Familia hii yahitaji msaada wa kibinadamu NSSF Dodoma darajani Njia panda ya Milembe

Ngapulila

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
838
731
Kwa wenyeji wa Dodoma karibu na Daraja kwenye Njia panda ya kuelekea Milembe na ile Iringa Road inayopita Police Central kwa Upande wa pile kabla ya kuvuka reli Kuna familia inaishi pale kwa karibu mwezi sasa.

Hii n familia yenye watoto watatu wadogo na pamoja na wazazi wao wawili.Familia hii inaishi chini ya mti na wanalala kwa kujisitiri kwa vipande vya maboksi .Kinachosikitisha zaidi n jinsi wanavyopata tabu pindi mvua ikinyesha au jua likiwa Kali ambapo wanapata shida kubwa sana

Wapita Njia wamekua wakiwashangaa kuwaona pale lakini pia kwakuwa wapo pembezoni mwa barabara Nina hakika Polisi wanapita na wanawaona

Kupitia jamiiforums nawaomba Ustawi was jamii Dodoma wafike kuisaidia familia hii.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom