Familia inateseka sana. Nisaidieni natafuta Kazi, Kibarua

Habari wana JF,

Mie kijana wa kiume, naishi Dodoma! Nina mke na mtoto mchanga wa miezi 4. Kitaalum ni muhitimu wa Bachelor ya Computer Science, na nilikuwa nimeajiriwa sehem lkn tulipunguzwa kipindi kile janga la corona limepamba moto.

Sina kazi maalum kwa muda sasa, naunga unga tu kiukweli, nikibahatisha kupata kazi ya mtu binafsi mfano kutengeneza website au la kidogo imekuwa ikinibeba hasa kulipia kodi, lkn sijapata hizo kazi kitambo sasa! nimejaribu sana na bado naendelea kutuma maombi lkn sijafanikiwa, hali imekuwa ngumu kweli kweli kwetu! Nafanya vibarua sometimes hadi vya kubeba zege japo tu familia ipate mlo hasa mke anaenyonyesha!

Lakini saa nane kasoro hii usiku naandika hapa, tumelala njaa, leo nimejaribu vibarua bila mafanikio, hatuna hata sh. mia hapa ndani, imeniuma sana ndio maana nimekuja kwenu kuomba kazi, kibarua chochote halali hata cha kipato kidogo tu!

Mtoto wa miezi minne imebidi tu aanze kunywa uji maana mlo wetu mmoja kwa siku mama anakosa maziwa ya kutosha!

Mwenye chumba kanivumilia hadi kachoka kaniambia nikabidhi tu chumba, japo hii laptop naitumia kwa kazi zangu, lakn kama kuna mteja wana JF naiuza laki3, au kama kuna mtu anakopesha niiweke bond, atunusuru tafadhalini tunatolewa kwenye hii nyumba!

Nipo tayari kuja popote kufanya kazi/kibarua chochote halali! Naombeni sapoti nateseka sana, hasa huyu mzazi kulala njaa hivi inanipa stress sana!

Kwa mawasiliano, namba zangu 0767 960 255 au 0629 531 358.

Natanguliza Shukrani na Mungu atubariki!
Pole sana mkuu maisha ndivyo yalivyo changamoto hayo yote yatapita Muombe Mungu
 
Yametupata mengi hapa JF. Bado utetezi wako haujafua dafu. Huwezi kulala njaa na asubuhi ukawa unaendesha baiskeli kijana! Niendelee?
Kiongozi naona unayo shida... Ila endeleeni labda upo kumpima mwamba ..... Na pengine labda wewe hukuwahi kuexperience hayo maisha... Ila acha kabisa kwasisi tuliopitia tunaelewa anachokiongea! Ngoja ninyamaze ....

Ila nakuomba tu, Kama huna Imani na mwana achana nae, acha sisi tumsaidie...
 
Kidogo wewe umenielewa
 
Wait a minute, nadhani nilijaribu kumsaidia kwa kumtafutia kazi maana nilijua mtu anayehitaji mtaalam kama yeye anavyodai. Unajua what happened? Tusiwe watu wa kukurupuka na kutetea kama huyo aliyeniita mjinga
what happened ndugu?
 
waweza tiririka kidogo mkuu...utuokoe baadhi yetu tusije dumbukia kubaya
 
Hapa JF ni mengi yametupata. Unampeleka mtu kwa mnaoheshimiana unakuta ni mbabaishaji au ni tapeli. Kabla ya kukubali kirahisi ukatapeliwa ni bora kujiridhisha. Unajua ukimuudhi mtu ndipo unamjua. Mfano akina kibatala wakiwa mahakamani utasiki, wewe si ni kikojozi, unahamaki - hapo ndipo ukweli unautoa. Tunafaa kuwa waangalifu maana unaambiwa kosa si kosa ila kurudia kosa. Nadhani angalau wenye akili za kiutu uzima wamenipata.
 
Hapa JF ni mengi yametupata. Unampeleka mtu kwa mnaoheshimiana unakuta ni mbabaishaji au ni tapeli. Kabla ya kukubali kirahisi ukatapeliwa ni bora kujiridhisha. Unajua ukimuudhi mtu ndipo unamjua. Mfano akina kibatala wakiwa mahakamani utasiki, wewe si ni kikojozi, unahamaki - hapo ndipo ukweli unautoa
Wanasema ukweli mwingi utaupata either mtu akiwa na HASIRA au kwenye Mvinyo ...
 
Hapa JF ni mengi yametupata. Unampeleka mtu kwa mnaoheshimiana unakuta ni mbabaishaji au ni tapeli. Kabla ya kukubali kirahisi ukatapeliwa ni bora kujiridhisha. Unajua ukimuudhi mtu ndipo unamjua. Mfano akina kibatala wakiwa mahakamani utasiki, wewe si ni kikojozi, unahamaki - hapo ndipo ukweli unautoa. Tunafaa kuwa waangalifu maana unaambiwa kosa si kosa ila kurudia kosa. Nadhani angalau wenye akili za kiutu uzima wamenipata.
Hakuna lolote unalozungumza zaidi ya tuhuma tu. Kama nia yako ilikuwa kumchunguza usingeanza kwa kumuita tapeli hadharani. Amekuchallenge zaidi ya mara moja kuthibitisha tuhuma zako unaongea ngonjera tu. Amekupa hadi taarifa zake zote na wapi unaweza kumpata na ukasema una mtu Dodoma wa kuthibitisha.

Usipende kuingilia njia ya mnyonge anayehangaika. Kuna kitu kinaitwa KARMA ndugu yangu....nakwambia tena kuna KARMA kwenye huu ulimwengu na inafanya kazi.
 
Dah pole sana mkuu
Habari wana JF,

Mie kijana wa kiume, naishi Dodoma! Nina mke na mtoto mchanga wa miezi 4. Kitaalum ni muhitimu wa Bachelor ya Computer Science, na nilikuwa nimeajiriwa sehem lkn tulipunguzwa kipindi kile janga la corona limepamba moto.

Sina kazi maalum kwa muda sasa, naunga unga tu kiukweli, nikibahatisha kupata kazi ya mtu binafsi mfano kutengeneza website au la kidogo imekuwa ikinibeba hasa kulipia kodi, lkn sijapata hizo kazi kitambo sasa! nimejaribu sana na bado naendelea kutuma maombi lkn sijafanikiwa, hali imekuwa ngumu kweli kweli kwetu! Nafanya vibarua sometimes hadi vya kubeba zege japo tu familia ipate mlo hasa mke anaenyonyesha!

Lakini saa nane kasoro hii usiku naandika hapa, tumelala njaa, leo nimejaribu vibarua bila mafanikio, hatuna hata sh. mia hapa ndani, imeniuma sana ndio maana nimekuja kwenu kuomba kazi, kibarua chochote halali hata cha kipato kidogo tu!

Mtoto wa miezi minne imebidi tu aanze kunywa uji maana mlo wetu mmoja kwa siku mama anakosa maziwa ya kutosha!

Mwenye chumba kanivumilia hadi kachoka kaniambia nikabidhi tu chumba, japo hii laptop naitumia kwa kazi zangu, lakn kama kuna mteja wana JF naiuza laki3, au kama kuna mtu anakopesha niiweke bond, atunusuru tafadhalini tunatolewa kwenye hii nyumba!

Nipo tayari kuja popote kufanya kazi/kibarua chochote halali! Naombeni sapoti nateseka sana, hasa huyu mzazi kulala njaa hivi inanipa stress sana!

Kwa mawasiliano, namba zangu 0767 960 255 au 0629 531 358.

Natanguliza Shukrani na Mungu atubariki!
pole kijana,una ujuzi gani mwingine, na mimi nilipitia mazingira kama yako ,ila nilisota miaka miwili huku sijielewi.Jitahidi kuwa karibu na MUNGU zaidi,na huu ni wakati wa kutoa zaka,na kufunga na umuombe MUNGU akuonyeshe njia.Nimeuliza ujuzi kwasababu kwa wakati huu ,ukipata hata kazi ya udereve chukua,,ungekua dsm ungeweza kufanya hata dereve wa uber .Ila usikate tamaa hamna jambo ambalo linakuja mbele yako na MUNGU hakuonyeshi njia.
 
Naomba Malumbano na ndugu kolola said: yaishe,tushaliongea via phone na tumemalizana,kiufupi tu ni kuwa aliniunganisha na mtu anayehitaji mtu wa IT,huyo mtu akanipigia simu mapema asubuhi,na mie niliondoka asubuh hyo nikaenda nje kidogo ya mji kufuatilia maziwa,nilikuwa kwenye baiskeli na kulikuwa na mvua sikusikia hyo call! Badae nilikuta missed call kadhaa za watu tofauti,Hata hivyo plan yangu ilikuwa nikitulia nianze fanya mawasilino nao,na hapo nikawa busy kuna walohitaji CV,walohitaji vyeti,nikatakiwa kutuma emails,wengine wakani ni interview via phone,call ya jamaa wa tigo ikaingia akinidadisi kama naweza fanya freelencer ya post paid vocha sales,inshort nilikuwa kwenye conversations nyingi,sasa ndugu yangu kolola said akaona siko serious,lkn tushaongea na niombe kwa heshima,mvutano uishe na tulipokwazana tusameheane!
 
Asante ndugu,pole nawe kwa yote ulopitia!hapa vijana tuna cha kujifunza,kuwa na vitu muhimu kama Leseni,kuna mwana JF ana bajaj na ni biashara nzuri sana hapa Dodoma,lkn imekuwa ngumu kwangu sababu sina leseni!kiukweli namtumainia Mungu..
 
Naomba Malumbano na ndugu kolola said: yaishe,tushaliongea via phone na tumemalizana,kiufupi tu ni kuwa aliniunganisha na mtu anayehitaji mtu wa IT,huyo mtu akanipigia simu mapema asubuhi,na mie niliondoka asubuh hyo nikaenda nje kidogo ya mji kufuatilia maziwa,nilikuwa kwenye baiskeli na kulikuwa na mvua sikusikia hyo call! Badae nilikuta missed call kadhaa za watu tofauti,Hata hivyo plan yangu ilikuwa nikitulia nianze fanya mawasilino nao,na hapo nikawa busy kuna walohitaji CV,walohitaji vyeti,nikatakiwa kutuma emails,wengine wakani ni interview via phone,call ya jamaa wa tigo ikaingia akinidadisi kama naweza fanya freelencer ya post paid vocha sales,inshort nilikuwa kwenye conversations nyingi,sasa ndugu yangu kolola said akaona siko serious,lkn tushaongea na niombe kwa heshima,mvutano uishe na tulipokwazana tusameheane!
Hukuongea na mimi bali jamaa yangu na nasikia na kazi umepata au siyo?
 
Sijasema nimeongea na wewe,nimesema tushaliongea limeisha!kuhusu kazi kasema ataongea nawe then atanijulisha,ila details za kazi husika yes tushaziongea!
 
Hakuna lolote unalozungumza zaidi ya tuhuma tu. Kama nia yako ilikuwa kumchunguza usingeanza kwa kumuita tapeli hadharani. Amekuchallenge zaidi ya mara moja kuthibitisha tuhuma zako unaongea ngonjera tu. Amekupa hadi taarifa zake zote na wapi unaweza kumpata na ukasema una mtu Dodoma wa kuthibitisha.

Usipende kuingilia njia ya mnyonge anayehangaika. Kuna kitu kinaitwa KARMA ndugu yangu....nakwambia tena kuna KARMA kwenye huu ulimwengu na inafanya kazi.

Huyu hayajamkuta bado, binafsi naelewa sana anachopitia mtoa mada...mimi yamenikuta naugulia mpaka leo hii, sema kinachoniumiza huyu ana familia kwakweli ni extraordinary time kama mtu hayupo vizuri kiakili anaweza ku commit suicide.

Kwa wale wasio na nia ya kumsaidia msiwavunje moyo wenye nia.
 
Hapa JF ni mengi yametupata. Unampeleka mtu kwa mnaoheshimiana unakuta ni mbabaishaji au ni tapeli. Kabla ya kukubali kirahisi ukatapeliwa ni bora kujiridhisha. Unajua ukimuudhi mtu ndipo unamjua. Mfano akina kibatala wakiwa mahakamani utasiki, wewe si ni kikojozi, unahamaki - hapo ndipo ukweli unautoa. Tunafaa kuwa waangalifu maana unaambiwa kosa si kosa ila kurudia kosa. Nadhani angalau wenye akili za kiutu uzima wamenipata.
Umeenda far Zaid,,hata Mimi umenikera. Inatosha kumuamini kijana mwenzetu. Nilimuamink once alivyotaja hizo sehemu na movement zake za biashara. Sometimes to be matured sio kumuweka mtu kwenye excess pressure kama hiyo, ni kufanya critical analysis.
 
Mkuu pole kwa unayopitia.
Ni mapito na kila kitu huwa kina sababu aminj nakuambia
Hebu fuatilia zabibu kule mpunguzi na mbabala ujue kilo wanauzaje huko mashambani naweza nikatoa hela ukawa unanitumia hapa mwanza ,kwa namna iyo unaweza ukapata kibarua Cha kufanya.
Kuna muda nilikuwa nazifuata dodoma nauzia pale karibia na yenu bar ubungo opposite na tanesco.
Watu tuliosoma nao hawakuaniamini wakajua mie ni double agent.
Kama soko liko vizuri tunaweza tukawa tunazipeleka Kenya kule Bei ni nzuri.
Mie nitakaaa kule afu wewe unazituma.
Pia unaweza ukawa na mtu mwenye akaunti ya crdb nikutumie kitu afu atatoa kwa atm makato ni 1200 huko Kuna unafuu namie kimakato.
Pia namie natuma bure crdb to crdb Kuna unafuu wa kunitumia mtu pesa.
Tafuta akaunti ya crdb ninacho kidogo nifanye ibada Mana sio lazima nipeleke kwa gwajima lusekelo ama kakobe ambao wanafuja zaka zetu
Sasa mkuu na sie wenye account za Crdb hatuwezeshani maana account zipo 0.00 , mpaka ya kufungulia ten haimo😅tuwezeshane
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom