to get married, Dad?
Father: I don't know son, I'm still paying for it.

Son: Is it true? Dad, I heard that in ancient China, a man doesn't know his wife until he marries.
Father: That happens everywhere, son, everywhere!

There was a man who said, "I never knew what happiness was until I got married...and then it was too late!"

Love is one long sweet dream, and marriage is the alarm clock.

They say when a man holds a woman's hand before marriage, it is love; after marriage, it is self-defense.

When a newly married man looks happy, we know why. But when a ten-year married man looks happy, we wonder why.

There was this lover who said that he would go through hell for her. They got married, and now he is going through hell.

My wife and I have the secret to making a marriage last

The last fight was my fault. My wife asked,
"What's on the TV?"...I said, 'Dust!"

15. In the beginning, God created earth and rested.
Then God created man and rested. Then God created
woman............
Since then, neither God nor man has rested.

16. Why do men die before their wives?...............
Because they want to
 
Jamani naombeni kujua wanawake wanapenda kufanyiwa nini na waume zao. Na wanaume pia wanapenda kufanyiwa nini na wake zao. Nataka kujua experience ya watu tofauti ili nijue. Wenye ndoa zenye furaha na amani zisizokuwa na constant arguments pia nini siri yake? Roles gani kila mtu anaplay kuhakikisha marriage inakuwa bed of roses. I mean kona zote, family responsibilities, sex life, entartainment e.g outings, gifts, communication, Care etc. Kila kitu kinatakiwa kifanyweje ili kuwepo na happines ndani ya ndoa.

...jifanye mjinga hata pale unapoona upo right, kwani dawa ya suluhu ya mapenzi ni kutokuwa mshindi wala mshindwa.
 
Furahia kutoa zaidi kuliko kupokea,
Jishushe zaidi kuliko kujikweza
In short -just do to your spouse what you would like them to do to you and don't do what you wouldn't like someone else to do to you.

In that way you wont be disappointed that much.

Ukitegemea a bed of roses, you will be in for a surprise.
 
Lasthope,

Kwanza wewe useme unataka ufanyiwe nini katika ndoa yako wewe na mkeo? na kama hujaoa je, ungependa ufanyiwe nini na mkeo mtarajiwa?
 
Ndoa ni muungano wa wapenzi, kufanyia au kufanyiwa hakutokuja kama hakuna mapenzi.
 
Ndoa ni muungano wa wapenzi, kufanyia au kufanyiwa hakutokuja kama hakuna mapenzi.

Haswaaa! vinginevyo hamstahili kufunga pingu za maisha. Na wako watu wengi tu ndani ya ndoa ambao wana furahia maamuzi yao ya kufunga pingu za maisha. Hata wakipewa nafasi nyingine tena ya kuendelea na ukapera au kuwa wana ndoa wengi wangechagua maisha ndani ya ndoa
 
Lasthope,

Kwanza wewe useme unataka ufanyiwe nini katika ndoa yako wewe na mkeo? na kama hujaoa je, ungependa ufanyiwe nini na mkeo mtarajiwa?

Mimi ningependa kuona najaliwa, nahusishwa katika kila jambo. In short yale maisha ya siku za kwanza za mapenzi na excitement viendelee bila kupungua. Lakini hii ndiyo hali halisi kwenye ndoa? Wenye experience please tuelezeni.
 
Furahia kutoa zaidi kuliko kupokea,
Jishushe zaidi kuliko kujikweza
In short -just do to your spouse what you would like them to do to you and don't do what you wouldn't like someone else to do to you.In that way you wont be disappointed that much.Ukitegemea a bed of roses, you will be in for a surprise.

This is easier said than done. Kwa mfano unajisikiaje ukiwa wewe ndo unamnunulia mwenzio zawadi kila mara, yeye wala hata hajisumbui na si kwamba hana pesa ila tu anona si muhimu or whatever, unakuwa wa kwanza kukomunicate everytime yeye wala, baada ya ndoa habari ya outing haoni umuhimu , anona kama ni anasa, je bado utakuwa na moyo wa kufurahia one way bila kurudishiwa?Je utakuwa na moyo huo?
 
Ndoa ni muungano wa wapenzi, kufanyia au kufanyiwa hakutokuja kama hakuna mapenzi.

Ndio kitu ninachouliza hapa mama, je ni kweli mapenzi yale yaliwasukuma kuoana ambayo naamini yalichangiwa na vitu vidogo vidogo vingi kama nilivyomention kwenye post ya kwanza kabisa huwa yanaendelea? Je kama vitu vile vikipuuzwa vina athari gani katika ndoa.
 
Ndio kitu ninachouliza hapa mama, je ni kweli mapenzi yale yaliwasukuma kuoana ambayo naamini yalichangiwa na vitu vidogo vidogo vingi kama nilivyomention kwenye post ya kwanza kabisa huwa yanaendelea? Je kama vitu vile vikipuuzwa vina athari gani katika ndoa.

Kuendelea kupata vitu hivyo inategemea mwanzo wenyewe... je wahusika walijilazimisha kwenda an extra mile au they were doing it naturally? Wengi huficha makucha yao mwanzo na wakioana ndo huyatoa... wengine wanachoka kuendelea kukimbia an extra mile maana hakuna motivation for doing so nakadhalika.Ndoa si mchezo ati!
Kitu kingine kila ndoa inasimama au kuanguka kutegemeana na wahusika wanacheza vipi karata zao.... the bottomline is give and take...wewe ukiwa hutoi usitegemee kupata...
 
Haswaaa, WOS,
Njoo kwenye ndoa na raha zako, umpate mwenye raha zake, basi raha+raha=2raha.
unafiki+unafiki=2unafiki.
vijana wengi wanaishi maisha artificial, wakiambiwa na wazazi au wakubwa uzuri si sura wanaona kama wanaonewa wivu au wananyimwa uhuru (wa kuchagua nimpendaye)
Kuna thread niwahi kuanzisha huko nyuma kwamba ujanja uko kwenye kuchagua, isome.
Kama wengine walivyosema awali, amua kuwa unamchagua mtu ambaye uko tayari kumpa kila uwezacho hadi mwisho, fanya uamuzi huo mapemaaaaa.
Kama unaingia kwenye ndoa ukitagemea kupata basi umeshakosa!!

Kama uko tayari kwenye ndoa basi vuta pumzi, fanya uamuzi wa kuamua kumpa mwenzi wako penzi kama ANAVYOTAKA YEYE.
Amua kwa moyo mweupe kwa hiari yako kumpenda. Basi, mengine ni ziada
 
I hear you Haika...
Haya mambo ni mazito..watu huyachukulia kwa wepesi ajabu.... wengine huingia kwenye ndoa na malengo tofauti..pesa, uzuri wa sura n.k. wakisahau kuwa hayo huisha au hugeuka si ishu tena.Imagine unaingia kwa gia ya kwamba umeoa Miss sijui wapi...siku umiss umeisha... thru natural processes au ugonjwa sijui utamlilia nani..au pesa zimeisha ndo hapo ndoa utaiona chungu.Bora wote muwe genuine na muoane without that "I love you because of......." oana na mtu because you just love him/her. hapo penzi na pendo litamea kadiri mtakavyolipalilia a kulitunza.Kumbuka MARRIED LOVE IS A PLANT WHICH NEEDS TO BE TAKEN CARE OF.....mwenye masikio na asikie.
 
Binafsi nafikiri sababu za kufunga ndoa na tabia za watu wakiwa ndani ya ndoa ndio chanzo cha mafanikio au kuvunjika kwa ndoa.

Ndoa nyingi za vijana huwa ni kutokana na sababu zifuatazo:
1. Mimba isiyopangwa
2. Umri wa kuoa umefikwa
3. Nina kazi, pesa, uwezo sasa iliyobaki ni kuwa na mke/mume
4. Nitambulike katika jamii
5. Fulani ni mzuri wa sura, anavutia n.k.

Wengi hawafikirii kuwa katika ndoa kuna masuala ya msingi ya kupatana kabla ya kufunga hizi ndoa.

1. Matumizi ya fedha
2. Mtaishi wapi
3. Ndugu na marafiki
4. Maisha ya watoto- elimu, afya, mahitaji
5. Wasaidizi/wafanyakazi wa nyumbani

Wanaume mara nyingi hufikiria haya na ndio inayowaletea matatizo sana badaye;

1. Mke ni mali yangu
2. Mke lazima afuate kila nitakachosema/amua
3. Mimi ni mwenye maamuzi ya mwisho
4. Heshima ni lazima kwangu hata nikiwa nimekosea mimi
5. Ndugu yangu ni zaidi ya mke wangu

Wanawake mara nyingi na wao hukosea yafuatayo;

1. Ndugu yangu ana haki kuliko ndugu wa mume wangu
2. Ndugu wa mume wangu ni wabaya wangu hata iweje
3. Fedha ya mume ni yangu ila ya kwangu ni yangu
4. Lazima nisikilizwe mimi

Mara zote matatizo yanatokana na utofauti wa ideals kati yetu. Wanaume wengi wanaoa kwa kutumia rules za utamaduni ambao mara nyingi hutumika kukandimiza wanawake na kumuona hasitahili. Wanawake na wao wameamka nakujua haki zao.

Cha muhimu ni kuhakikisha tunaelimishana mapema kabla ya kuingia katika hizi ndoa maana majukumu yanaongezeka kadri ya siku. Kutazama mlipotoka ni muhimu sana ili mjue kubadilika kwa nyakati.

Hakuna ndoa inayo pay-off kama ndoa ambayo mwananume atampenda mkewe na mwanamke atamheshimu mumewe. Ila kumbuka ili kupata vyote hivyo lazima mchangie yawezekane msitegemee yatatokea tu.

Marriage is a full time job.
 
Nafikiria ndoa nyingi hazidumu due to the fact that people take a short time to know each other well enough, and most men these days look at outside beauty and not the inside beauty, this then brings competition as one opts to marry somegirl more beautiful than his brothers, relative or even a friends ... external influence also sets in ... family and friends with a lot of pushing ... mwanamke atalalamika mpaka ... some even seek traditional doctors help to achieve this .... eventually you get married ... kila kitu perfect at the beginning ... everyone of you willing to go extra mile ... unajua tena ... mara tiiiiiii you cannot pretend anymore .... bse you eventually find out you did not love him in the first place and you cannot take it anymore ...

Jambo muhimu sana nafikiria ... ni nyote kuwa tayari bila hiyari kuoana .... halafu i advocate pia kwa kuchunguzana kwanza even approach ya kuwa wapenzi ... 1 would also urge men not to look at outside beauty ... uzuri wa ndani ni tulivu na tamu kuliko wanavyofikiria ... dont mind mtu akikuambia mume wako au mkeo anasura mbaya ... kwani unajuwa kabisa kwamba roho kama yake kamwe hatoipata
 
Nafikiria ndoa nyingi hazidumu due to the fact that people take a short time to know each other well enough, and most men these days look at outside beauty and not the inside beauty, this then brings competition as one opts to marry somegirl more beautiful than his brothers, relative or even a friends ... external influence also sets in ... family and friends with a lot of pushing ... mwanamke atalalamika mpaka ... some even seek traditional doctors help to achieve this .... eventually you get married ... kila kitu perfect at the beginning ... everyone of you willing to go extra mile ... unajua tena ... mara tiiiiiii you cannot pretend anymore .... bse you eventually find out you did not love him in the first place and you cannot take it anymore ...

Jambo muhimu sana nafikiria ... ni nyote kuwa tayari bila hiyari kuoana .... halafu i advocate pia kwa kuchunguzana kwanza even approach ya kuwa wapenzi ... 1 would also urge men not to look at outside beauty ... uzuri wa ndani ni tulivu na tamu kuliko wanavyofikiria ... dont mind mtu akikuambia mume wako au mkeo anasura mbaya ... kwani unajuwa kabisa kwamba roho kama yake kamwe hatoipata

Inafurahisha na kutia Moyo unaposikia maneno mazuri kama haya yanatoka kwa Mwanamama.Kama una mtoto wa kike tuwasiliane Naima,najua Mwanangu wa kiume atapata Mke mzuri....maana Bibi (Nyanya) yangu alinambia kuwa "Binti ni Taswira ya Mamaye" .
 
Inafurahisha na kutia Moyo unaposikia maneno mazuri kama haya yanatoka kwa Mwanamama.Kama una mtoto wa kike tuwasiliane Naima,najua Mwanangu wa kiume atapata Mke mzuri....maana Bibi (Nyanya) yangu alinambia kuwa "Binti ni Taswira ya Mamaye" .

Ninao tena wengi tu Mkwe ... uje na ngombe tu ...maana hawanywi maji wanakunywa maziwa tu.

Mungu akukuzie mwanao .. na ampe mke mwema ... ni vizuri kwamba umepata mwongozo ... naye mda ukifika umkalishe chini umpe mlolongo mzima na ushauri mzuri pia kuhusu kuchagua mke ... zaidi ya yote awe mcha Mungu, mwenye aibu na tabia nzuri ...
 
Jamani naombeni kujua wanawake wanapenda kufanyiwa nini na waume zao. Na wanaume pia wanapenda kufanyiwa nini na wake zao. Nataka kujua experience ya watu tofauti ili nijue. Wenye ndoa zenye furaha na amani zisizokuwa na constant arguments pia nini siri yake? Roles gani kila mtu anaplay kuhakikisha marriage inakuwa bed of roses. I mean kona zote, family responsibilities, sex life, entartainment e.g outings, gifts, communication, Care etc. Kila kitu kinatakiwa kifanyweje ili kuwepo na happines ndani ya ndoa.


siri ya furaha;...hutagundua thamani ya unachokitaka. ndoa nayo ndio hivyo hivyo... ukioa/kuolewa ndipo utapogundua kama ni kweli ulikuwa unamhitaji au ulikuwa ukimtamani tu!

furaha maishani mwenu ni sawa na mbegu unayoipanda mpaka kuvuna matunda ya mmea huo. Mapenzi nayo ndio hivyo hivyo, hasa ukizingatia kuna 4seasons of happiness vile vile, kama ilivyo Spring, Summer, Autumn, na winter...

 
Back
Top Bottom